Kama hili litakuwa ni la kweli basi sasa naanza Kuamini kuwa Roho Mkatatifu ameshakita Kambi ndani ya TBC

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,402
2,000
Labda kama hali ni tete na sasa wanataka kupate fedha kupitia vipindi vya aina hiyo.

Ulilosema nakubaliana nalo kwa 85% Ndugu kwani inavyoonyesha hilo Tangazo la DG Rioba limekaa Kipesa zaidi na siyo Kisiasa kama tuwazavyo.
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
7,777
2,000
Ukitaka kuamini kuwa TBC ni wakweli ama waongo, CHADEMA ama ACT - Wazalendo waombe airtime ya kurusha LIVE matangazo yao ya uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Rais...

Mtakoma na kujuta kwanini mmewalipa fedha zenu maana watawarushia matangazo yenu vibaya kwa kukata kata kwa kisingizio cha "hitilafu za kiufundi"....

Kinachopaswa kufanyika ni vyombo vyote vya habari kuwa huru na kila anayehitaji huduma ya chombo chochote, aipate bila taabu. Hatuhitaji " censorship" ya taarifa ama habari....

Tunahitaji "HARD NEWS" kama zilivyo na zisizochujwa siyo "SOFT NEWS" zilizochujwa ku - suit interest za kikundi fulani cha watu....
 

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,497
2,000
Mimi nimeacha kutazama kabisa TV station za nyumbani mana hawana kingine cha kujadili zaidi ya Praise mimi natambua mchango mzuri wa JPM katika Taifa hili ila kwa huu uoga wa Media kwa kweli hata sihangaiki tena na local media ivi ku broadcast habari za Vyama vingine ni dhambi? ITV nao wako humo humo nao very unprofessional
Kuna mambo mengi ya ovyo yanaendelea na mimi naamini hayana baraka za mkuu wa nchi basi tu ni UOGA
 

Tate Mkuu

JF-Expert Member
Jan 24, 2019
10,054
2,000
Shirika lenyewe tu linatambulika kama TBCCM! Halafu litapata wapi sifa ya kurusha matangazo bila ya ubaguzi wa kisiasa na kiitikadi? Watangazaji wake wote ni Ccm na wamekaa standby kusubiria uteuzi wa Ukuu wa Wilaya na U DED kutoka kwa Mwenyekiti wa chama!

TBC ilijitahidi kuwa neutral enzi zile Mkurugenzi Mtendaji akiwa ni muasisi wake Mh.Tido Mhando. Baada ya kusababisha mvurugano kwa ccm kwenye ule uchaguzi mkuu wa 2010, tunakumbuka kilichoikuta TBC na huyo Tido mwenyewe miezi michache baadaye.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,686
2,000
Mkurugenzi Mtendaji wa TBC Dkt. Ayoub Rioba amesema chombo hicho cha habari hakibagui chama chochote cha siasa katika kurusha matangazo.

Dkt. Rioba amesema kuwa chombo hicho cha umma hakibagui chama bali wanatimiza wajibu wa kuwahabarisha wananchi kama inavyopaswa na sio kukaa kwenye mrengo mmoja wa chama kimoja.

Dkt.Rioba pia amesema baadhi ya vyama vilifikia hatua kukataa kushiriki kwenye vipindi endapo wanaalikwa ndani ya chombo hicho cha umma.

Aidha, amesema ikitokea vyama vya siasa vinaenda kuomba muda wa kipindi au matangazo chombo hicho cha umma kinatoa fursa na nafasi kwa vyama vyote nchini na anavikaribisha vyama vyote kwenye chombo hicho cha umma hususani kuelekea kipindi hiki cha uchaguzi Mkuu bila ubaguzi wowote.

Habari Star TV Tanzania

Kuna Mtu Mmoja aliwahi Kuniambia Mzukulu kuwa kuna tofauti kubwa sana kati ya Kuongea na Kutenda au Uhalisia na Ukweli wa Jambo husika.

Nimeangalia hicho kipindi leo asubuhi akiwa kwenye mjadala ndani ya Star TV. Nilichogundua kitendo cha viongozi au watumishi wa taasisi za umma wakiwa na tabia za kuhojiwa hadharani, zinaweza kuwafanya waone aibu kwa kiwango fulani kwenye nyendo zao, na wanaweza kubadilika kama itawezekana. Alijaribu kuzunguka zunguka japo alirusha utetezi wa hapa na pale, lakini wangalau ameonyesha kuwa kwamba anajua chombo chake kina tuhuma za kutokuwa fair. Nashukuru Paskali Mayalla alimbana vyema kwenye hili.
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,686
2,000
Shirika lenyewe tu linatambulika kama TBCCM! Halafu litapata wapi sifa ya kurusha matangazo bila ya ubaguzi wa kisiasa na kiitikadi? Watangazaji wake wote ni Ccm na wamekaa standby kusubiria uteuzi wa Ukuu wa Wilaya na U DED kitoka kwa Mwenyekiti wa chama!

TBC ilijitahidi kuwa neutral enzi zile Mkurugenzi Mtendaji akiwa ni muasisi wake Mh.Tido Mhando. Baada kusababisha mvurugano kwenye ule uchaguzi mkuu wa 2010, tunakumbuka kilichoikuta TBC na huyo Tido mwenyewe miezi michache baadaye.

Ngoja tumpe benefit of doubt, nimemuoana leo akiwa Star TV kwenye kipindi cha jicho letu ndani ya habari akiwa kwenye mjadala na nguli Dotto Bulendu. Natagemea nione mabadiliko kuanzia sasa kama ni kweli alichokisema.
 

Nanye Go

JF-Expert Member
Oct 29, 2018
7,732
2,000
kusema tu kwamba vyama vyote vinakaribishwa inaonyesha kwamba anatambua HAVIKARIBISHWI.

Ukimsikia Sheikh anatangaza kwamba msikiti wetu haubagui madhehebu mengine, inamaanisha hajawahi kuaona watu wa hayo madhehebu mengine msikitini kwake.

Hii ni kujidanganya na kujifurahisha anafanya, ila ukweli anaufahamu.
 

ostrichegg

JF-Expert Member
Jun 30, 2013
11,562
2,000
Hawezi kutumbuliwa kwa kusema alichosema. Asingeweza kusema kuwa wao kama combo cha umma wanapendelea Chama au mtu. Kusema alichosema ni ushahidi kuwa anajua taasisi anayoiongoza inatazamwa visivyo katika sehemu ya jamii. Vitendo vyake ndio vitathibitisha kama hawamtendei haki au la, sio maneno yake. Na anajua hilo. Na viongozi wake wanajua hilo.

Amanda...
Ngawethu
 

Mzukulu

JF-Expert Member
Feb 14, 2020
1,402
2,000
Ngoja tumpe benefit of doubt, nimemuoana leo akiwa Star TV kwenye kipindi cha jicho letu ndani ya habari akiwa kwenye mjadala na nguli Dotto Bulendu. Natagemea nione mabadiliko kuanzia sasa kama ni kweli alichokisema.

Na Wewe unamwamini kabisa tena 100% huyo DG wa TBC juu ya alichokisema Ndugu? Yaani TBC waturushie Maudhui ya Madongo ya Wapinzani?
 

Tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
43,686
2,000
Na Wewe unamwamini kabisa tena 100% huyo DG wa TBC juu ya alichokisema Ndugu? Yaani TBC waturushie Maudhui ya Madongo ya Wapinzani?

Ndio maana nimesema tumpe muda ili athibitishe.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom