Kama hawakumuenzi hayati Mwl Nyerere ndio watamuenzi hayati J.P. Magufuli? Yetu macho...

Nyankurungu2020

JF-Expert Member
Oct 2, 2020
4,087
6,568
Hayati baba wa Taifa alipong'atuka na kuliacha hili taifa mikonononi mwa warithi wake kwa namna alivyokuwa hapendi rushwa,ubadhirifu na uzembe hakuna mtu aliyetegemea kuwa litakuja kugeuka kuwa taifa la wanaCcm mafisadi na walarushwa.

Mpaka hayati JPM anapewa nafasi ya kugombea CCM ilikuwa imechafuka. Ndio maana alipoingia madarakani alijitahidi kusafisha uchafu na kubana ufisadi na ubadhirifu usifanyike. Ndio maana alikuwa na ndoto ya kuhakikisha anakamilisha miradi kama Sgr,JNHPP na kufufua mashirika ya umma kama Atcl kwa pesa za ndani.

Sasa hayati JPM amefariki tunasikia kila mwanaCcm tutaenzi yale mazuri aliyofanya hayati JPM. Je mtaweza kumuenzi? Mbona hata Baba wa taifa hakumuenzi na mkawa wapigaji wa pesa kupitia Kagoda,Epa,meremeta, Escrow n.k
 
Kutamka hivyo tu ni kuonyesha uzuri wa aliyoyafanya na kwamba yanapaswa kufuatwa.

Kama wanaongea kinafiki hilo ni Jambo lingine na watahukumiwa kwa kauli zao
 
Back
Top Bottom