Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,597
- 215,272
Kama taarifa hii ya gazeti la Nipashe mwezi jana ina ukweli basi hii inaweza kuwa sababu ya Bwana Ndugai kumchukia CAG.
Dola milioni 12 kwa miezi 6 ni sawa na TZS Bilioni 27. Yani 4.6Bil kwa mwezi au Milioni 153 kwa siku. Yani kila akilala tunalipa 153Mil, siku ya kwanza, ya pili hadi ikatimia miezi 6.
Hapa kuna hoja kadhaa:
Mosi, ni ugonjwa wa Ndugai. Japokua ugonjwa ni siri yake na daktari lakini kwa kiongozi wananchi wanapaswa kujua kwa sababu ndio wanaogharamia matibabu. Mwalimu Nyerere alipolazwa St.Thomas tulitangaziwa ni saratani ya damu. Rais Mkapa alipolazwa Ujerumani tuliambiwa alifanyiwa upasuaji wa mguu. Hata Kikwete alipolazwa Johns Hopkins, USA tulijulishwa ni tezi dume. Ugonjwa wa kiongozi sio suala binafsi.
Pili, gharama zilizotumika ni kubwa sana. Lissu amelazwa miaka miwili kitandani lakini hajatumia hata robo ya pesa hizi, pamoja na 'operation' nyingi alizofanyiwa. Baraza la wazee Chadema limesema Ndugai hakutumia kiasi hicho cha pesa, bali alitumia ugonjwa wake kama njia ya kutakatisha fedha. Ndugai anatakiwa kuclear doubts, vinginevyo wananchi wataamini maneno ya wazee wa Chadema.
Tatu, Ndugai ameulizwa ni ugonjwa gani uliokua ukimsumbua hadi atumie 153mil kwa siku, badala ya kujibu swali akaanza kulaumu. Anasema watu waangalie thamani ya mtu sio kiwango cha pesa kilichotumika. Alipobanwa zaidi akasema huenda wanaouliza maswali hayo walitaka afe. Huu ni utetezi DHAIFU sana. Mtu kujua gharama za matibabu haimaanishi alitaka ufe. Tena hao wanaotaka kujua ndio waliokulipia. Sasa unawazuiaje haki yao ya kuhoji?
Nne, kama matibabu ya kiongozi mmoja yanatumia fedha nyingi kiasi hiki kwanini hizo pesa zisitumike kujenga hospitali nchini na wananchi wa kawaida watibiwe? Hospitali ya taifa Muhimbili (Mloganzila) ilijengwa kwa TZ 120Bil mkopo kutoka Korea kusini. Ndugai ametumia 27Bil kwa miezi 6. This means wakiugua akina Ndugai wanne tunajenga Mloganzila mpya.
Tano; Ripoti ya CAG inaonesha idadi ya viongozi kutibiwa nje imepungua lakini gharama zinaongezeka kila mwaka. Watu wakajiuliza hii paradox inawezekanaje? Leo majibu yamepatikana. Unazuia watu 100 ambao kwa pamoja wangetumia 1Bil. Unamruhusu mtu mmoja kutumia 27Bil. Ridiculous.!