mtzedi
JF-Expert Member
- Dec 13, 2011
- 5,597
- 5,602
Ungemnunulia tu nyingine kumsaidia kuifanya iyo kazi ya Mungu ya ualimu.Jana katika kazi zangu za ujenzi wa taifa nilikuwa mjini Babati katika shule ya sekondari x. Miongoni mwa changamoto zinazowakabili walimu kwa sasa ni utovu wa nidhamu kutoka kwa wanafunzi wao.
Hebu fikiria mwanaJF mwenzangu hivi inakuwaje mwanafunzi anapata ujasiri wa kuiba baiskeli ya mwalimu wake!
Yule mwalimu aliyeibiwa baiskeli alituelezea kwa hisia mno jinsi alivyojibana hadi kupata baiskeli yake ambayo hakudumu nayo hata siku 2 mwanafunzi akaiotea.
Muhimu ni sisi wazazi au walezi kuwasaidia walimu katika kuwaform watoto wetu kimaadili ili kuwamotisha walimu kuwasaidie wanetu ktk masomo yao.
Ni kweli pia kwamba hata walimu wa zama hizi wana changamoto zao kimaadili lakini sisi kama wazazi au walezi tutimize wajibu wetu ktk malezi ili tuwe na kizazi bora kimaadili.
Naomba kuwasilisha