Kama hii ni kweli, CCM Zanzibar ndiyo Bye Bye? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hii ni kweli, CCM Zanzibar ndiyo Bye Bye?

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Pascal Mayalla, Oct 6, 2010.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,518
  Trophy Points: 280
  Wanabodi,
  Haya ninayoyaandika ni maoni yangu binafsi ya nilichokishuhudia na nilicho ambiwa kuhusu kampeni za CCM, Zanzibar, kama ni kweli, basi October 31, CCM bye bye Zanzibar, wajiandae kuwa chama cha upinzani katika serikali mpya ya mseto.

  Leo nilipata kajinafasi kwenye muda wangu, hivyo nikaamua kutia timu Zanzibar.

  Kama moja ya viashiria vya ushindi ni wingi wa mabango, CCM imeshashinda Zanzibar kwa asilimia 90% na asilimia 10% iliyobaki ndio vyama vingine kwa jinsi mji wa Zanzibar ulivyoshehenezwa mabango ya CCM.

  Nimehudhuria kampeni ya CCM pale Kibanda Maiti ambapo mgeni rasmi ni JK mwenyewe. Tangu kuanza kwa kampeni, leo ndio nimebahatika kuhudhuria kampeni za CCM akiwemo JK mwenyewe ndani ya nyumba.

  Nimehudhuria kampeni za urais Zanzibar toka uchaguzi wa 1995, 2000, 2005 na sasa huu wa 2010, sijawahi kuona umati mkubwa wa watu kama niliuona leo hapo Kibanda Maiti. Hivyo tathmini yangu binafsi, kama ushindi ni umati wa watu, CCM imeshinda tena kwa
  asilimia 90% tena.

  Sambamba na umati huo, kwa haraka haraka unaweza kudhani ndio umati wa wananchi, la hasha!, asilimia 90% ya umati huu, ni ama wanachama wa CCM ama washabiki wa CCM
  na asilimia 10% ndio wanachi wa kawaida. Asilimia hii nimeipiga kufuatia mavazi, t-shirt, kofia, kanga na scalf.

  Uwanja wa Kibanda Maiti ukazungukwa na magari zile Chai Maharage za Zanzibar, mabasi na malori yaani ilikuwa ni vurugu mechi ya parking.

  Nikashuhudia wasanii mbali mbali wakipanda jukwaani wakiwemo ze comedy original, huku waandishi wa habari, tena waheshimiwa sana 'akiwemo mkuu wa wilaya' na wale wa magogoni, wamepiga ama sare za CCM ama "Press Kikwete 2010". Wajameni wanahabari!, hizi njaa zitatuua!, sikatai kufadhiliwa viwalo, ndio mmenunuliwa kabisa?.

  Ndipo nikafanya kajidodoso kadogo bila hojaji.

  Matokeo ya dodoso hiyo ndiyo yaliyopelekea kutoa opinion yangu kuwa baada ya October 31, 2010, CCM Zanzibar ni bye bye.

  Matokeo ya dodoso hiyo, yanafuatia hivi punde!
  Update
  Kwanza samahani sana wanabodi, jana nilishindwa kumaliza, nikitegemea ningemalizia usiku kabla sijajala, sasa wengine wetu tukisafiri ndio hivyo tena, kumbe unaweza ukamalizia kazi nyakati za usiku ukiwa home, sio ukiwa safari, Zanzibar nako!...

  Matokeo ya Dodoso ni haya.
  1.Nilimuuliza mwanahabari fulani aliyehudhuria uzinduzi wa kampeni za CCM na CUF kisiwani Unguja na jana alikuwepo kuhusu wingi wa watu, alikiri kuwa CCM kwa Unguja imeifunika CUF. Hivyo nikafikia conclusion 1. Kama ushindi ni wingi wa watu, basi CCM itashinda.
  2. Nikamuuliza hayo magari yalitapakaa hapo, akanijibu, ndio yamesomba watu toka kila kona ya kisiwa cha Unguja, yaani CCM imekodisha magari yote bila kujali ni ya nani, na kugawa fulana kwa wananchi wote bila kujali ushabiki wao, na kwa chini chini nasikia pia wameshikishwa na kidogo dogo cha nauli.
  3. Hivyo kuna uwezekano uwingi ule wa watu, sio tuu ni ushabiki kwa CCM au mapenzi yako kwa CCM, bali ni usafiri bute, fulana bure na kidogo dogo lakini siku ya kura, watapeleka yalipo mapenzi yao!.
  4. Aliniambia hata mikutano ya CUF, watu hujitokeza kwa wingi kama unavyoona mkutano wa CCM, tofauti ya CUF na CCM, ni kuwa wale washabiki wa CUF hawapewi nauli, hujigharimia kwa mifuko yao, hawapewi fulana na kofia za bure, wala hawalipwi sentano toka CUF ili wahudhurie, hivyo wanahudhuria mikutano ya CUF bila shinikizo lolote. Hawa sasa ndio washabiki wa ukweli wakati wenzao ni washabiki maandazi!.
  5. Kama ni kweli CCM imekodisha yale magari yote niliyoyaona jana, kama ni kweli CCM inagawa fulana, kofia, kanga na scuf kwa yoyote, na kama ni kweli, CCM inagawa kidogo dogo kwa hao wahudhuriaji mikutano yake ya kampeni kwa maoni yangu, hii inaweza kuwa ni kiashiria tosha kuwa October 31 kuna uwezekano mkubwa kwa CCM ndio Bye Bye Zanzibar!.

  Angalizo: Washabiki wa CCM msinitolee mimacho, haya ni maoni yangu tuu kwa kutumia freedom of expression bila kuingilia mchakato wa uchaguzi, kwani kama hizo hoja ni za uwongo, si mtashinda kwa kishindo! hivyo hakuna haja ya kutoleana lugha kali kali humu!

  Washabiki wa CUF pia msijifariji sana na mashabiki wenu ambao ni genuine, kunauwezekano hayo makundi yenu ni washabiki tuu na sio wapiga kura, hivyo jiandaeni kwa matokeo yoyote, sio mnapata kipigo halali na bado mnaendelea kulia lia.
   
 2. W

  We know next JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Lete habari Pasco lete habari, nacho fahamu mimi, Dr Shein hana ubavu wa kushindana na Seif hata siku moja.
   
 3. The Dreamer

  The Dreamer JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 1,280
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Zanzibar? Uchaguzi wao lini maaana uko mshindi na mshindwa ni serikali moja. Yaani ni kwamba hakuna upinzani..coalition gvt...Democrasia imechakachuliwa
   
 4. MwanaCBE

  MwanaCBE JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 1,773
  Likes Received: 544
  Trophy Points: 280
  We vipi!!!!
   
 5. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Pasco umeishiwa...! Ama ulipita Buyu na Shakani kuvizia nibu za dezo
   
 6. M

  Mkandara Verified User

  #6
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nawashauri CUF ambao wanategemea serikali ya Mseto watambue tu kwamba huku Bara Chadema anachukua nchi sasa huo Mseto sijui ndio utakuwa shubiri.. Ni bora kabisa CUF wajiandae kuongoza Zanzibar kwa ushirika waliopewa na Chadema kuliko kuunda serikali ya mseto na chama ambacho kitashindwa bara. Wazanzibar wamecheza tombola na hakika wana wasiwasi mkubwa baada ya kuweka muafaka ambao hauna afueni kwao.

  Mwisho, Dr.Slaa tinga Zanzibar na uwafahamishe Wazanzibar, Chadema ina wapa offer gani!..
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Pasco mbona umekimbia...njooo uwaambie CCM kuwa chama chao kimeshakufa kule Zanzibar kinasubiri Oktoba 31 kutimiza ada tu!
  Naona sasa hata Dr. Sheni anaona uvivu kufanya kampeni...unategemea nini wakati meneja wa kampeni CCM-Z'bar anakuwa Hafidh Ali Tahiri hata darasa la watu wazima hakusoma?
   
