Kama haya matokeo ni ya kweli tuna shida kubwa

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,605
8,744
1579267757102.png
 
mwl . nyerere alisema tusipowafundisha vizuri watoto wazungu watatuchunga kama wanyama wa serengeti. mwisho wa kunukuu. profesa shivji aliwahi kusema hata kama hakuna darasa watoto wakakaa chini ya mti ukampa mwl. motisha watoto watafaulu. mwisho wa kunukuu.

Serikali inacheza na mwl. na hawataki kuelewa ukweli huo watanzania wanaumizwa sana na walimu kwa kiwango kisichomithilika. angalia nyekundu na nyeusi asilimia zake hali ni mbaya sana

Nami nasema bila kumpa mwal motisha hata kama watoto watapewa kila moja na kitabu, madarasa mazuri, viti na meza nzuri ni kazi bure tu. kwa sasa habari ni biashara na shughuli nyingine zinazoweza kuingiza kipato shuleni walimu wapo kimwili sio kiakili. nalog off. Ova.
 
Ukifuatilia kwa makini, utagundua kwamba Shule za Taasisi binafsi na Watu Binafsi ndizo zinapandisha ufaulu.
Serikali inatakiwa kizipa motisha shule hizi badala ya kuziona kuwa zinafanya biashara na kutoza kodi kubwa kwenye taasisi hizi kiasi cha kushindwa kujiendesha baada ya kuelemewa na kodi mbali mbali.
 
Majanga ni mengi,wachukue walimu wa sekondari wapeleke msingi,unadhani wamefurahi kufanya wasichokisomea?
Sijui jafo mawazo hayo aliyatoa wapi,yaani kushauriwa tu kafanya kweli na watu wakampongeza,Sasa walimu wanagoma moyoni tu,wameacha kazi wanalinda ajira.
Serikali wataelewa tu,hata Kama kidogo kidogo,Moro Kuna jamaa Ana masters ya hesabu alikua sekondari,wamempeleka msingi,kapewa hisabati darasa la pili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua elimu ni msingi wa umoja. Ukiangalia vizuri matabaka ya kimaendeleo hata wanaosingizia ukanda elimu ni muhimu.Elimu ya sekondali ni muhimu kuliko hata chuo!. Hata hapa niliko USA 33.4% tu wenye degree au zaidi lakini elimu mpaka miaka 18 ni kama lazima. German wengi wanasoma kama kwenye VETA zetu hivyo elimu ya sekondari ni muhimu sana.

Kulikuwa na NGO ya ELIMU kwanza
 
Back
Top Bottom