Kama hili lilishindikana, la Kibanda halitafanikiwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hili lilishindikana, la Kibanda halitafanikiwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dr.Godbless, Mar 17, 2013.

 1. Dr.Godbless

  Dr.Godbless JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2013
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 800
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 180
  Historia inatukumbusha kuwa Mnamo mwaka 2008, Chadema ilikumbwa na mgogoro baina ya viongozi wake wa juu katika suala la Mgawanyo wa rasilimali za chama. Tofauti hizo zilipanuka zaidi baada ya Mhe. Chacha Wangwe kutumia vyombo vya habari kutoa maoni yake juu ya kile ambacho alikiamini kuwa ni sahihi.

  Ni katika hali hiyo ya malumbano basi Mhe. Chacha Zakayo Wangwe alifariki katika mazingira ya kutia shaka. Kwa kiasi kikubwa Kifo hicho kilitumika kama mtaji wa kisiasa na CCM. Propaganda hiyo ilidumu mpaka katika Uchaguzi mdogo wa Ubunge ambapo Chadema ilitwaa tena kiti hicho. Wananchi wa Tarime waliujua ukweli wakachagua kweli.

  Soma propaganda

  Chanzo: Blogu ya Tarishi Hauwawi

  August,15 2008.

  Mbowe afanyia sherehe Kifo cha Chacha Wangwe

  MWENYEKITI wa CHADEMA, Bw. Freeman Mbowe, anadaiwa kufanya hafla kubwa Afrika Kusini saa chache baada ya kupata taarifa za kifo cha Makamu wake, marehemu Chacha Wangwe.Habari zilizopatikana kutoka hoteli ya Garden Court jijini Johanesburg ilikoifanyika hafla hiyo Julai 29 mwaka huu, zilisema baada ya Mwenyekiti Mbowe kupokea taarifa za msiba, alifanya hafla ya kuwaaga wajumbe aliokuwa nao huko ili arejee nchini kwa mazishi.

  "Kwanza taarifa ilipopatikana, hakututangazia mpaka tulipopata kutoka kwa vyanzo vyetu vingine ndipo tukathibitisha naye…akatuandalia hafla jioni ya siku hiyo," kilidai chanzo cha habari hii.

  Kilidai kuwa kilishangaa kuona katika mazingira yale ya majonzi, kuandaliwa hafla kubwa namna ile.

  "Tulishangaa na kumuuliza kwa nini hafla ile, akatujibu kuwa alikuwa akituaga, kwani anarudi nchini kushiriki mazishi ya marehemu Wangwe," kiliongeza chanzo hicho.

  Kilidai kuwa hata wajumbe wa vyama vya siasa waliokuwa nchini humo kuhudhuria semina ya vyama vyenye wabunge Afrika, walipotaka kumchangia rambirambi, hakutaka kuipokea na badala yake kuwaambia kila mmoja ataje kiwango naye atawalipia.

  "Tulitaka kumchangia fedha za rambirambi mwenzetu huyo, lakini hakuonesha nia ya kuzipokea na badala yake akatuambia kila mmoja ataje kiwango chake naye akifika Tanzania ataziwasilisha msibani," kilidai chanzo hicho.

  Wajumbe tisa kutoka Tanzania walikuwa wakiongozwa na Bw. Mbowe katika semina hiyo ya siku nne ya kujifunza jinsi Tume Huru ya Uchaguzi inavyofanya kazi nchini Afrika Kusini.

  Chanzo hicho cha habari kilisema semina hiyo ilikuwa ni kwa ajili ya makatibu na naibu makatibu wa vyama vya siasa nchini, lakini walishangaa kumwona Mwenyekiti wa CHADEMA naye akishiriki.

  "Yawezekana alialikwa, lakini mbona wenyeviti wenzake hawakualikwa, tulijiuliza sana lakini tukaacha mambo yaendelee hivyo hivyo," kilidai chanzo hicho.

  Pia wanasiasa hao walikutana na viongozi wa chama tawala cha Afrika Kusini cha African National Congress (ANC).

  Wajumbe waliohudhuria semina hiyo ni wawili kutoka CHADEMA, wawili CCM, mmoja mmoja CUF, TLP, Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Tume ya Haki za Binadamu na Mkurugenzi wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD).

  Bw. Mbowe alipoulizwa kuhusiana na madai ya kuwaandalia tafrija baadhi ya watu aliokuwa akihudhuria nao mkutano huo, kabla ya kurejea Dar es Salaam kuhudhuria msiba wa marehemu Wangwe, alijibu:

  "Hao waliokuambia ni akina nani! Waambie wakuthibitishie maana siwezi kuingia kwenye malumbano ya mambo ambayo hayakuwapo."

