Kama Hauna Connection, Pesa au siyo In Service Kuna Kozi Hautakiwi Kusoma

R7R7

New Member
Sep 3, 2020
3
45
Kuna watu tunafanya makosa kisha makosa yetu yanakua case study kwa wengine kosa langu lilikua nilipofika level ya degree nikaamua kusoma kozi moja hivi inaitwa Management of Social Development.

Wakati nafika chuo nilikuta hiyo kozi ina jina linaitwa Degree in Politics and Management of Social Development waliograduate kozi ikiwa na jina hilo walirudi chuoni kulalamika kwamba hilo jina 'Politics' linasababisha wasiajiriwe. Chuo kikaamua kuondoa jina 'Politics' na kubakiwa na 'Management of Social Development'

Baada ya muda nikiwa mwaka wa pili mwishoni ikaja kufahamika kwamba kiukweli tatizo halikua neno 'Politics' tatizo ni kwamba hii kozi haitambuliwi na 'Lawson' ( sina uhakika kama nimeandika sahihi ila ni mfumo wa mishahara na kupandisha ngazi kwa serikali) hivyo utumishi wanaona kua kumuajiri mtu aliyesomea hii kozi italeta shida kwa kutojua kiasi cha kumlipa na namna ya kupanda cheo.

Anyway, nikiwa mwaka wa tatu ikaja julikana pia kwamba hata kozi nyingine pale chuoni nayo haitambuliki na Lawson. Hii kozi ni ya uchumi ila nimesahau jina lake.

Wanafunzi wa kozi yangu na wa uchumi tukaungana na kwenda utumishi kufuatilia. Tulivyofika pale tukakutana na wanafunzi wa Mzumbe (Jina la Kozi nimesahau) na wao wana shida inafanana na yetu.

Utumishi wakasema wao hawahusiki twende Wizara ya Elimu, Wizara ya Elimu wakatoa jibu la watafuatilia. Baada ya hapo ikawa ni kurushwa huku na kule mpaka tukawa tunakaribia kuondoka chuo.

Kufikia hapo Utumishi wakawa wameweka banner kwenye ajira portal kwamba kwa yeyote aliyesoma kozi ya Management of Social Development akiingia ajira portal aiandike kama Community Development.

And then baada ya 2015 ile banner ikaondolewa, serikali ikasimama kuajiri, akachaguliwa Waziri mwingine wa elimu na bahati mbaya kila kiongozi huja na kuanza upya.

Mwaka huu niliitwa kwenye usaili DUCE nilivyofika katika kukaguliwa nikaulizwa 'Mbona cheti kina jina Management of Social Development?' hivi unajua ni aibu kiasi gani kuanza kuelezea ishu nzima?

But I did.

Mkuu wa ule usaili akaniambia "Umeidanganya system, siwezi kukuruhusu kuingia"
Nikakasirika kwakua sikua naongopa na sina sababu. Nikaondoka.

Baada ya pale sijakaa karibu na maswala hayo kwa muda leo nimelog in ajira portal nimekuta kuna posts za Administrative Officers zipo kwenye cartegory ambayo imo kozi niliyosomea.

Nikalog in nikaclick apply ikaniambia sina vigezo.

Hii kozi ingawa inasemwa haitambuliwi lakini mule darasani tulikuepo wanufaika wa mkopo, binafsi nilinufaika na mkopo. Yaani HESLB inaijua kozi inahitaji ada kiasi gani na kiasi cha stationeries ila Utumishi na Wizara ya Elimu hawaitambui.

In service niliosoma nao wamepandishwa cheo kwa kozi hii ambayo haitambuliwi. Mambo ni vururu vururu. Baba na mama wananiambia mi muongo sikumaliza chuo

Yaani kwa tulioisoma hii kozi tunabakiwa na options chache;
  • Kusoma master au Kurudi kusoma kitu kipya
  • Kuajiriwa na taasisi za serikali au taasisi binafsi (Connection)
  • Kujiajiri

Anyway, kilichotokea kimetokea. Kama naweza kumpa mtu head up kabla hajadumbukia humu acha iwe hivyo. Kama una ndugu au mdogo mpe ushauri haswa inapofika muda wa kuchagua kozi. Inawezekana 'Industrial Relation' inasound poa ila kwa hapa Tz bila connection ikawa ni tatizo.

Naattach kozi zilizofundishwa kwenye hii kozi.

View attachment 1913987

View attachment 1913988
Sema nmekuja kugundua uko na akili kubwa, kwa kuangalia tu the way unavyo respond kwny comments, big up
 

Kunguru wa Manzese

JF-Expert Member
Apr 20, 2016
7,744
2,000
Yaaah, ndo nilikuwa nampa ushukuda wangu huyo mtoa mada.. SUA wanaumiza sana, pale hakuna Kitabu na Bata ni Kitabu na misoto tu y@ masomo
Kwanzia mwaka wa kwanza hadi watatu nimepata sup kasoro semister 6 tu sikupata na ya tano angalau nilipata moja ila zote freedom square kwenye sup nilikuwa naingia na U.E kabisa sikosi masomo sita au tano


Sahivi nipo kitaa tu yote tisa bora kuteseka kitaa kuliko kuwepo Sua na kumenifanya nichukie kusoma yaani nilisema nikimaliza degree hapa ndio mwisho sisomi tena hata gazeti
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
27,799
2,000
Update:

Katika tangazo la ajira lenye post ya Afisa Maendeleo ya Jamii II post location ikiwa ni Halmashauri ya Mwanga mtu ambaye amesoma hii kozi ameweza kuapply.

Post ni 1. Na tangazo ni la 31st March 2022,

Maoni yangu:
Katika hili tangazo kuna posts ambazo mtu aliyesoma Community Development au Social Welfare anaweza omba, nafikiri hizo posts hata aliyesoma Management of Social Development anaweza kuomba lakini bado utumishi hawaruhusu.

Tangazo ni hili hapa
 

Attachments

  • 220401115506TANGAZO LA NAFASI KAZI WIZARA YA MIFUGO,WIZARA YA ARDHI & MWANGA DC.pdf
    385.6 KB · Views: 8

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
27,799
2,000
Update 5th May 2022:
Wizara ya Afya kupitia Sekretarieti ya Ajira imetangaza nafasi za kazi za 'Afisa Ustawi wa Jamii' mtu aliyesoma hii kozi ameshindwa kufanya maombi.
 

UTEKELEZAJI

Member
Oct 14, 2018
57
150
pole sana mwanangu, ungekuwa na koneksheni hata ya UVCCM ungepata kazi kiurahisi sana.
JOJO mesoma PSPA huwa hazina kazi lakini sasa hivi ni DC.
Maji marefu alifeli lasaba ila akawa mbunge.
MADELU naye hivyo hivyo, dah one day yes, kama unaishi Kawe nenda kajiandikishe kwa Gwajima anatafuta vijana wa kupeleka Barmingham Marekani kwenye exchange program.
Daa umenikumbusha wakati wa kampeni. Hii nchi ni Mungu tu........
 

platozoom

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
9,036
2,000
Hyo portal ya utumishi ina makosa mengi na ina limit watu kwenye ajira nfano ict, computer science, software engineer ni course zinazo relate why wakitaka mtu wa ict mwenye course related igome, same applies to course za science science why igome kama si ufinyu wa mawazo, mtu anaweza kuwa na experience ya hicho na course related ila wanamgomea. Mashirika makubwa mbona huita and related course ka hyo plus experience ndio advantage kubwa kuliko hyo degree.
One day nilijipinda kumu saidia rafiki yangu utumishi na amesoma mambo ya environmental studies bachelor nimefika mwisho ku submit inagoma eti mpaka awe na bachelor ya misitu.
In short utumishi wachange hyo system kaxi ka ni ya Art's waweke vigezo bachelor zote hizo.
Ni sawa unayoyasema, lakini tuwe wakweli, utumishi kwa mfumo huo sioni hata kama italeta mantiki sana kama ukibadilishwa. Kimsingi at end of the day kwa mfumo huohuo bado Mtu ataajiriwa tu. Yaani akikosa huyu kuna mwingine atapata.

Changamoto iliyopo sasa ni idadi kubwa ya Wahitimu kulinganisha na soko la ajira iwe Serikalini au sekta binafsi, hapo ndipo Serikali inatakiwa 'ikune kichwa' haswaa. Na tusiwe wabinafsi, si Wasomi tu, kuna kundi kubwa la waliokosa ajira (wale waliomaliza darasa la saba wakashindwa kuendelea au walifeli, waliomaliza kidato cha nne na kufeli, walioshindwa kumaliza elimu ya Msingi na ambao hawakukanyaga hata darasa moja).
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom