Kama hawa ndiyo wanafunzi wa leo basi walimu kazi ipo

mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
3,986
2,000
Jana katika kazi zangu za ujenzi wa taifa nilikuwa mjini Babati katika shule ya sekondari x. Miongoni mwa changamoto zinazowakabili walimu kwa sasa ni utovu wa nidhamu kutoka kwa wanafunzi wao.

Hebu fikiria mwanaJF mwenzangu hivi inakuwaje mwanafunzi anapata ujasiri wa kuiba baiskeli ya mwalimu wake!

Yule mwalimu aliyeibiwa baiskeli alituelezea kwa hisia mno jinsi alivyojibana hadi kupata baiskeli yake ambayo hakudumu nayo hata siku 2 mwanafunzi akaiotea.

Muhimu ni sisi wazazi au walezi kuwasaidia walimu katika kuwaform watoto wetu kimaadili ili kuwamotisha walimu kuwasaidie wanetu ktk masomo yao.

Ni kweli pia kwamba hata walimu wa zama hizi wana changamoto zao kimaadili lakini sisi kama wazazi au walezi tutimize wajibu wetu ktk malezi ili tuwe na kizazi bora kimaadili.

Naomba kuwasilisha
Ungemnunulia tu nyingine kumsaidia kuifanya iyo kazi ya Mungu ya ualimu.
 

to yeye

JF-Expert Member
May 30, 2016
4,709
2,000
walimu tuna hali ngumu.mi nilipanda mbegu ya muda mfupi ya mahindi mwanzo wa December wameshaanza kuyatoboatoboa kuchungulia kama yamekomaa.nikijaaliwa kaz nyingine hii mi naacha kiukweli
 

Aigoo

JF-Expert Member
Feb 27, 2015
3,069
2,000
Unaweza kuta alie muibia sio mwanafunz ni mwalimu mwenzake... Binadamu hatuko sawa kuna watu ni vichwa maji hata uwakanye au kuwafundisha hawabadiliki
 

Adrian Stepp

JF-Expert Member
Jul 1, 2011
2,501
2,000
walimu tuna hali ngumu.mi nilipanda mbegu ya muda mfupi ya mahindi mwanzo wa December wameshaanza kuyatoboatoboa kuchungulia kama yamekomaa.nikijaaliwa kaz nyingine hii mi naacha kiukweli

Nimecheka sana ..pole aiseee..ha ha ha!
 

SPINE

JF-Expert Member
Dec 11, 2017
1,012
2,000
Vituko mashuleni vipo vingi sana, kutokana na utandawazi wa sasa ndio maana inaonekana kama ni tatizo kubwa, hiyo hali ipo tangu hapo awali....maadili kwa mwanafunzi sio jukumu la mwalimu peke yake, wazazi na walezi ni vyema kushiriki kikamilifu ili kujenga jamii iliyo bora.
 

mtzedi

JF-Expert Member
Dec 13, 2011
3,986
2,000
walimu tuna hali ngumu.mi nilipanda mbegu ya muda mfupi ya mahindi mwanzo wa December wameshaanza kuyatoboatoboa kuchungulia kama yamekomaa.nikijaaliwa kaz nyingine hii mi naacha kiukweli
Naona walimu mnatoa ya moyoni.
 

Chris14

JF-Expert Member
Oct 2, 2017
3,084
2,000
Huu uzi unanifikkirisha na kunichekesha sana..kwa mfano, umeelewa nini hapa "Yule mwalimu aliyeibiwa baiskeli alituelezea kwa hisia mno jinsi alivyojibana hadi kupata baiskeli yake ambayo hakudumu nayo hata siku 2 mwanafunzi akaiotea"
Ni mmoja ya wale wahanga wa mikopo ya mabenki ambao hupokea pesa kidogo.
 

nyanimzungu

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,207
2,000
Wizi upo tangu zamani, siku hizi mmefanya kama ni kitu kipya ambacho hakikuwahi kutokea.
Aliyeiba baiskeli ni mwizi, ilitokea tu kwamba alikuwa anasoma hiyo sekondari, lakini ni mwizi.
Hata matajiri ni wezi, wizi sio swala masikini ni tabia ya mtu.
Wizi sio swala la,maadili ni tabia ya mtu, ndio maana utaona mapadri au masheikh wazinzi.
Tabia hizi zimekuwepo tangu B.C.
Hilo jina lako mkuu limekaa kichatochato
 

nyanimzungu

JF-Expert Member
Mar 4, 2017
1,207
2,000
walimu tuna hali ngumu.mi nilipanda mbegu ya muda mfupi ya mahindi mwanzo wa December wameshaanza kuyatoboatoboa kuchungulia kama yamekomaa.nikijaaliwa kaz nyingine hii mi naacha kiukweli
Ha ha ha ha walimu dizain yako ndo wale wapole hata kushika bakora hawajui.kuwa kama mm kabla sijaingia class napiga cha arusha halafu nabeba bakora yangu matata ambayo naweza chapa shule nzima na isikatike.watoto wananiogopa kama kipindupindu hakuna wakuthubutu kuniwazia jambo baya
 

loosimingori

JF-Expert Member
Oct 30, 2017
922
1,000
walimu tuna hali ngumu.mi nilipanda mbegu ya muda mfupi ya mahindi mwanzo wa December wameshaanza kuyatoboatoboa kuchungulia kama yamekomaa.nikijaaliwa kaz nyingine hii mi naacha kiukweli
kuacha kazi sio suluhisho kila kazi inachangamoto zake.Kumbuka tunafanya dhambi lakini viongozi wa dini hawaachi kazi kikubwa ni kuhimiza wazazi na walezi kutekeleza majukumu yao ktk malezi ya wanafunzi
 

loosimingori

JF-Expert Member
Oct 30, 2017
922
1,000
Tuna safari ndefu..yani Maisha ya mtu muhimu kama Mwalimu amejibana na kujinyima akanunua baiskeli..Hana tofauti na Katekista..something has to be done!
something to be done is to support teachers in making these learners to be acceptable members of the society
 

loosimingori

JF-Expert Member
Oct 30, 2017
922
1,000
92% ya watanzania ni wategemezi.
Wana Jf, hao watoto wezi,watukutu,panya road, ninjas,madanga ni wanetu.wadogo zetu.Tusiwaache. Tutapata wajukuu vichwa maji
ndio mkuu ,nafikiri tatizo ni kwamba wazazi ama walezi tumeacha kuelekeza maadili mema kwa tunaowalea
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom