Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!. | Page 5 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Hii ni Kweli, Then, Serikali ya Magufuli ni Serikali Haramu. Hukumu ya Karma ii Juu Yake!.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 29, 2015.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,659
  Likes Received: 23,892
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,

  Kuna hii tuhuma iliyotolewa leo na Edward Lowassa.

  Kama tuhuma hii ni kweli, then serikali ya Magufuli ni serikali haramu na serikali iliyopatikana kwa njia za udhalimu kitu ambacho sio kizuri kwa mustakabali mwema wa taifa letu.

  Kwa mujibu wa katiba yetu, Tume ya Uchaguzi, ikiisha kumtangaza fulani ndie mshindi, kwa tangazo hilo ndio limehitimisha rasmi mchakato wote wa urais.

  Mgombea urais akiishatangazwa kuwa ni mshindi, regardless amepatikanaje, kihalali au kiharamu, by means of hooks or crooks, kwa bao la kisigino, faulo au bao la mkono, as long as yeye ndie ametangazwa mshindi, this is the end that justifies the means!, there is nothing more anyone can do, ukubali usikubali matokeo, uwe ulimchagua, au hukumchagua, umtambue, au usimtambue, its never gonna change a thing!, huyu sasa ndie rais wetu and this is a fact!.

  Kitu kizuri kuhusu haki, haki kamwe huwa haipotei, hata kama sio kwa dunia hii, bali kwa dunia ijayo, na ubaya siku zote huwa haulipi na malipo yote ni hapa hapa duniani, hata kama sio kwako, then kwa kizazi chako!.

  Then namshauri Edward Lowassa, kuwa umetimiza wajibu wako, kutaka kuwatumikia Watanzania!. Umefanya kazi yako, imekamilika!. Sasa nakuomba statement yako hii iwe ndio ya mwisho, usiendelee kulalamika popote, bali sasa nenda zako kajipumzikie kwa amani kwa kuchunga ng'ombe wako kama ulivyoahidi, tena usipeleke malalamiko yako mahali pengine popote zaidi ya kwa aliye JUU, hivyo haya meingine yote muachie Mungu!, YEYE ndiye atakulipia!. kuna mahakama ya haki kuliko mahakama zote za dunia hii, au za ulimwengu huu!, hii ni mahakama ya karma, ndio mahakama pekee ya haki bin haki!.

  Kwa wale wote waliomchagua Lowassa lakini haki zenu zikadhulumiwa, poleni sana!, Mungu atawalipia.

  Na wale wengine wote wanaoshangilia ushindi haramu, ushindi dhalimu, hawa wanashangilia ujinga!, hawa nao pia watakuwa na sehemu ya malipo yao kwenye karma.

  Na kama ni kweli Magufuli ameupata urais wa Tanzania kwa hila, na udhalimu, then tutashuhudia utawala wa mkono wa chuma, the reign of iron hand. Mtashuhudia udikiteta na udhalimu wa ajabu, kuna watu kwa sasa wanashangilia, lakini mwisho wa siku, watakuja kulia na kusaga meno!.

  Kama uchaguzi mkubwa hivi wa rais na wabunge kumeweza kufanyika hila, hii inamaanisha kule ambako wapinzani wameshinda ni maeneo ambako hila zimeshindikana, hivyo kwa uchaguzi wa 2020, wapinzani jiandaeni kuyarejesha majimbo karibu yote na nchi kurejea kwenye mfumo wa chama kimoja.

  Kipimo cha hili kitapimwa kwa chaguzi ndogo zozote zitakazotokea hapa katikati, kwanza upinzani hautaweza tena kushinda uchaguzi wowote, na kama kiti cha ubunge au udiwani kilichokuwa kinashikiliwa na upinzani kitakuwa wazi, uchaguzi wa marudio utakirudisha CCM kwa mbinu zile zile dhalimu by hooks and crooks!.

  Kwa hili hasiri ya Mungu itawaka juu ya Tanzania yetu, tutapata mabalaa na majanga ya ajabu kwa sababu ya hasira ya Mungu, na as taifa tutasuffer ba kuna watu wataangamia!.

  Ila pia, endapo tuhuma hizi ni za uongo, ni za kupika na ni uzushi, then John Pombe Magufuli, ndiye rais chaguo la Mungu kwa Tanzania aliyetangazwa mshindi siku yake ya kuzaliwa!, katika uchaguzi huru na wa haki, hivyo atasimama test in time, of which time will tell!.