  Alipoulizwa ilikuwaje akahudhuria mkutano huo wakati ulikuwa ni kwa ajili ya makatibu wakuu na manaibu wao kutoka vyama vyenye wabunge, Bw. Mbowe alisema alipewa mwaliko wa kuhudhuria mkutano huo.

  "Mimi nilialikwa na watu TCD kuhudhuria mkutano huo," alisisitiza Bw. Mbowe alipozungumza na gazeti hili kwa njia ya simu.

  Akizungumzia madai kuwa alikataa michango waliyotaka kutoa baadhi ya washiriki aliokuwa nao kwa ajili ya rambirambi na badala yake kudaiwa kuwataka watoe ahadi zao na akifika Dar es Salaam atawatolea, Bw. Mbowe alijibu:

  "Wewe zungumza na vyanzo vyako hivyo vikuthibitishie kama hayo yalitokea."

  Kwa sasa propaganda hii imejirudia tena katika staili mpya ya kufake video clip na kumezesha watu maneno ili kuhalalisha propaganda hizo.
   
 2. MALUNGU

  MALUNGU JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2013
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 250
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Maccm katika propaganda zao za kusuka mipango ya kihalifu na kusingizia wengine ndo mtindo wao wa siku nyingi sana tangu mfumo wa vyama vingi uanze hapa nchini. Tushukuru mungu yupo upande wa wengi, hili nalo ninapita na kutuongezea umaarufu kwa watanzania. Wanapaswa watekeleze ahadi walizozitoa tangu 2005 na hizi za 2010 hapo ndo wananchi watawaelewa.
   
 3. Dr.Godbless

  Dr.Godbless JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2013
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 800
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 180
  Upo sahihi kabisa, Kwa hali ilipofikia CCM wana uhakika kuwa hawawezi kushinda uchaguzi 2015 ndhidi ya chadema. Ukiachilia nguvu ya chadema CCM bado ina changamoto nyingi sana ambazo haziwezi tena kupatiwa ufumbuzi, Mfano Kuna suala la kukithiri kwa umasikini kwa Watanzania wengi, Mgogoro wa kirasilimali kati ya raia na Serikali ya CCM, Uwezo finyu wa utekelezaji wa ahadi kwa Wananchi, Makundi ndani ya chama ambayo ni vigumu kukutanishwa na kuungana, Kukosa mgombea wa Uraisi ambaye atakuwa na mvuto kwa Watanzania. Hivyo kilichobaki ni kudhoofisha ama kuua upinzani ili kisiwe na mshindani wa kweli. Propaganda ya Udini imeonekana kudhoofisha Taifa kuliko chadema, Ukabila umeonekana kukosa mashiko, Mauaji ndio umekuwa mtaji zaidi. Ni propaganda hii ya mauaji hutumiwa zaidi kama silaha ya mwisho. Mfano ni kama CUF walipozushiwa tuhuma za kuingiza makontena ya majambia na mapanga siku moja kabla ya zoezi la kupiga kura.
   
 4. M

  MASIKITIKO JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2013
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 853
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  Kizuri chajiuza,hakiitaji video clip fake
   
 5. Rweye

  Rweye JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2013
  Joined: Mar 16, 2011
  Messages: 15,466
  Likes Received: 3,360
  Trophy Points: 280
  nashindwa kuelewa kama ilani ya CCM 2010 kwa wananchi ilikuwa na kuuwa raia wake make naona ndo mpango mkakati sasa.
   
 6. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2013
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Propaganda huwa haishindwi,ïla inaposhindwa inambna aliyeitumia ni mpumbavu
   
 7. b

  blueray JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2013
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Mkuu uko sahihi kabisa, hii propaganda kwa magamba is the last though but one. Hii inaonyesha dhahiri kwamba CCM imekwisha shindwa.
  Inavyoelekea watu waliotengeneza hii movie ya Lwakatare wametumia akili sana lakini hawakuwa makini.
  Kwa hii tuhuma Chadema imekwishashinda hata kabla ya kwenda mahakamani kwa sababu inaonekana dhahiri hiyo video ni feki au imeigizwa
   
 8. M

  Mr.Busta JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2013
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 672
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Propaganda huwa haishindwi,ïla inaposhindwa inambna aliyeitumia ni mpumbavu
   
 9. Bei Mbaya

  Bei Mbaya JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2013
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,265
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Wakati Denis Malya walimhusisha na Mbowe kwa kuwa kabila moja

  Ludovick Rwehumbiza vivyo hivyo kwa Lwakatare

  wote wawili wanajihusisha na I.T

  wote ni watu wasiokuwa na shughuli maalum lakini haya ya hadharani sasa ndiyo shughuli yao
   
Loading...