Kama hii ni kweli, kocha wa Yanga Nasreddine Nabi anajichimbia kaburi

nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,430
5,769
Kama ni kweli basi Mwarabu wa watu anajichimbia kaburi historia ya kocha klabu zetu haswa yanga kuja na wachezaji wa nchini mwake siyo nzuri, kwanza wakiwa chini ya kiwango atalazimisha kuwapanga.

Wenzao watawachukia. Wachezaji hao wataanza kulalamikia viwanja vibovu hapo itabidi wapangwe viwanja visvyozidi hata vi nne vyenye quality

Mwisho wa siku kocha atafukuzwa watabaki kama yatima nao itabidi waondoke au kuvunjiwa mkataba kwa gharama kubwa. NARUDIA TENA KAMA NI KWELI BASI HUU NDIYO MWANZO WA MWISHO WA MWARABU PALE YANGA

========

KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi imeelezwa kuwa anahitaji kumleta mchezaji ndani ya Yanga ambaye atatoka nchini Tunisia.

Hiyo yote katika kuhakikisha kikosi chao kinaimarika katika kujiandaa na michuano ya kimataifa msimu ujao ambayo Yanga huenda ikashiriki.

Yanga tayari imefanikisha usajili wa mabeki Shaban Djuma aliyemaliza mkataba AS Vita ya DR Congo na David Bryson wa KMC.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo tumezipata kutoka ndani ya benchi la ufundi la timu hiyo, Kocha Nabi ndiye aliyependekeza usajili wa wachezaji wawili katika kukiimarisha kikosi hicho.

Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, wachezaji hao ni chaguo lake kocha ambaye anaamini kama wakitua, basi wataisadia timu hiyo kutokana na uwezo na uzoefu wa kucheza michuano ya kimataifa.

Aliongeza kuwa, wachezaji hao aliowapendekeza ni kiungo mchezeshaji na mshambuliaji mmoja mwenye uwezo mkubwa wa kupachika mabao.

“Kocha Nabi amepewa majukumu yote ya kusimamia usajili kwa ajili ya msimu ujao, tayari amependekeza usajili wa wachezaji anaowahitaji.

“Nabi tayari ametoa mapendekezo ya usajili ukiwemo wa Bryson na Djuma baada ya kuridhishwa na uwezo wao.

“Pia kocha ametoa mapendekezo ya kusajili wachezaji wawili kutoka Tunisia, kati ya hao ni kiungo mchezeshaji na mshambuliaji mmoja,” alisema mtoa taarifa huyo.
 
Acha wafu wazikane!
huyu jamaa anaonekana ni kocha mzuri ila kama atawaleta wenzake atakuwa amekosea, Tunisia kwa sasa wana hali ya kushuka kiuchumi sasa ataokota ndugu zake huko yaje kuwa mambo ya maximo na kina jaja au zahera na kina molinga au kaze na kina fistoni

Huwa inaleta makundi na kupendeleana na mwishowe viwanja vyetu vinatukanwa wakati walijua wanakuja kwenye nchi ya aina gani
 
Wewe jamaa unaweweseka sana na Yanga, mara mseme usajili uliopita haukuwa kwa sababu wachezaji hawakupatikana kutokana na mapendekezo ya mwalimu, sasa mwalimu kalendekeza unakuja na hoja tofauti.
Ingekuwa unatoa hoja kuwa wachezaji wanaopendekezwa ni wabovu, hapo tungekuelewa. Kwa mchezaji mzuri pitch ya uwanja siyo kigezo sana. Tumwache mwalimu afanye kazi yake kwa uhuru.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Ni kawaida ya Makocha 90% wanaotoka nchi za mpira kupenda kwenda club wanasopata kazi pamoja na wachezaji kutoka kwao. Refer, Cedric Kaze na Ntibanzokiza pia Fiston, Wakina jaja na Cotinho, Mwinyi Zaheara na Wakina Molinga, Makambo nadhani case ni nyingi ..
Hao wa kwao ndio anaowajua vizuri kwa plan anayotaka..Kama anaweza kuwaleta awaleta ili mradi wawe wazuri na afanikiwe kwenye kamari yake..

Msianze kuogopa!
 
Wewe jamaa unaweweseka sana na Yanga, mara mseme usajili uliopita haukuwa kwa sababu wachezaji hawakupatikana kutokana na mapendekezo ya mwalimu, sasa mwalimu kalendekeza unakuja na hoja tofauti.
Ingekuwa unatoa hoja kuwa wachezaji wanaopendekezwa ni wabovu, hapo tungekuelewa. Kwa mchezaji mzuri pitch ya uwanja siyo kigezo sana. Tumwache mwalimu afanye kazi yake kwa uhuru.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
shida ni kwamba majembe yakitua karia anayafanyia hujuma
 
huyu jamaa anaonekana ni kocha mzuri ila kama atawaleta wenzake atakuwa amekosea, Tunisia kwa sasa wana hali ya kushuka kiuchumi sasa ataokota ndugu zake huko yaje kuwa mambo ya maximo na kina jaja au zahera na kina molinga au kaze na kina fistoni

Huwa inaleta makundi na kupendeleana na mwishowe viwanja vyetu vinatukanwa wakati walijua wanakuja kwenye nchi ya aina gani
Nakumbuka Kuna siku Fiston alillalamika kuwa wenzake hawampi pasi🤣
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom