Kama haya yanampata Waziri wa nchi, je mwananchi wa kawaida itakuaje?

ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,263
521
Waliomuibia Dk Chami waendeleza ubabe
Saturday, 15 October 2011 07:56
Daniel Mjema, Moshi
KUNDI la wahalifu linalodaiwa kuvunja nyumba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Cyrill Chami na kuiba vitu mbalimbali usiku wa kuamkia juzi, limetishia kuendeleza uhalifu katika familia ya waziri huyo.
*
Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma kutuma kikosi cha polisi wa pikipiki, iteligensia na upelelezi juzi ili kuwasaka wahalifu hao, kundi hilo lilirudi tena katika nyumba hiyo usiku wa kuamkia jana.
*
Habari za uhakika zilizopatikana jana, zilisema tukio la wezi hao kuingia nyumbani kwa Dk Chami ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), lilitokea Kijiji cha Manushi, Kibosho usiku wa kuamkia juzi.
*
Kamanda Mwakyoma alipotafutwa jana, alikataa kuzungumza lolote kwa hoja kwamba hakuwa mahali pazuri pa kufanya hivyo, lakini Dk Chami alisema hakuwapo wakati tukio hilo likitokea.
Kwa mujibu wa Dk Chami katika kundi hilo, yupo mhalifu sugu maarufu ‘Askofu’ na kwamba ametishia kumuua mama yake mzazi, Agness Chami kama njia ya kulipiza kisasi.
*
“Ametishia kumchinja mama yangu kwa sababu alimtaja Askofu baada ya polisi kufika kijijini hapo, amedhamiria, hata usiku wa kuamkia leo (jana) 'Askofu' na kundi lake walikuja tena nyumbani,”alifafanua Dk Chami.
*
Waziri Chami alisema kutokana na vitisho hivyo, jana aliwasiliana na Kamanda Mwakyoma ambaye alimshauri amhamishe mama yake na kumpeleka eneo lenye usalama wakati polisi wakimsaka mhalifu huyo.
*
Akizungumzia tukio hilo, Dk Chami alisema siku hiyo usiku, wezi walivunja milango miwili ya nyumba yake na kuiba vitu mbalimbali vya elektroniki.
*
“Unajua walipanga wavamie ile nyumba wakati mimi nipo kwa sababu wanajua nimekuja kwa ziara ya jimboni, lakini bahati nzuri mimi sikuwa nimelala humo, nafikiri tungekuwa tunazungumza mengine,”alisema.
*
Waziri Chami alisema baada ya kuvunja milango hiyo miwili, waliingia ndani na kuiba televisheni moja, mashine ya DVD, seti ya muziki na begi kubwa la nguo ambalo walidhani kuna fedha au bastola.
*
*“Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba huyu 'Askofu' siku zote hatajwi kwenye vyombo vya dola kwa sababu anaogopwa sana na hili limempa nguvu ya kufanya hayo anayoyafanya bila uwoga wa kukamatwa,”alisema.
*
Chami alisema anaamini polisi wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao. Alisema tishio la kuuawa kwa mama yake limeripotiwa polisi.
source:Gazeti mwananchi
 
Kimbunga

Platinum Member
Oct 4, 2007
14,869
9,820
Duh mkuu mbona inatisha.Waziri wa Serikali ambaye ni mjumbe wa Baraza la mawaziri anapiga mayowe kwamba mama yake anakaribia kuchinjwa na "askofu" itakuwaje sisi wavuja jasho na mama zetu!! Duh hii noma yaani huyo askofu hatajwi na inaonekana waziri naye alikuwa anamfahamu lakini hakumtaja hata kwa waziri mwenzake hadi Mama yake alipomtaja na kutishia kumchinja!! kwa nini waziri hakumuuma sikio waziri mwenzake juu ya huyo mhalifu au ndio mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu yaani hadi ameguswa ndio anamtaja.
 
Kweli inashangaza sana,huyu waziri angeweza kabisa kumstua waziri wa mambo ya ndani manake wote wako kwenye level moja ya uwaziri,au angemfuata IGP apige nae story kidogo,au hawa jamaa hawana ushirikiano?sasa hapo ni waziri ambaye yeye alitakiwa kusimamia mpaka askofu apatikane anaanza kutetemeka na kulialia ovyo,na huyu askofu ambaye alikuwa hamna mwananchi yoyote aliyethubutu kumtaja mpaka waziri ni hatari sana,huyo atakua ameliteka hilo jimbo lote.Askofu akipatikana dawa yake ni kupigwa risasi hapohapo hatakiwi kucheleweshwa manake inaonekana ni mtu hatari sana.
 
