Kama hiki kinachozungumzwa chini chini juu ya CHADEMA ni kweli, basi tuendako wenye sifa walizonazo vibaka watagombea Uenyekiti

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,865
Inasemekana (japo bado naendelea kulithibitisha hili) kwamba mmoja wa viongozi ‘waandamizi‘ kabisa ndani ya CHADEMA alisikika akimwambia mtu kuwa ili uwe Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA na uaminike basi ni lazima uwe angalau katika maisha yako ya ‘kutukuka‘ kabisa ndani ya CHADEMA uwe umekumbana na yafuatayo ambayo kwa bahati mbaya Mzee Sumaye hakuwa nayo ndiyo maana yakamshinda na kuachana na siasa.

Uwe:

- Umewahi kuhojiwa kunakopitiliza na Polisi (Mandata)

- Uwe na kesi nyingi Mahakamani na angalau uwe na ufahamu wa Mahakama ya Kisutu ilivyo

- Uwe umewahi kulala sana polisi au gerezani na hata ukiwa uraiani basi uonekane unatamani kufungwa

Kazi kweli kweli hakyanani!
 
Zamani kidoho ilikua da mange kasema , sasa ni kigogo kasema. Hii nchi vijana hawana akili kabisa, hawawazi, hawafikirii, akili zao wameziweka kwa watu wafikirie kwa niaba yao.

Ndio maana ccm inaendelea kuongoza hata baada ya miaka 50 ya uhuru na bado umasikin ujinga na maradhi yametamalaki.
 
Inasemekana (japo bado naendelea kulithibitisha hili) kwamba mmoja wa viongozi ‘waandamizi‘ kabisa ndani ya CHADEMA alisikika akimwambia mtu kuwa ili uwe Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA na uaminike basi ni lazima uwe angalau katika maisha yako ya ‘kutukuka‘ kabisa ndani ya CHADEMA uwe umekumbana na yafuatayo ambayo kwa bahati mbaya Mzee Sumaye hakuwa nayo ndiyo maana yakamshinda na kuachana na siasa.

Uwe:

- Umewahi kuhojiwa kunakopitiliza na Polisi (Mandata)

- Uwe na kesi nyingi Mahakamani na angalau uwe na ufahamu wa Mahakama ya Kisutu ilivyo

- Uwe umewahi kulala sana polisi au gerezani na hata ukiwa uraiani basi uonekane unatamani kufungwa

Kazi kweli kweli hakyanani!
Kumbe #Kigogo2014 kwako ni kiongozi mwandamizi wa Chadema.

IMG_20191206_073526.jpg
 
Kwani ilikuwa lazima Sumaye awe mwenyekiti? Watu wanajadili utadhani ni lazima agombee. Hivi ingekuwa wewe ni kiongozi katika hili wimbi la hama hama, ungeweza kuruhusu yeyote awe kiongozi hasa kama ana vinasaba na ccm? Mwenyewe kalalamika kunyanganywa mashamba na kuchukiwa na familia, je ukimpa uongozi akazidiwa na nguvu ya familia isiyotaka kaskash za kuwa mpinzani na kunyang'anywa Mali zaidi na huku tayari ameshakuwa mwenyekiti wa Taifa, kama una akili timamu, huioni hatari itakayoikabili Chadema?

Ukitaka kujua ninachokisema kinafanyaje kazi, subiri kura za maoni 2020 kwa wagombea wa ccm uone kama walioubga juhudi watapita hata mmoja tofauti na wale raisi atajaowakingia kifua baada ya kubwagwa vibaya kwenye kura za maoni.

Mark my words, hivyo ndivyo ilivyo na itakavyokuwa.
 
Tumabisha kwa sababu tunapenda malumbano tuu.
Hivi kama chama viongozi wote wanabambikwa kesi kila siku, kila kukicha polisi, viongozi na wanachama wanashambuliwa wao au Mali zao na hayo ndio maisha ya wanachama.
Lakini wewe uje from nowhere na dhahma hizo wazipatazo wanachama huzijui zaidi ya kusoma kwenye magazeti halafu upewe nafasi ya juu kabisa? Shubamit, hakuna kitu kama hicho.
Nenda kwenye nchi mfano za kusini kizazi kile kilichopigania Uhuru kingalipo hakuna kupewa madaraka eti ulikuwa unaishi nje ya utaratibu wa harakati za Uhuru upewe nafasi ya juu. Ajabu nini kwa Chadema? Au jinsi presentation ya jambo hilo ndio haijakaa vizuri lakini MAANA halisi ndio hii.
 
Hata kwa Jamhuri ya Muungano Tanzania ni vivyo hivyo Huwezi kua rais kama huna hizi sifa
1. Mwanachama wa Ccm
2. Hujawahi kuwekwa ndani au magereza kwa kesi yoyote ya jinai hata ya kusingiziwa wala kupelekwa mahakaman
3 umewahi kushika nafasi kubwa kwenye serikali ( waziri kwenda juu)
Umeona jinsi vigezo vyao ambavyo sio rasmi vinavyokinzana na vigezo vya serikali visivyo rasmi pia
 
Chadema Demokrasia hawaiwezi kama ilivyowashinda Ccm ... Tanzania hatuna chama cha upinzani ni vikundi vya wahuni tu... kila mtu apambanie maslahi yake
 
CDM huwa wanafurahisha sana yaan KIGOGO2104 akiiponda serikali basi ni mwenzao leo akiwaponda wenyewe wanamjia juuuu
 
Back
Top Bottom