Kama hii ndio sababu ya maamuzi mliyochukua basi yanga mmchemsha kwelikweli | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hii ndio sababu ya maamuzi mliyochukua basi yanga mmchemsha kwelikweli

Discussion in 'Sports' started by Livanga, May 22, 2012.

 1. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Jana wakati nasikiliza kipindi cha michezo radio one nilisikitishwa sana na kauli ya kiongozi wa wazee Akilimali wa yanga ambao watanzania tulitegemea wangetumi busara zao kufanya maamuzi kwa maslahi ya Club matokeo yake ni kinyume kabisa kumbe wao wamefanya hivyo ili kumkomoa Mchunga. Jana Akilimali alisema wazi kuwa wamefanya hivyo kumkomoa Mchunga.

  Swali ni je kweli kama hiyo ndio sababu tunategemea soka la Tanzania kukua kwa hali hii ya maamuzi tena anasema ndio vizuri kama yanga wasipocheza? Ziko wapi busara zao kama wazee?
   
 2. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,005
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Zipi hizo?
   
 3. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Ingawa simpendi mchunga,hawa wazee sitaki kuwasikia hawana tija katika soka la sasa..Nchunga akomae nao mpaka dakk ya mwisho ili wajifunze kusoma katiba
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kinachosumbua kwenye timu zetu ni njaa tuu, mchunga wanamuonea tuu.
   
 5. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,812
  Likes Received: 1,055
  Trophy Points: 280
  mpira wa tanzania hauwezi kukua kwa sababu unaongozwa na watu wasio na uchungu nao. simba na yanga wanaotoa hela sio watoa maamuzi.
   
 6. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Ina maana wewe huoni wapi penye makosa katika maelezo ya Akilimali. How can he say tumefanya hivi haswaa ili kumkomoa Mchunga so what???!!! ITasaidia nini baada ya kumkomoa mchunga. Je yanga wasipocheza wananchi na washabiki wa Yanga watafurahi? Wazee kuweni na mantiki ya maamuzi na iwe mantiki yenye mashiko ya kumfanya kila mtu kuona kweli kuna umuhimu wa maamuzi yenu otherwise huu unakuwa kama ujinga tu. NB: mimi siko upande wowote wa wazee wala wala wa mchunga bali nataka mfunguke na muone mbele. Samahani kama nitakuwa nimekosea ila ukweli uwekwe wazi ili watu waelimike
   
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Hiyo yawezekana kuwa ilikuwa ni kauli yao binafsi Wazee kama si ya kwake binafsi msemaji(Mzee Akilimali) lkn nia yetu wana'yanga wengi wetu ni kuona sasa "Kilaza" Nchunga anakaa pembeni pale tunamweka mtu mwingine makini zaidi atayeweza kutufanya turudishe heshima zetu kwenye secta hii ya soka, full stop (.)
   
 8. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  Acha hizo,kama yanga wangechukua ubingwa,na huku wana madeni, nchunga mngemtoa madarakani?
  Na kwanini hoja ya kumtoa nchunga ilianzia kwenye mechi na simba,does it wangeifunga wangepata pointi zaid ya 3.
  Kama anayosema akilimali ni yake binafsi,tutaprove vipi?
   
 9. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #9
  May 24, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Narudia tena,kauli(kama walitoa) ya kwamba songombingo lote lililoanzishwa ni kwaajili ya kumkomoa Nchunga ilikuwa ni ya kwao(Wazee) sisi kama Yanga (kumbuka mimi ni Mwanachama) tulikuwa tunafanya yote hayo kwaajili ya kuinusuru team,bila Nchunga kung'oka pale pangeendelea kuchimbika.
  Na nikuhabarishe tu kampeni ya kumuondoa Nchunga haijasababishwa na mechi na Simba,lilianza pale tulipopoteza point 3 za Coastal plus wachezaji kutokulipwa mishahara na posho zao kwa wakati,na likachochewa zaidi na kipigo cha Simba,kwa hayo ilikuwa lazima a'go...tunashukuru MUNGU Nchunga ametambua hitaji letu na kuamua kutuachia team yetu,kwahiyo kama unampenda sana unaweza kwenda kujiunga naye mkaanzisha team yenu.
   
