Kama hii itakuwa ndivyo ilivyo, orijino komedi hongera. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hii itakuwa ndivyo ilivyo, orijino komedi hongera.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GAGL, Aug 28, 2011.

 1. G

  GAGL Senior Member

  #1
  Aug 28, 2011
  Joined: Aug 5, 2010
  Messages: 138
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Mwanzoni mwa mwaka huu kama si mwishoni mwaka jana, kipindi cha orijino komedi kinachorushwa kupitia TBC, kilirusha uchakavu na utelekezwaji wa makumbusho ya mzalendo wa kweli hayati Edward Moringe Sokoine. Kwa kweli palionesha hali mbaya sana pale.

  Leo nimepita pale nimeona kuna ujenzi unaendelea na bila shaka itakuwa ni sehemu ya uboreshaji wa makumbusho hayo. Kwa mara nyingine serikali inatimiza wajibu wake baada ya kusimangwa tena na vijana wanaoendesha maisha yao kwa kutumia vipaji na si elimu.

  Serikali imejaa wasomi na wataalamu wa kada mbalimbali ila wameshindwa kuona hata jambo hili lililo na impact kubwa katika historia ya nchi yetu hadi waliposimangwa na orijino komedi!

  Hivi hii serikali ni lini itatimiza wajibu wake kwa hiari? Hongereni sana orijino komedi.
   
 2. only83

  only83 JF-Expert Member

  #2
  Aug 28, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  .....................Mkuu hiyo ni danganya toto ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika.Serikali yetu haiwezi fanya mambo bila kupata msukumo,ni serikali ya kusukumwa tu.Miaka nenda rudi makumbusho yale waliyatelekeza bila hata kufagia,pakageuka maficho ya wahuni na wavuta bangi,pakawa ndio choo cha kujisaidia...sasa tunapokaribia miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika ndio wanastuka....hii serikali inatia hasira sana...
   
 3. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #3
  Aug 28, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  <br />
  <br />
  hapa kwel?. Wadanganyika.
   
 4. NewDawnTz

  NewDawnTz JF-Expert Member

  #4
  Aug 28, 2011
  Joined: Nov 15, 2010
  Messages: 1,675
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0

  Ni vema kuwapa heshima waliofanya kazi kubwa kwa taifa hili........wasiwasi wangu ni hiyo bajeti iliyotumika hapo...sitaki kuifahamu inaweza poteza mood!!!!!!
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Aug 29, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sitoshangaa hata kidogo kusikia EL na yule mtoto wa marehemu Sokoine ambaye pia ni mbunge wa kuteuliwa (ccm) wanatanganza kufanya MISA maalum/ufunguzi wa hiyo memorial site!
   
Loading...