 8. hashycool

  hashycool JF-Expert Member

  #8
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 2, 2010
  Messages: 5,899
  Likes Received: 442
  Trophy Points: 180
  "unategemea nini wakati meneja wa kampeni CCM-Z'bar anakuwa Hafidh Ali Tahiri hata darasa la watu wazima hakusoma?"
  Duuuh nackia mawaziri wengi kule walowekwa na brazameni Karume ni vihiyo na karume mpaka leo anahangaika na Open university kwa miaka 10 sasa
   
 9. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #9
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu mkandara,
  Naona kama huelewi kwa nini CUF wamekubali serikali ya mseto. Ujuwe CUF haingekuwa na haja ya kukubali kuunda serikali ya mseto kama uchaguzi Zanzibar ungekuwa uhuru na haki na bila ya vurugu na mbinu chafu za CCM.

  Ukumbuke kuwa chaguzi zote CCM imeiba kura na matokeo na kusababisha umwagaji mkubwa wa damu. Ukumbuke wao ndiwo wenye dola na vyombo vyake, wao ndiyo waliouwa watu, wao ndiyo waliosababisha wakimbizi (shimoni Mombasa-Kenya), wao ndiyo waliochochea migawanyiko ya U-Pemba na U-Unguja, wao ndiyo waliokuwa tayari kufanya chochote mradi maamuzi ya wananchi yapinduliwe.

  CUF, kwa kuona hayo na kutafakari vizuri hiyo hali wameona wabadilishe mbinu ya mapambano, wameona kuwa CCM ni vin'gan'ganizi wa madaraka na hawatakubali kushindwa na wapo tayari kumwaga damu (kama una doubt nukta hii jiulize kwanini JWTZ litowe vitisho katika uchaguzi huu ambao CCM wamekabiliwa na hali ya upinzani usiotabirika?).

  Kinachofanywa na CUF ni kuwa-assimilate CCM katika serikali ya pamoja ili kupoza joto la kushindwa na kidogo kidogo watazowea na mwishowe watakubali kuwa demokrasia si ugomvi.

  Wazanzibar hawana hofu na serikali ya mseto, siku zote mabadiliko ya system iliyooza kwa mda mrefu ni faraja kwa wananchi. Wenzetu Kenya wameondowa system mbovu kwanza na mpaka sasa wamepiga hatuwa kubwa mpaka kubadilisha katiba ukiwatazama kimaendeleo wapo mbali hasa huku wakiwa wamepitwa na Tanzania kwa rasilimali nyingi zisizowafaidisha wananchi wake.

  Kama wao hawakuwa na hofu kufanya mabadiliko hayo kwanini Wazanzibari wawe na hofu.
  Ukiishi kuamini kuwa bila ya CCM nchi itayumba...ujuwe umasikini, maradhi na ujinga havitapunguwa hata siku moja...!

   
 10. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135

  kwanza pole sana

  nataka ujue wewe na maCUF wenzio safari hii mnaangukia pua maana mpaka kwenye ngome yenu kuu Pemba tutachukua viti tena si chini ya vitano

  jengine nataka ujue kuwa hadi sasa hakuna mkutano uliofanywa na CUF uliofunika wa CCM popote pale na hilo walijua


  bila ya kusita maCUF walitaka serikali ya pamoja kwa kujua weshapoteza mwelekeo na bila ya mtaji huo ndio CUF bye bye

  kuhusu upemba na uunguja ni suali lilopandikizwa na viongozi wa CUf kwa uroho wao wa madaraka na hiliinajulikana wazi

  kukimbi nchi hili nalo ni viongozi wenu kuchochea vurugu na uhasama na ukitaka kujua jiulize kwa nn Salim Msabah alijiondoa CUf hali akiwa muwakilishi jimbo la Mkunazini?

  jiandaeni kuangukia pua ila tutakuliwazeni kwa unakamo na tumeona kufanya hivi ili tuendelee maana nyny mkishindwa tu mnawachochea wananchi wakae vibarazani na kuiga stori baada ya kufanya kazi kuleta maendeleo

  nyny mna jadi ya fitna na choko choko na ukitaka kujua tembelea website Mzalendo.net utaona nn hasa nnamaanisha
   
 11. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,095
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kwa kuenzia kufa kwa CUF inatokana na hawa viongozi wa huku kujiona wao watukufu au bora kuliko hawa wenzao au wanawaita magozi
   
 12. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 418,551
  Trophy Points: 280
  Kwa kipimo hiki, basi CCM ni "BYE-BYE" bara:-

   
 13. K

  Kifoi JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: May 12, 2007
  Messages: 836
  Likes Received: 232
  Trophy Points: 60
  kwa wale wanao tegemea Chadema kushinda hivi kweli Munaimani na NEC ya Lewis Makame na Kiravu??????????????
   
