Kama hawa Wazee Wanne wa Simba SC wakifanya wanachotaka Kukifanya kwa Hasira waliyonayo, Haji Manara anakuwa Chizi au Marehemu upesi

MINOCYCLINE

JF-Expert Member
Apr 2, 2015
8,011
16,748
Nimejaribu Kuwasihi mno wasifanye wanachotaka Kukifanya kwa Kitendo cha Haji Manara wakanionya ninyamaze vinginevyo nami pia watanijumuisha katika Kafara lao Kubwa wanaloenda kulifanya kwa Usaliti mkubwa na Dharau dhidi ya Simba SC.

Na Kilichonitisha zaidi kuna Wazee Wawili kati ya hawa Wazee Wanne ndiyo walishiriki katika kufanya Kafara baya na la Hatari ambalo lilitoa Uhai wa Wasaliti wa Simba SC Kundi la Simba Taliban wakiongozwa na Marehemu Ngumi Jiwe kwa kusababisha Ajali mbaya ya Basi lao Mkoani Singida wakielekea Kuisaliti Simba SC Mkoani Kagera ilipokuwa ikicheza na Kagera Sugar.

Maneno yao ya mwisho Kwangu Mightier ni kwamba ama nitegemee kuna Mtu anaenda kuwa Taahira au Marehemu Siku si nyingi na Salama yake awatafute Viongozi wa Simba SC na Mzee Mmoja wa Magomeni awaombe Radhi upesi ndani ya Siku 7 tu kutoka hii leo.

Yanga SC kuna Mtu mmeshamponza.
 
Hao wazee hawana lolote lile na hakuna baya litakalo mfika haji manara.

Kama wao kweli ni mabingwa wa ulozi na ndumba basi wangemroga MBUYU TWITE kwa kuchukua US$ 40,000 na kesho yake kusaini Young Africans huku akionyesha dharau kwa simba kwa kuvaa jersey ya yanga iliyoandikwa DALALI mgongoni

Ngedelec...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ndio Haji Manara, sirogeki, hamna uchawi wa kumdhuru mtu wa aina yangu.

Ngozi ba viungo vyangu ni uchawi tosha, ndio maana ili kunidhuru ni lazima utumie silaha na nguvu na sio uchawi
 
Nimegundua kua simba wameumia sana kwa haji kuingia yanga.

Fatilia tu nyuzi za humu ndani kuhusu manara 95% waanzishaji wake ni simba, yanga wao wametulia tu hata hawahangaiki na hii inshu, ila simba sasa mala kumpongeza CEO wao, kutaka kumuomba msamaha mo, kuishambulia yanga kua imelamba galasa aisee yaani tafrani.

Kumuongelea mtu mlietengana tayari hasa kwa kumkandia ni ishara ya kua umeumia na kuondoka kwake. Poleni simba.
 
Namkubali manara toka alivyokuwa simba pamoja sikuwa mshabiki wa simba jamaa namkubali kwa mchango wake katika mpira.
ameweza kutengeneza nafasi ya washabiki kuwa ya muhimu katika soka hivyo nategemea Yanga wataanza kwenda uwanjani kwa wingi kama simba walivyo hamasishwa.

Kwa ugomvi wa sasa amesema ukweli kile ambacho timu zetu imekuwa ikipoteza kwa kuwakumbatia hawa jamaa ambao wao wanatengeneza fedha sisi tunabaki na ushabiki tu japo ndivyo yanga linaenda kutokea siku si nyingi.

Kwa kweli mwacheni atumike atengeneze maisha simba wakimwitaji wamchukue kwa bei nyingine ambayo itamsaidia kuwa na maisha mazuri kushangilia timu wakati unanjaa ni ushamba kama wapo wachezaji ambao nafsi zao ziko yanga lakini inabidi waifunge yanga kwa kuwa wameajiriwa na simba itakuwa kwa mshabiki kuhama?

Wapo viongozi wa simba walikuwa yanga kwa maslahi wakaenda simba wakapiga hela na maisha yao yakaenda mwacheni kijana wa watu atafute muda alionao ukilinganisha na elimu yake ni mfupi mno akicheza vibaya atavuna mabua na hakuna atakayetunza watoto wake.
 
Mimi ndio Haji Manara, sirogeki, hamna uchawi wa kumdhuru mtu wa aina yangu.
Ngozi ba viungo vyangu ni uchawi tosha, ndio maana ili kunidhuru ni lazima utumie silaha na nguvu na sio uchawi
Hawawajui akina Salula hao
 
Back
Top Bottom