We Know Next

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
797
363
Nilisha wahi kusema kuwa, hawa viongozi wasidhani kwa vile wao wapo salama na walinzi masaa 24, basi na familia zao zipo salama. Nilisema, haya wanayofanyiwa watanzania maskini yatalipizwa tu kwa familia za hawa watu waporaji na walioko serikalini, wanaojifanya wameziba masikio. Na bado, huo ndo mwanzo tegemeeni makubwa zaidi ktk familia za hawa wakubwa. Hembu fikirieni, watu wanauawa, akina mama Igunga wanauawa, mnafikiri yatapita hivihivi? uchungu huo ni lazima utawarudia na wao. Shauri yenu, mmeyataka wenyewe haya... na bado.
 
Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
7,938
Duh mkuu mbona inatisha.Waziri wa Serikali ambaye ni mjumbe wa Baraza la mawaziri anapiga mayowe kwamba mama yake anakaribia kuchinjwa na "askofu" itakuwaje sisi wavuja jasho na mama zetu!! Duh hii noma yaani huyo askofu hatajwi na inaonekana waziri naye alikuwa anamfahamu lakini hakumtaja hata kwa waziri mwenzake hadi Mama yake alipomtaja na kutishia kumchinja!! kwa nini waziri hakumuuma sikio waziri mwenzake juu ya huyo mhalifu au ndio mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu yaani hadi ameguswa ndio anamtaja.

Maajabu makubwa, kwamba waziri anamfahamu jambazi husika tena maarufu Askofu lakini hajawahi kuthubutu kumwambia waziri mwenzake ama IGP ama RPC kwamba kuna jambazi sugu Askofu hapo moshi vijijini hadi mama yake alipotishiwa kifo ndio anasema tena kupitia magazetini.

Like faza like son. Kikwete anawafahamu wauza unga na wala rushwa lakini hawachukulii hatua, Chami naye anafuata nyayo za mkuu wake.
 
Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,857
10,361
Mbona anamtishia familia yake au wana ugomvi zaidi ya kuiba tv??maana wanajua kuwa ni askofu aliekuja na amekuja tena isije kuwa visasi vya biashara au uchaguzi!!kwa nn avamie wakati waziri akiwa jimboni???
 
Daudi Mchambuzi

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
58,606
116,759
Waliomuibia Dk Chami waendeleza ubabe
Saturday, 15 October 2011 07:56
Daniel Mjema, Moshi
KUNDI la wahalifu linalodaiwa kuvunja nyumba ya Waziri wa Viwanda, Biashara na Masoko, Dk Cyrill Chami na kuiba vitu mbalimbali usiku wa kuamkia juzi, limetishia kuendeleza uhalifu katika familia ya waziri huyo.
*
Licha ya Kamanda wa Polisi Mkoa Kilimanjaro, Absolom Mwakyoma kutuma kikosi cha polisi wa pikipiki, iteligensia na upelelezi juzi ili kuwasaka wahalifu hao, kundi hilo lilirudi tena katika nyumba hiyo usiku wa kuamkia jana.
*
Habari za uhakika zilizopatikana jana, zilisema tukio la wezi hao kuingia nyumbani kwa Dk Chami ambaye pia ni Mbunge wa Moshi Vijijini (CCM), lilitokea Kijiji cha Manushi, Kibosho usiku wa kuamkia juzi.
*
Kamanda Mwakyoma alipotafutwa jana, alikataa kuzungumza lolote kwa hoja kwamba hakuwa mahali pazuri pa kufanya hivyo, lakini Dk Chami alisema hakuwapo wakati tukio hilo likitokea.
Kwa mujibu wa Dk Chami katika kundi hilo, yupo mhalifu sugu maarufu ‘Askofu' na kwamba ametishia kumuua mama yake mzazi, Agness Chami kama njia ya kulipiza kisasi.
*
"Ametishia kumchinja mama yangu kwa sababu alimtaja Askofu baada ya polisi kufika kijijini hapo, amedhamiria, hata usiku wa kuamkia leo (jana) 'Askofu' na kundi lake walikuja tena nyumbani,"alifafanua Dk Chami.
*
Waziri Chami alisema kutokana na vitisho hivyo, jana aliwasiliana na Kamanda Mwakyoma ambaye alimshauri amhamishe mama yake na kumpeleka eneo lenye usalama wakati polisi wakimsaka mhalifu huyo.
*
Akizungumzia tukio hilo, Dk Chami alisema siku hiyo usiku, wezi walivunja milango miwili ya nyumba yake na kuiba vitu mbalimbali vya elektroniki.
*
"Unajua walipanga wavamie ile nyumba wakati mimi nipo kwa sababu wanajua nimekuja kwa ziara ya jimboni, lakini bahati nzuri mimi sikuwa nimelala humo, nafikiri tungekuwa tunazungumza mengine,"alisema.
*
Waziri Chami alisema baada ya kuvunja milango hiyo miwili, waliingia ndani na kuiba televisheni moja, mashine ya DVD, seti ya muziki na begi kubwa la nguo ambalo walidhani kuna fedha au bastola.
*
*"Tatizo ninaloliona hapa ni kwamba huyu 'Askofu' siku zote hatajwi kwenye vyombo vya dola kwa sababu anaogopwa sana na hili limempa nguvu ya kufanya hayo anayoyafanya bila uwoga wa kukamatwa,"alisema.
*
Chami alisema anaamini polisi wataendelea kutekeleza wajibu wao wa kulinda raia na mali zao. Alisema tishio la kuuawa kwa mama yake limeripotiwa polisi.
source:Gazeti mwananchi
Kwa nini Chami anadhani waizi hawa walitarajia kukuta pistola na pesa kwenye bag???
 
NDOFU

JF-Expert Member
Feb 23, 2009
656
144
Mbona anamtishia familia yake au wana ugomvi zaidi ya kuiba tv??maana wanajua kuwa ni askofu aliekuja na amekuja tena isije kuwa visasi vya biashara au uchaguzi!!kwa nn avamie wakati waziri akiwa jimboni???

Kilichonishtua ni ile kauli ya kuwa wakachukua na begi kubwa la nguo wakidhani kuna HELA AU BASTOLA.Inamaana waziri anajua anachokitafuta Askofu?!
 
Samkyjr

JF-Expert Member
Mar 21, 2011
363
62
Waziri mzima hana maadiri ya uongozi , labda wakianza kuguswa nao na shida za majambazi na wapiga nondo kama mbeya watajaribu kuchukua hatua.
 
montroll

JF-Expert Member
Jul 31, 2011
319
126
Kweli inashangaza sana,huyu waziri angeweza kabisa kumstua waziri wa mambo ya ndani manake wote wako kwenye level moja ya uwaziri,au angemfuata IGP apige nae story kidogo,au hawa jamaa hawana ushirikiano?sasa hapo ni waziri ambaye yeye alitakiwa kusimamia mpaka askofu apatikane anaanza kutetemeka na kulialia ovyo,na huyu askofu ambaye alikuwa hamna mwananchi yoyote aliyethubutu kumtaja mpaka waziri ni hatari sana,huyo atakua ameliteka hilo jimbo lote.Askofu akipatikana dawa yake ni kupigwa risasi hapohapo hatakiwi kucheleweshwa manake inaonekana ni mtu hatari sana.

Umepotea hapo mwisho mkuu,
yaani akikamatwa tu auawe! Hapana.

Akikamatwa apimwe akili na IQ yake.
Mtu binafsi asiye na mamlaka yoyote kuweza kuitiisha na kuitisha serikali hadi kumfanya waziri wake alielie na kutetemeka, anaweza kuwa mtu muhimu sana.

Uwezo wake umetokana na nini?
Motive yake ni nini?
Alisoma wapi na kulelewa na nani na katika mazingira yapi?
Tunawza kujifunza mengi tu ya kutusaidia.
Kumwua mhalifu kwa hasira na chuki si sahihi kwa mtazamo wangu.
Lets for reasons.
Lets reason with them if we can get an oportunity.
Ni kwa njia hii tu, tunaweza kuhakikisha askofu mwingine hatokei.
Ni mawazo yangu tu.
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,882
Nilisha wahi kusema kuwa, hawa viongozi wasidhani kwa vile wao wapo salama na walinzi masaa 24, basi na familia zao zipo salama. Nilisema, haya wanayofanyiwa watanzania maskini yatalipizwa tu kwa familia za hawa watu waporaji na walioko serikalini, wanaojifanya wameziba masikio. Na bado, huo ndo mwanzo tegemeeni makubwa zaidi ktk familia za hawa wakubwa. Hembu fikirieni, watu wanauawa, akina mama Igunga wanauawa, mnafikiri yatapita hivihivi? uchungu huo ni lazima utawarudia na wao. Shauri yenu, mmeyataka wenyewe haya... na bado.

Umesema maneno mazito kabisa sina la kuongeza .
 
Binti Magufuli

JF-Expert Member
Apr 2, 2011
7,480
5,109
Mbona anamtishia familia yake au wana ugomvi zaidi ya kuiba tv??maana wanajua kuwa ni askofu aliekuja na amekuja tena isije kuwa visasi vya biashara au uchaguzi!!kwa nn avamie wakati waziri akiwa jimboni???

Huyu waziri anaiba mpaka mademu wa watu...yule demu wake mweupe mrombo alimnyang'anya mmasai wa watu pale udsm, yani jamaa alikuwa anasaidia madesa na mambo yote ya muhimu kwa demu, ila waziri alipotuma messenger aitiwe huyu demu mrombo mmasai wa watu hakuona ndani
 
Buto

JF-Expert Member
Sep 23, 2011
250
29
Sasa waziri analalamika nn?Hata kama mama yake akiuliwa na Askofu si atazikwa na Askofu? Majambazi wote wanajuana hawa na inaonekana wamedhulumiana ndio mana Askofu kasema atalipiza kisasi! Ccm oyeeee
 
ureni

JF-Expert Member
Jun 14, 2011
1,263
521
Umepotea hapo mwisho mkuu,
yaani akikamatwa tu auawe! Hapana.

Akikamatwa apimwe akili na IQ yake.
Mtu binafsi asiye na mamlaka yoyote kuweza kuitiisha na kuitisha serikali hadi kumfanya waziri wake alielie na kutetemeka, anaweza kuwa mtu muhimu sana.

Uwezo wake umetokana na nini?
Motive yake ni nini?
Alisoma wapi na kulelewa na nani na katika mazingira yapi?
Tunawza kujifunza mengi tu ya kutusaidia.
Kumwua mhalifu kwa hasira na chuki si sahihi kwa mtazamo wangu.
Lets for reasons.
Lets reason with them if we can get an oportunity.
Ni kwa njia hii tu, tunaweza kuhakikisha askofu mwingine hatokei.
Ni mawazo yangu tu.

Mimi kilichonisukuma mpaka nione kua anahitajika kupigwa risasi ni kuwa nahuhakika katika nchi kama yetu Tanzania iliyojaa rushwa askofu akikamatwa lazima ataachiwa baada mda mfupi hata kama akifungwa baada ya mda utasikia yuko nje kwa msamaa wa rais kwa hiyo piga ua lazima atapata mda wa kulipiza kisasi tu,kwa hiyo nikaona uamuzi sahihi ni kummaliza tu.
Maoni yako ni mazuri kwa nchi zilizoendelea ambapo mambo ya rushwa yako kwa kiwango kidogo.Kama Marekani au Uingereza,ukija in reality nchi kama yetu huo mda hawana wanachoangalia ni fedha tu na rushwa kwa wingi.
 
Umesema vema, kulingana na mfumo na utamaduni wetu. Lakini naamini hata wewe mwenyewe unajua hiyo si sahihi.
Tusimpe ushindi kaburu Botha,kuhusu sisi waafrika na uduni wetu!

Utamaduni gani wetu huu?
Nahisi kuuchukia utamaduni wetu wa kiaafrika kwani yaelekea ndio chimbuko na msingi wa mapungufu yetu yote.
Tunaweza kufuta utamaduni wetu na kuuandika upya kama tunavyo andika upya katiba?
Naomba Mungu iwe inawezekana kubadilisha utamaduni!
Utamaduni gani unaoruhusu i sukuma jamii kumchoma moto mwizi wa simu ya sh 15000 au kuku wa sh 3000 na kumpongeza fisadi aliyefisidi mabilioni?
Askofu apigwe risasi?
Kina chenge,lowasa,rostam, mkapa nk
tume wafanya nini?
Si upendi utamaduni wetu.
Tuuandike upya.
 
Pancras Suday

JF-Expert Member
Jun 24, 2011
7,870
3,408
Najua majambazi sasa hivi wamegundua kuwa kwa wananchi hakuna cha kuchukua sasa wanakwenda kwa hao majambazi wenzao wa kutumia kalamu, sasa tuone itakuwaje
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

0 Reactions
Reply
Top Bottom