 14. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,491
  Likes Received: 1,220
  Trophy Points: 280
  CUF ngangari kinoma huko zenji
   
 15. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  mkuu hivi hafidh ali tahir ndo meneja wa kampeni? huyu ni rafiki sana wa bilal
   
 16. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,518
  Trophy Points: 280
  Matokeo ya dodoso hiyo, yanafuatia hivi punde!
  Update
  Kwanza samahani sana wanabodi, jana nilishindwa kumaliza, nikitegemea ningemalizia usiku kabla sijajala, sasa wengine wetu tukisafiri ndio hivyo tena, kumbe unaweza ukamalizia kazi nyakati za usiku ukiwa home, sio ukiwa safari, Zanzibar nako!...

  Matokeo ya Dodoso ni haya.
  1.Nilimuuliza mwanahabari fulani aliyehudhuria uzinduzi wa kampeni za CCM na CUF kisiwani Unguja na jana alikuwepo kuhusu wingi wa watu, alikiri kuwa CCM kwa Unguja imeifunika CUF. Hivyo nikafikia conclusion 1. Kama ushindi ni wingi wa watu, basi CCM itashinda.
  2. Nikamuuliza hayo magari yalitapakaa hapo, akanijibu, ndio yamesomba watu toka kila kona ya kisiwa cha Unguja, yaani CCM imekodisha magari yote bila kujali ni ya nani, na kugawa fulana kwa wananchi wote bila kujali ushabiki wao, na kwa chini chini nasikia pia wameshikishwa na kidogo dogo cha nauli.
  3. Hivyo kuna uwezekano uwingi ule wa watu, sio tuu ni ushabiki kwa CCM au mapenzi yako kwa CCM, bali ni usafiri bute, fulana bure na kidogo dogo lakini siku ya kura, watapeleka yalipo mapenzi yao!.
  4. Aliniambia hata mikutano ya CUF, watu hujitokeza kwa wingi kama unavyoona mkutano wa CCM, tofauti ya CUF na CCM, ni kuwa wale washabiki wa CUF hawapewi nauli, hujigharimia kwa mifuko yao, hawapewi fulana na kofia za bure, wala hawalipwi sentano toka CUF ili wahudhurie, hivyo wanahudhuria mikutano ya CUF bila shinikizo lolote. Hawa sasa ndio washabiki wa ukweli wakati wenzao ni washabiki maandazi!.
  5. Kama ni kweli CCM imekodisha yale magari yote niliyoyaona jana, kama ni kweli CCM inagawa fulana, kofia, kanga na scuf kwa yoyote, na kama ni kweli, CCM inagawa kidogo dogo kwa hao wahudhuriaji mikutano yake ya kampeni kwa maoni yangu, hii inaweza kuwa ni kiashiria tosha kuwa October 31 kuna uwezekano mkubwa kwa CCM ndio Bye Bye Zanzibar!.

  Angalizo: Washabiki wa CCM msinitolee mimacho, haya ni maoni yangu tuu kwa kutumia freedom of expression bila kuingilia mchakato wa uchaguzi, kwani kama hizo hoja ni za uwongo, si mtashinda kwa kishindo! hivyo hakuna haja ya kutoleana lugha kali kali humu!

  Washabiki wa CUF pia msijifariji sana na mashabiki wenu ambao ni genuine, kunauwezekano hayo makundi yenu ni washabiki tuu na sio wapiga kura, hivyo jiandaeni kwa matokeo yoyote, sio mnapata kipigo halali na bado mnaendelea kulia lia.
   