  Tanzania itapata neema, mafanikio na maendeleo ya ajabu kwa sababu ya baraka za Mungu zitakuwa juu yake, nchi yetu inakwenda kageuka kuwa ni ile nchi ya ahadi ya maziwa na asali.


  Neno litasimama, mambo mengine yote yatapita, lakini neno litasimama!.

  Mungu ibariki Tanzania.

  Paskali

  Kwa rejea mambo ya karma, karibu mitaa hii
  "The Power of 'Karma'- Ndio Hukumu Pekee ya Haki Kamili
  "Bora Katiba", Tuikubali!, Tusiichukie CCM!, Kwa Sababu
  When Karma comes calling, she stings like a bitch
  Psychic Powers: Ni Nguvu za Kufanya Miujiza. Wengi wanaz
  "Will Powers!", "Faith Healing!"-Nguvu ya Miujiza Ya Uponyaji kwa
   
 2. G'taxi

  G'taxi JF-Expert Member

  #81
  Oct 30, 2015
  Joined: Sep 15, 2013
  Messages: 3,187
  Likes Received: 2,600
  Trophy Points: 280
  Unajua bwana watu tuliomba makanisani na misikitini,na tunaamini kiongozi yeyote anatoka kwa MUNGU na kwa makusudi mazima kwa watu wake.hvyo basi mimi binafsi naamini kua MAGUFULI ni chaguo la MUNGU na waliompigia kura hawajakosea,by the way ni watu tu kujaribu kupotezea lakini wanajua MAGUFULI ni mtu gani,tukiachana na madhaifu ya kibinadamu lakini ndo wazili pekee ambae tumekua tunaona hajawah kufeli ktk kazi,na huyu wa upande wa pili ndiye mtu ambae alihubiliwa na hawa hawa walokua wanamnadi kua alikua fisadi na hafai kua kiongozi,leo wamekuja nae kusema anatufaa sana,tunamheshimu sana huyo mzee lakini kuna mambo juu yake na walokua wakimnadi ambayo hayahitaji degree kupambanua mambo! MUNGU IBARIKI TANZANIA YANGU.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #82
  Oct 30, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,659
  Likes Received: 23,892
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mgeni wa Mungu, sisi Watanzania tuna tatizo kubwa sana la upungufu wa elimu ya uraia na elimu ya haki zetu za msingi!. Kwa mujibu wa katiba hii iliyopo, matokeo ya urais yakiishatangazwa na NEC, ndio the end of the world!. Hakuna mamlaka yoyote duniani au mbinguni inaweza kubadilisha kitu!, ndio maana nimemshauri Lowassa ajirudie zake tuu kijini kwake akajichungie ngombe wake kama alivyoahidi, there is nothing more one can do!.

  Pasco


   
 4. MSUMARI WA MOTO

  MSUMARI WA MOTO JF-Expert Member

  #83
  Oct 30, 2015
  Joined: Oct 25, 2015
  Messages: 461
  Likes Received: 127
  Trophy Points: 60
  Mungu ndiye mtetezi wetu!
   
 5. m

  mzalendo15 JF-Expert Member

  #84
  Oct 30, 2015
  Joined: Sep 16, 2015
  Messages: 1,367
  Likes Received: 1,004
  Trophy Points: 280
  ccm wameua muungano wenyewe hakuna muungano tenaaa!!!!
   
 6. YEHODAYA

  YEHODAYA JF-Expert Member

  #85
  Oct 30, 2015
  Joined: Aug 9, 2015
  Messages: 11,767
  Likes Received: 11,142
  Trophy Points: 280
  Nani unayemfungia na kumwombea huyo kwenye picha? Mzee wa michanganyo? Usipoteze muda kale ulale

  [​IMG]
   
 7. aretasludovick

  aretasludovick JF-Expert Member

  #86
  Oct 30, 2015
  Joined: Aug 8, 2015
  Messages: 3,027
  Likes Received: 1,942
  Trophy Points: 280
  Nimekosa kitufe cha like aisee
   
 8. Deeboyfrexh

  Deeboyfrexh JF-Expert Member

  #87
  Oct 30, 2015
  Joined: Apr 3, 2015
  Messages: 996
  Likes Received: 108
  Trophy Points: 160
  UKAWA,It my sorry to you muthafuckas...Blame game ain't workin' shitbirds!
   
