Kama haya tunayoyasikia yana ukweli, basi nampa hongera sana Mama, ila nina wasiwasi atalazimika kufanya reshuffle wakati wowote

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
47,011
144,371
Tunasoma mitandaoni kuwa kuna watu hivi sasa wanashikiliwa, watu ambao wanatajwa kuwa karibu na mtangulizi wa Mama yetu kwa tuhuma mbalimbali. Whistleblower wetu kule Twitter licha ya kumtaja jina mtuhumiwa, kaweka mpaka picha yake sambamba na tuhuma zinazomkabili huku akidai mtu huyo anashikiliwa.

Iwapo madai haya ni ya kweli, basi kuna hatari uchunguzi huo ukagusa wengi wakiwemo wale ambao Mama leo hii kaamua kufanya nao kazi kwani kunaweza kukawa na kutajana katika hatua za kujitetea, kukusanya ushahidi, n.k.

Hivyo,tutarajie kuona baadhi ya watu wakitakiwa kujiuzilu au kuondolewa katika nafasi zao kadri uchunguzi unavyoendelea.

Time will tell.
 
Back
Top Bottom