 17. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,518
  Trophy Points: 280
  Nimesha update pale juu
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,578
  Likes Received: 18,518
  Trophy Points: 280
  Rutashubanyuma na washabiki wa makundi ya watu, msijitabirie ushindi kwa kipimo cha makundi ya watu, wengine ni kweli huenda tuu kushangaa helcopter na wengine kufuata vikundi vya burudani tuu lakini sio wapiga kura!.

  Mimi ni mmoja wa waliotangaza mwelekeo wa ushindi kwa Chadema wakati wa uchaguzi mdogo wa Busanda na Biharamulo kutiokana na makundi makubwa ya watu kwenye mikutano ya Chadema, na CCM ilikuwa inatilisha huruma licha ya 'Tingatinga' lao kuongoza mashambulizi, lakini bado Chadema ilifunika mwanzo mwisho!, Matokeo yalipotangazwa, mbona uso ulinishuka!.

  Umati usiwe kipimo, kipimo ni commitment na wachezaji haswa wa ile game ya October 31, tusichuuzwe na washangiliaji tuu!. Ndio maana kuna mahali nilisema Online polls karibu zote zinaelekea upande mmoja, ila kumbuka most of online voters ni washangiliaji na watazamaji tuu wa game ya October 31 na sii wachezaji!.
   
 19. M

  Mkandara Verified User

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu najua sana CUF wamefanya nini na kama unakumbuka niliwaambieni mnafanya makosa makubwa sana kukubali muafaka kwa faida ya CCM ambao walikuwa wakichukiwa na watu wengi Zanzibar (kama Bara). Na ktk mahesabu ya CCM walijua fika kwamba mwaka huu hawataweza tena kuiba kura kihahisi Zanzibar ushindi ni wa CUF. Hata nguvu ya dola inaweza tu kutumika sehemu moja na sio visiwa vyote. Kushindwa kwa CCM kulikuwa Obvious hakuna hila isipokuwa....

  Ndipo walipokuja na hili la Muafaka ili kuondoa chuki ya wananchi kwa CCM ili kuunda umoja na urafiki na CUF hali hakuna urafiki huo..Na leo hii CCM inaonekana kama sii chama kibaya visiwani na wabaya wao wako bara, hali wachawi wapo palepale Visiwani..Na asikwambie mtu ati kwamba hawa viongozi kina Karume, Salmin Amour, Seif Hamad, Bilal na wengineo wanaweza kuungana kuunda kitu kimoja.. Haiwezekani. Na utofauti wao ni wa kiitikadi sio maswala ya uzawa hivyo uongozi hauwezi kukamilika ikiwa itikadi bado zinatofautiana kama ilivyokuwa toka enzi ya Sultan.

  Hivyo muafaka wote umeweza kurudisha uhalisia wa CCM visiwani na sasa hivi kuna dalili tosha za CCM kushinda visiwani ambako wao walikupigia mahesabu wakasahau huku bara wakidhania hakuna Upinzani. Lau kama CUF ingeungana na Chadema kwa malengo sawa na hayo ya muafaka na CCM, basi CUF wangesimama nafasi nzuri zaidi kwa kuwepo ktk uongozi wa bara (serikali kuu) na kikubwa zaidi kuongoza Zanzibar bila Ubia (mseto) na chama chochote. Na kikubwa zaidi uwezekanao wa Zanzibar kutambulika kama ni nchi ndani ya Muungano ingetimia pengine mwaka au miaka miwili tu baada ya ushindi. Lakini kwa ujinga wa huyo Seif amekubali kuwa Musolini kuweka muafaka na Hitler kwa hofu isokuwa na Ujasiri wa kusimamia haki ya wananchi wake.

  Mara zote nasema kwamba Mpiganaji, mwanamapinduzi yeyote anayesalimu amri na ku shake hands na devil, basi jua fika yeye mwenyewe uatabadilika na kuwa devil.. CUF ni a long run will become devil themselves - Natanguliza SAMAHANI...
   
 20. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Ungeunganisha hiyo update na ile main topic ili wana JF waweze kuipata kirahisi,
  bila ya hivyo wengine hawatoiona hapa.
   
Loading...