Kama hili ni kweli na siyo Uzushi tu nitaanza kumdharau Mo Dewji na Watendaji wake wa Simba SC wanaomzunguka

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,546
108,876
Ni nani aliyowaambia kuwa Kiufundi (hasa katika Mpira) Timu yako ikiwa imefungwa katika ' Margin ' kubwa ili nayo Kulipiza Kisasi (Kupundua Meza) Wachezaji wanatakiwa waahidiwe Magari ya Kifahari na kila Goli watakalofunga litanunuliwa kwa Tsh 260 Milioni?

Hizi Ahadi ndizo zitafanya Mabeki wa pembeni akina Kapombe na Hussein wasiwe wanakatika hovyo Uwanjani?

Hizi Ahadi ndizo zitafanya Beki za Kati zilizochoka na hazina Kasi Wawa na Onyango safari hii zichangamke na ziwe zinacheza vyema aerial balls ambazo ndilo limekuwa tatizo kubwa la Mabeki wa Simba SC?

Yaani tunaacha kwa muda huu mfupi uliobaki Kutafuta Psychists wakae na Wachezaji wetu Waandamizi ambao wameshaathirika Kisaikolojia baada ya Kufungwa Kiufundi na Kiuwezo na Kaizer Chiefs FC tunakimbilia kutoa Ahadi hizi Kuu Kuu?

Leo Wanasimba tumesahau Dhambi kama hii ilivyotugharimu mwaka 1993 ( kama sijakosea ) ambapo aliyekuwa Mfadhili Mkuu enzi hizo Azim Dewji ( Mpwa kwa Mwekezaji Mo Dewji ) alipotoa Ahadi za Gari za KIA ambazo ziliharibu kabisa Saikolojia ya Wachezaji wa Simba SC kuelekea Fainali ile ya CAF dhidi ya Stella Abidjan FC?

Kuna Mambo ya Kipumbavu yanafanyika katika Soka la Tanzania na Vilabu vyake halafu tusiopendezwa nayo ( akina GENTAMYCINE ) tukikosoa tunaishia Kutukanwa, Kuchukiwa na kuambiwa kuwa ni Mashabiki wa Yanga SC au tuna Chuki na Simba SC na hasa hasa Mwekezaji wake Mohammed ' Mo ' Dewji.

Wakati hivi sasa Klabu ya Kaizer Chiefs wakijiandaa Kusafiri kuja Dar es Salaam wapo Darasani wakisoma Mbinu nyingi zaidi za Kiufundi za Kuikabili na Kuifunga Simba SC Wenyewe Simba SC sasa wanaomba Uwanja wa Mkapa ili Waroge, wafanye Umafia wa 4-4-2 Vyumbani na kutoa Ahadi za Magari ya Harrier na Shilingi Milioni 260 kwa kila Goli (Bao) litakalofungwa.

Mpaka hivi sasa sitaki Kuamini kuwa haya niliyoyasikia ni ya kweli kutokana na ninavyomjua Mwekezaji Mo Dewji na Mtendaji Mkuu Barbara, Mwenyekiti Mangungu na Mshauri Mkuu wa Mwekezaji na Ufundi wa Simba SC (Poti wangu kabisa kutoka Kwetu Mkoani Mara ) Crescentius Magori ila kama ni kweli basi kuanzia sasa nitaanza Kuwadharau wote hawa na watanisamehe kwa hilo ( hili )

Tukishinda Mechi ya marudiano nitafurahi ila tukitolewa (iwe kwa Kuwafunga Goli chache au hata kwa Kufungwa nao tena) GENTAMYCINE nitashukuru zaidi ili tumalizie Viporo vyetu vya VPL na Mechi zilizobaki na za ASFC ili tuchukue Ubingwa kote kote ili sasa Mwekezaji Mo Dewji ajipange zaidi katika Kusajili Wachezaji imara na mahiri wa Kimataifa ambao hawaifikisha tu Simba SC Robo Fainali bali hivi sasa watatufikisha hadi Fainali na Simba SC kuwa Bingwa kabisa.

Dawa Chungu ndiyo nzuri na huponya zaidi na kwa haraka hivyo mtakaochukia huu Uzi na Mimi mwenyewe GENTAMYCINE mnivumilie tu japo najua hapa nawasaidia kuliko mnavyofikiri.
 
Poti mgonjwa yuko hoi , sasa hivi hata uji ameukaa sembuse hizo milioni na magari.

Sisi tunaotumia jicho la tatu malaika mtoa roho kamsimamia mgonjwa.

Wanahangaika tu na mavitu yao haponi.
 
Bro mechi ya kwanza kina chama walipokea chao mapema toka dar kama magoli unafahamiana nae mtafute akujuze kidogo.

Jinsi kina chama wawa walivopokea chao kupitia kwa mawakala wao mzee.
 
Am a zetu ama za0

FB_IMG_16214232566631652.jpg
 
Alichofanya Mo ni sahihi tu. Kwenye timu kila mtu atimize majukumu yake.

Makocha wafundishe mbinu ya uchezaji uwanjani, Wachezaji watimize majukumu yao, Mashabiki tushangilie ili kuongeza hamasa, Viongozi walipe maslahi na motisha kama Mo alivyofanya.

Wala Sijaona tatizo, sio jukumu la Mo kufanya mambo ya kiufundi ya uwanjani.
 
Back
Top Bottom