Kama hili ni kweli na siyo Uzushi tu nitaanza kumdharau Mo Dewji na Watendaji wake wa Simba SC wanaomzunguka

Unaambiwa hiyo njemba ndio WINGA yao, inakimbia KISINDA akasome, alikuwa majeruhi.View attachment 1791217
Kwahiyo unaogopa miili ya watu, dooh hii ni ligi ya mabingwa mkuu huku hakuna watoto wakuonea hovyo we Kama unaogopa basi huku si sehemu sahihi kwako waacheni Azam, biashara na Namungo nyie bakini hapa hapa mpambane na Gwambina.
 
Sasa mo awafundishe kucheza mipira ya juu, awafundishe mabeki wasifanye makosa? Ndio kazi ya Mo?

Mtazamo wangu Mo kutoa motisha yupo sahihi, hayo mengine na majukumu ya kocha.
Ni nani aliyowaambia kuwa Kiufundi (hasa katika Mpira) Timu yako ikiwa imefungwa katika ' Margin ' kubwa ili nayo Kulipiza Kisasi (Kupundua Meza) Wachezaji wanatakiwa waahidiwe Magari ya Kifahari na kila Goli watakalofunga litanunuliwa kwa Tsh 260 Milioni?

Hizi Ahadi ndizo zitafanya Mabeki wa pembeni akina Kapombe na Hussein wasiwe wanakatika hovyo Uwanjani?

Hizi Ahadi ndizo zitafanya Beki za Kati zilizochoka na hazina Kasi Wawa na Onyango safari hii zichangamke na ziwe zinacheza vyema aerial balls ambazo ndilo limekuwa tatizo kubwa la Mabeki wa Simba SC?

Yaani tunaacha kwa muda huu mfupi uliobaki Kutafuta Psychists wakae na Wachezaji wetu Waandamizi ambao wameshaathirika Kisaikolojia baada ya Kufungwa Kiufundi na Kiuwezo na Kaizer Chiefs FC tunakimbilia kutoa Ahadi hizi Kuu Kuu?

Leo Wanasimba tumesahau Dhambi kama hii ilivyotugharimu mwaka 1993 ( kama sijakosea ) ambapo aliyekuwa Mfadhili Mkuu enzi hizo Azim Dewji ( Mpwa kwa Mwekezaji Mo Dewji ) alipotoa Ahadi za Gari za KIA ambazo ziliharibu kabisa Saikolojia ya Wachezaji wa Simba SC kuelekea Fainali ile ya CAF dhidi ya Stella Abidjan FC?

Kuna Mambo ya Kipumbavu yanafanyika katika Soka la Tanzania na Vilabu vyake halafu tusiopendezwa nayo ( akina GENTAMYCINE ) tukikosoa tunaishia Kutukanwa, Kuchukiwa na kuambiwa kuwa ni Mashabiki wa Yanga SC au tuna Chuki na Simba SC na hasa hasa Mwekezaji wake Mohammed ' Mo ' Dewji.

Wakati hivi sasa Klabu ya Kaizer Chiefs wakijiandaa Kusafiri kuja Dar es Salaam wapo Darasani wakisoma Mbinu nyingi zaidi za Kiufundi za Kuikabili na Kuifunga Simba SC Wenyewe Simba SC sasa wanaomba Uwanja wa Mkapa ili Waroge, wafanye Umafia wa 4-4-2 Vyumbani na kutoa Ahadi za Magari ya Harrier na Shilingi Milioni 260 kwa kila Goli (Bao) litakalofungwa.

Mpaka hivi sasa sitaki Kuamini kuwa haya niliyoyasikia ni ya kweli kutokana na ninavyomjua Mwekezaji Mo Dewji na Mtendaji Mkuu Barbara, Mwenyekiti Mangungu na Mshauri Mkuu wa Mwekezaji na Ufundi wa Simba SC (Poti wangu kabisa kutoka Kwetu Mkoani Mara ) Crescentius Magori ila kama ni kweli basi kuanzia sasa nitaanza Kuwadharau wote hawa na watanisamehe kwa hilo ( hili )

Tukishinda Mechi ya marudiano nitafurahi ila tukitolewa (iwe kwa Kuwafunga Goli chache au hata kwa Kufungwa nao tena) GENTAMYCINE nitashukuru zaidi ili tumalizie Viporo vyetu vya VPL na Mechi zilizobaki na za ASFC ili tuchukue Ubingwa kote kote ili sasa Mwekezaji Mo Dewji ajipange zaidi katika Kusajili Wachezaji imara na mahiri wa Kimataifa ambao hawaifikisha tu Simba SC Robo Fainali bali hivi sasa watatufikisha hadi Fainali na Simba SC kuwa Bingwa kabisa.

Dawa Chungu ndiyo nzuri na huponya zaidi na kwa haraka hivyo mtakaochukia huu Uzi na Mimi mwenyewe GENTAMYCINE mnivumilie tu japo najua hapa nawasaidia kuliko mnavyofikiri.
 
