Kama hujajipanga usiache kazi na kukimbilia kujiajiri

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
May 11, 2014
3,268
7,779
Binafsi ni miongoni mwa wahitimu wa shahada ya elimu wa mwaka 2017. Katika kipindi chote Cha kusotea ajira nilijikita kwenye kilimo champunga, huku nikitafuta kazi yakufindisha bila mafanikio.

Kuna jamaa ambao waliingia kwenye biashara na wengine wakitafuta center na kujishikiza huko.

Baada ya miaka miwili yakuajiliwa katika shule fulani jamaa yangu mmoja alinambia anaacha kazi. Madai yake makuu ni kuwa anafanya kazi kubwa na analipwa laki 3 kwa mwezi. Alidai kuwa anaingia kazini saa moja na ktutoka saa kumi na moja na usiku wanarudi mpaka saa tano kila siku isipokua juma pili tu.

Kwakua yupo mkoa wa iringa alidai kua ataacha kazi na kufanya shughuli nyingine ambazo zitampa uhuru wa kutumia muda wake.

Mwaka jana aliacha kazi miezi miwili tu baada ya likizo ya Corona. Mpaka kufikia leo ambapo amemaliza mwaka mmoja nje ya ajira anatamani kupata hata center ya kulipwa hata laki kwa mwezi lakini ndo basi tena.

USIACHE KAZI KAMA HUJAJIPANGA
KUISHI NJE YA AJIRA.
 
Back
Top Bottom