 10. Livanga

  Livanga JF-Expert Member

  #10
  May 25, 2012
  Joined: Apr 15, 2010
  Messages: 458
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Swala la kumpenda hapa halipo swala ni kuwa na hoja ya kutaka kumtoa na pia kufanya maamuzi kwa maslahi ya club na sio vinginevyo. Ukiwa kama mwanachama hakikisha unawaelimisha wanachama wenzio kufikiri kabla ya kutenda na kuwa na mantiki ya kutenda na pia kuwa na mtu mmoja wa kuongea kwa niaba ya club na sio kila mtu kuongea. Vilevile ingekuwa ilikuwa ni kauli yao kama wazee nyinyi wanachama wengine mlitakiwa kupinga mara moja lili kusafisha club kwa washabiki na wanahci kwa ujumla.
   
 11. yahoo

  yahoo JF-Expert Member

  #11
  May 25, 2012
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 3,424
  Likes Received: 363
  Trophy Points: 180
  ha! haaa! Anslem kumbe mwanachama kabisa! Ndo mana unamisimamo mikali kama alshababu! Anywayz,mimi ni mshabiki sana wa yanga,but ninatabia ya kutoshabikia uozo,jitahidini kuibadilisha timu yetu.Baada ya azam yanga ndo timu tajiri tz.BUTnaamini simba wanaviongozi wenye akili nyepesi na wapo wellorganized kuliko yanga (miaka yote) so badilikeni bwana!
   
 12. Gedeli

  Gedeli JF Gold Member

  #12
  May 25, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 452
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45

  timu zetu hazitafika mbali kwa staili hii kwa sababu kubwa mmoja tunashindwa kabisa kujipanga na kuendesha timu kwa umoja bila kutegemea wafadhili . hebu fikiria ugekuwepo mpango kila mwanachama wa yanga akichangia sh 1000 kwa mwaka nadhani yanga haitateteleaka lakini sasa uongozi uliopo madarakani ukipishana kidogo na wenye pesa manji basi kazi imeisha jama anafunga koki mwenyekiti utafanya nini mishahara ya wachezaji inaaza kuwa shida na madeni mengine yanaanza kuwa kibao huku mwekezaji anaanza kusema pembeni bila kumtoa huyo siweki pesa yangu na sisi vijana na wazee bila kutafakari tunashabikia bila kujali hata katiba sababu ya kitu kidogo mzuguko mwingine unaanza na huyu atakayepatikana akipishana tu na mwenye pesa mambo yanakuwa ni yaleyale
   
 13. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #13
  May 25, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,705
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Gedeli,
  1,000 kwa mwaka kwa kila mwanachama ni kidogo sana isingetosha kitu, hata hivyo nataka nikuambie Yanga sasa hivi ina wanachama wasiopungua 15,000 nchi nzima na ada ya uanachama kwa mwaka ni Tshs 14,000/= kwahiyo ikiwa kila Mwanchama hai wa Yanga atalipa ada yake ya mwaka kwa wakati account ya team itaingiza Tshs 210,000,000/= kwa mwaka, kumbuka kuna fedha za mishahara kutoka TBL,kwa wafadhili wachache ambao bado wana'inject kwa team,kodi za rasilimali mbalimbali za Club kama majengo ya Twiga na Jangwani na mapato ya uwanjani,katika hali ya kawaida tusingetegemea Club kama Yanga wachezaji wake na makocha walie njaa hata siku 1,na hiyo ndo ilikuwa point yetu,kwanini Mheshimiwa alikuwa hasimamii stahili za wachezaji na jopo lao la ufundi ambao ndo mhimili mzima wa Club.
  Na kama kutofuata katiba pande zote 2 zilikiuka katiba,waliofanya kikao cha kumpindua Nchunga hawakufuata katiba na hata Nchunga mwenyewe kwa kung'ang'ania kukaa madarakani wakati kazi ilishamshinda alikuwa anakiuka katiba pia,tatizo letu kila mtu akipata nafasi anataka achumie tumboni style ambayo inazidi kutengeneza mfumo wa utegemezi kwa wafadhili na hili ndo tatizo ambalo limekuwa likiendelea kutafuna Club hizi kongwe,right kama mawazo ya Yanga kuwa Kampuni enzi zile za kina Tarimba Abas na Mpondela yangefanyiwa kazi leo hii Yanga ingekuwa ni team ya level nyingine kabisa.
   
Loading...