Acha wachezaji wafaidike kwa hizo motisha ww ungekuwa mchezaji usinge lialia hapa goal moja mil 200 mpra wa bongo kuwa tajir inahitaji utoboe lkn offers km hizo zikija ni nzur kwa wachezaji wetu wa kibongo
 
Foolish.
 
Tutaziweka humu humu.

Hivyo na wewe kuna kitu kinakwambia bao tano zipo. 😂😂😂
Ngoja tuone ila msije kukimbia tu humu.

Ushindi upo tena mnono kabisa wale walituotea tu kule hawana lolote.
Tulimpiga vita 4 na platinum kapigwa 4 utopolo kapigwa 4 hapa hapa basi hata na hao Kaiza sijui Kaze watakufa tu hao
🤣
 
Bro mechi ya kwanza kina chama walipokea chao mapema toka dar kama magoli unafahamiana nae mtafute akujuze kidogo.

Jinsi kina chama wawa walivopokea chao kupitia kwa mawakala wao mzee.
Acha uwongo mlizidiwa mbinu tu
 
Mo mwenyew anajua hilo haliwezekan na sisi kama watani wenu tumejipanga vilivyo Kuhakikisha tunavya tua kila aina ya mtego mtakao tega
 
Ngoja tuone ila msije kukimbia tu humu.

Ushindi upo tena mnono kabisa wale walituotea tu kule hawana lolote.
Tulimpiga vita 4 na platinum kapigwa 4 utopolo kapigwa 4 hapa hapa basi hata na hao Kaiza sijui Kaze watakufa tu hao
🤣
Unasahau kabisa kama huyu inatakiwa umfunge tano. 😂😂😂

Tofautisha Nne na tano pia yakupasa ujue hizo goli nne mlizofunga zilitimia nne kama nne ndani ya dkk ngapi hapo ndo utajua goli tano sio mchezo.

Msije bakia tu kusema zingeongezwa dkk kadhaa basi Kaizer Chiefs angekufa 5. 😅😅
 
Wewe utakuwa una matatizo kwenye medula,muda wote ni matusi tu,huna uwezo wa kujenga hoja,unaanzisha nyuzi zako za kishabiki,watu wakichangia unawatukana!!!anzisha nyuzi uko nyumbani kwako,uchangie wewe na mke wako tu,sijui wewe ni mtu wa aina gani?!!!
 
Mudi ana shida ameshaekewa kwamba hawawezi kushinda ndiyo maana ametoa ahadi tunajua kabisa uwezo wa Mudi ni bodaboda.
Haya mengine ni kufurahisha baraza
 
Unasahau kabisa kama huyu inatakiwa umfunge tano. 😂😂😂

Tofautisha Nne na tano pia yakupasa ujue hizo goli nne mlizofunga zilitimia nne kama nne ndani ya dkk ngapi hapo ndo utajua goli tano sio mchezo.

Msije bakia tu kusema zingeongezwa dkk kadhaa basi Kaizer Chiefs angekufa 5. 😅😅
Sijasahau wala ila cha muhimu kusawazisha kwanza agg 4-4 then ndo tunatafuta ushindi sasa!

Kufunga goli tano unaweza funga hata ndani ya dk 45 tu hilo linawezekana kwenye mpira. Usijisahaurishe hata wewe tulikufunga 5-0 ndani ya dk 90 🤣.

Kuna watu wanapigwa hadi 8 we unaongea tano tu!!
Nyie nunueni tu hizo jezi za hao sijui Kaiza Chifu mtazivua tu pale kwa mkapa mwisho wa lami Lupaso.🤣🤣
 
Ndio nikauliza uwezo wa kufunga hizo nne kwa muda mfupi munao mana hizo game ulizosema
karibia zote hadi dakika ya 70 au 80 una bao mbili. 🤣🤣🤣

Mie yangu ninayo tayari hapa nasubiria kwenda Airport tu. 😉

Cc. Troisième Ceil
 
Uwezo tunao tena mkubwa we tulia uone pira biryani na mabao ya kutosha tu.

Kamati ya mapokezi wanafiki wa nchi 🤣🤣 ndio kazi yenu hiyo tunajua ila safari hii mtaumbuka sana.
 
Mama ni saa tisa wameumia hawajazoe jua

FB_IMG_16215254435690390.jpg
 
Wewe utakuwa una matatizo kwenye medula,muda wote ni matusi tu,huna uwezo wa kujenga hoja,unaanzisha nyuzi zako za kishabiki,watu wakichangia unawatukana!!!anzisha nyuzi uko nyumbani kwako,uchangie wewe na mke wako tu,sijui wewe ni mtu wa aina gani?!!!
Nilipoanzisha huu Uzi nilikuita You Nut?
 
Dah! Umenikumbusha 1993! Damian Kimti! Kila akitupia cross jamaa wanajikosesha magoli! Anawauliza "nyi wa.se.nge hamtakia KIA?" Kumbe watu washaahidiwa hivyo hakuna kufunga!
 
Back
Top Bottom