Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,188
- 7,490
Katika hali ya kawaida tunategemea kuwa;
Mabadiliko ya kifikra yaanzie vyuo vikuu (wasomi?)
Chimbuko la mawazo mapya yaanzie vyuo vikuu (wasomi?)
Masuala yote yanayohitaji fikra pevu ili kutatuliwa yaanzie vyuo vikuu (Wasomi!)
Mawazo, utafititi na mapendekezo (ya kitaalam) ya Suluhu za matatizo sugu yanayoikabili jamii , yatoke huko huko.
Sipingi mtu au kundi linalodai maslahi yake halali kupigania maslahi hayo; ila jambo linalonipa shida sana ni pale inapoonekana kwamba hawa wasomi wetu huchukua hatua pale tu, maslahi yao yanapoguswa. Basi hapo utasikia "Sisi wasomi wa chuo kikuu cha taifa tunasema......."!
Najiuliza kwamba ina maana "wasomi" wetu hawa, ukiacha suala la "Boom" huwa hakuna tatizo lingine la kijamii au kitaifa wanaloliona katika zama hizi na wakashinikiza lishughulikiwe (huku wakitoa ushauri wa kitaalam juu ya namna ya kulishughulikia kwa kuwa wao ni wasomi) au hata kuita vyombo vya habari na kuli address kama "Wasomi" (kama wanavyojiita wenyewe)?
Hivi mfano mtu kudai hela yake (ambayo anatakiwa apewe tu kimsingi), kunahusiana nini na usomi au kutokusoma? hivi kama hao wanaodai au kudaiwa kuwa ni wasomi hawaoni kwamba kuna masuala ya kitaifa na kijamii ya kufikiria, kuchanganua na kutoa mapendekezo au kushinikiza juu ya namna ya kutatua matatizo hayo; Tutegemee nini kipya sasa katika nchi hii? Hivi usomi huo una maana gani hasa na faida yake nini? hivi ni nani atakayeibadilisha nchi hii jamani? hivi hizi elimu huwa zinawasaidia watanzanania na taifa kweli?
Napata shida sana ninapowaza hatma ya Tanzania kama ma "Great thinkers" na wasomi wetu ndio wa dizaini hii huku tukitegemea mabadiliko na kuzaliwa kwa Tanzania mpya tunayoiota kila siku!.
Kama hii ndio aina ya wasomi wetu wa zama hizi, Kweli nawaambieni "Tanzania tunayoiota hatutaiona hadi kiama!".