 9. Mbaliche

  Mbaliche JF-Expert Member

  #88
  Oct 30, 2015
  Joined: Jul 6, 2011
  Messages: 291
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Itafahamika malipo hapahapa duniani!
   
 10. Mgeni wa Mungu

  Mgeni wa Mungu JF-Expert Member

  #89
  Oct 30, 2015
  Joined: Mar 5, 2015
  Messages: 1,239
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Sasa nikukumbushe kitendo alichokifanya huyu kiongozi cha kuiacha Ccm kwa Mara ya Kwanza katika historia ya siasa za Tanzania alikua ni yeye, je huoni pia kama kwa Mara ya kwanza tena akaweza pia kuyafanya hayo unayoyasema hayawezekani yena kubadilishwa? Kitendo kile kila mmoja kilimshangaza sana na mimi sikuwahi kuzitegemea siasa zetu kuwa zingelifikia kiwango kile.

  Ni kwambie tu kwa Mungu tunaona,na tutaona maajabu mengi sana ya kawaida na yasio ya kawaida.. Kwa kupitia jitihada zake yeye kama Mungu yuko nae anaweza akaleta mabadiliko makubwa na akaiandikia tena historia nyingine nchi hii.

  Mimi nionavo ni mapema sana kumwambia akachunge ngombe kwanza Tumuache atafakari cha kufanya na sisi tumejifunza mengi kupitia kwake na pengine tutazidi kujifunza kuliko tukimuacha akenda akafuga ngombe.

  Ahsante
   
 11. jd41

  jd41 JF-Expert Member

  #90
  Oct 30, 2015
  Joined: Aug 23, 2015
  Messages: 2,608
  Likes Received: 1,314
  Trophy Points: 280
  ni sheria ipi inayosema mgombea urais lazima ahutubie kwa masaa matatu?!
  mbona wote mnaoitetea ccm humu jf mna akili fupi sana?!
   
 12. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #91
  Oct 30, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,659
  Likes Received: 23,892
  Trophy Points: 280
  Mkuu KipimaPembe, kwanza asante kwa objectivity kwenye bandiko lako hili. Nimependa zaidi mstari huu,
  na hapa ndipo mahali pekee, kama kuna wizi ulifanyika, ndipo karma ita strike!.

  Naungana na wewe sio tuu kuwa Magufuli hakuhitaji kuiba kura kumshinda Lowassa, kwa sababu in reality Magufuli ni mzuri kushinda Lowassa na hili nililisema kabla hata Magufuli hajateuliwa na CCM, nilieleza humu kuna 'sababu fulani' lazima awe Magufuli, nilizieleza humu!
  [h=3]Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John [/h] ile day 1 tuu Magufuli amepitishwa pia nikatoa ushauri huu kwa Lowassa
  [h=3]Ushauri wa Bure Kwa Lowassa: Kwa Vile ni Magufuli, [/h]Hivyo hakuhitaji kuiba kura kushinda, ila ilifika mahali CCM wakatambua kuwa Lowassa ana mvuto wa ajabu wa kupendwa na watu [h=3]Hii 'Vox Populi' ni 'Vox Dei' Kuhusu 'Jiwe Walilolikataa Waashi .
  [/h]for a reason or no apparent reasons at all ila anapendwa na ana mvuto!, hivyo wangejiachia tuu kuiacha nature itoe ushindi, kulikuwa na hatari ya kushindwa na ndipo wakapanga mambo yao!. Haiwezekani kabisa, kama kila kituo kila mpiga kura alipiga kura tatu, haiwezekani jumla ya matokeo ya udiwani, ubunge na urais yatofautiane kwa sababu every vote was casted and caunted!. Jazia jazia kubwa imefanyika kwenye kura za ubunge na rais!. Kule wapinzani walikotangazwa washindi, ujue the gap was too wide to bridge!. Ila mimi jiliwashauri sana hawa jamaa zangu to ivest on numbers because numbers dont lie!.
  [h=3]Kuelekea 2015: CHADEMA, Don't Miss the Target,
  [/h]they missed the target!.

  Pasco


   
 13. K

  KipimaPembe JF-Expert Member

  #92
  Oct 30, 2015
  Joined: Aug 5, 2007
  Messages: 1,284
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Pasco,
  Does it mean kwamba kila jimbo CCM waliiba? Kila kata CCM waliiba? zile ambazo hawakuiba basi upinzani ulishinda? I doubt kama wengi tunaoleta hayo madai ya wizi tulikuwa na contact zozote on the ground.

  Nina ndugu yangu aligombea udiwani kupitia Chadema alishindwa na anakiri alishindwa kihalali! Lazima tujue kuwa huku kupendwa kwa Edo hakukuwa perfect jamani. Tuwe wakweli. Kama kupendwa kama kampeni yake mlivyokuwa mnamchora ni kweli alikuwa anapendwa; lakini kwamba alikuwa anapendwa perfectly na kila mtu?? That's delussional!
   
 14. Mkaruka

  Mkaruka JF-Expert Member

  #93
  Oct 30, 2015
  Joined: Feb 5, 2013
  Messages: 9,551
  Likes Received: 6,372
  Trophy Points: 280
  Uko sawa kabisa na "AKIKAIDI"......Halafu hawa kina Mbowe akili ndogo sana yaani wanaleta vijana wa IT kutoka sijui Korea halafu wanaona kama watafanikiwa lengo lao kabisaa.Tanzania siyo Somalia
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #94
  Oct 30, 2015
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,659
  Likes Received: 23,892
  Trophy Points: 280
  Mkuu The Boss, you have the powers, usijiogope bali jitumie!. Hili la majina nawaachia watu wa numerology, tena sio majina tuu hara vibrations za rhymes, John Pombe, Joseph Magufuli yenye herufi zinazojirudia mara mbili mbili, angalia jina hili John Pombe, Joseph Magufuli, lina herufi hizi JJ, EE, HH, MM, PP, OO na UU na jina la Samia Suluhu Hassan lenye SSSS, AAAA, UUU, sio bure!.

  Hata ile kushinda tuu siku yake ya kuzaliwa it is not nothing!, kwenye mambo haya hakuna coincidence, kila jambo ni pre meditated move!, hivyo hawakuhitaji kabisa kuiba kura!.

  Pasco

   
 16. f

  fesi Senior Member

  #95
  Oct 30, 2015
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 125
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndugu inaonekana hujui maana ya democrasia. Km unadhani mawazo yako ni bora kuliko ya watanzania walio baki basi una tatizo.
  Waache na wengine watumie uhuru wao km EL alivyotumia Uhuru wake kuja CDM kutuchafulia chaka chetu
   
 17. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #96
  Oct 30, 2015
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,956
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Ndio maana ombi la Lowassa kwa tume siku zote limekuwa kuhesabu kura kwa kutumia karatasi za kura zilizosainiwa na mawakala vituoni. Kura zilizotangazwa na NEC zimetoka kwa vijana wa CCM pale Kempinski hotel na hazifanani na kura halisi.
   
 18. a

  analaizi JF-Expert Member

  #97
  Oct 30, 2015
  Joined: Mar 8, 2014
  Messages: 1,351
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Watanzania tumeikataa UKAWA KUANZIA madiwani,wabunge na Rais.pia tumefahamu wazi wazi kwamba UKAWA ilikuwa na mamluki KUTOKA nje kuwasaidia kampeni..kwa hali UKAWA isahau kuongoza tz
   
 19. MVUMBUZI

  MVUMBUZI JF-Expert Member

  #98
  Oct 30, 2015
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 5,021
  Likes Received: 699
  Trophy Points: 280

  That was planned not Coincidence. Kama ni chaguo la Mungu its a matter of time kama Mungu atasimamia utawala wake tutajua. Sitaki kuzungumzia habari za Mfalme Belshaza lakini naziona dalili kuwa Magufuli is destined to be Belshaza of our time.
   
 20. G'taxi

  G'taxi JF-Expert Member

  #99
  Oct 30, 2015
  Joined: Sep 15, 2013
  Messages: 3,187
  Likes Received: 2,600
  Trophy Points: 280
  Unaweza kutoa uthibitisho hadharani?
   
 21. a

  analaizi JF-Expert Member

  #100
  Oct 30, 2015
  Joined: Mar 8, 2014
  Messages: 1,351
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Nahisi wale mamluki walishauri hivi@
  1) kamata vyombo habari na NGOs mapema
  2)ponda media na NGOs zisizokukubali
  3)waahidi wenye changamoto kila kitu duniani-bodaboda, mama ntilie
  3)usijibu hoja nzito.jidai unaonewa
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...