Kama hatutobadilika, maendeleo tutayasikia kwa wenzetu daima! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hatutobadilika, maendeleo tutayasikia kwa wenzetu daima!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwanamageuko, Mar 18, 2011.

 1. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  TATIZO KUBWA LA WATANZANIA NI KUTOJITAMBUA, TUNAKWENDA NA WIMBO ULIOPO NA SI UHALISIA WA MATATIZO YETU NA JINSI ZA KUYAFUMBUA! TUNAKARIRI HARAKA KILA WIMBO MPYA BILA KUTAMBUA ALA ZAKE. INASIKITISHA SANA, LAKINI HATUJACHELEWA....

  Lazima tujue nini maana ya SIASA, na lazima pia utambue nini maana ya VYAMA! Leo hii nimeamua kuviita vyama vyetu vya siasa Tanzania kuwa ni VYAMA TAKATAKA, Havina tija wala faida kwa raia wa Tanzania bali maslahi yao binafsi. Vyama ambavyo kusimama kwake kunategema kina fulani na si wanachama na mashabiki wake... vyama ambavyo vinakua na kudumaa kwa msimu kama mazao katika masika na kiangazi! VYAMA TAKATAKA ambavyo hakuna hata kimoja chenye uchungu na maisha ya Watanzania na nchi yenyewe. Mradi wakishiba wao wanatuletea maneno yasiyo na tija.. "fulani yuko vile, tukio lile liko hivi!!" hivi tutakwenda hivi mpaka lini? Siasa ni MAISHA! lakini wanasiasa wa Tanzania wanafanya kuwa SIASA NI MAIGIZO! ndio maana sishangai WABUNGE Wanashindana sasa kupeleka watu kwa "babu" si wa chama kile wala vyama hivi! maana huu ni msimu wao wa kuvuna! kwa sababu ya ADUI MARADHI watanzania wote ni WAGONJWA! kwa sababu ya adui UJINGA watanzania tumetopea kwenye lindi la UJINGA! Wameshatutoa kwenye hoja za msingi kuhusu DOWANS, JANGA LA UMEME, NJAA inayokuja, UMASKINI, MARADHI, ELIMU DUNI, sasa tuna wimbo mpya wa LOLIONDO! sijui baada ya wimbo huo ni upi utakaofuata! (tumekuwa kama wabrazil sasa! na kwa hakika tunakoelekea tutafanana nao kila kitu....

  Ndugu zangu, tatafute darubini ili tuone mbali, la si hivyo basi kizazi hiki kiangamizwe ili kianze kizazi kipya.

  Ahsanteni
   
 2. Negrodemus

  Negrodemus JF Gold Member

  #2
  Mar 18, 2011
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 2,127
  Likes Received: 101
  Trophy Points: 160
  cni wabantu na hasiri yetu ni ngoma so wimbo wowote ukipigwa tukisika ala tu lzm tucheze mabadiriko yatakuja mbelen upo. na tunajitambua vzr kbsa kama hatujitambui tusingekuwa hapaaaaaa bana
   
 3. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Mkuu, laiti kama tungelijitambuatusingelikuwa haoa tulipo... tungelikuwa zaidi ya hapa. wenzetu wakati wanawaza kuongeza elimu watz tunawaza kuongeza vimada! hebu nenda kwa wenzetu tazama barabara zao (ukiuliza huku kwetu watakwambia usitufananishe na wale kanchi kao kadogo. hapo hupaswi kuuliza mbona na rasilimali zao ni kidogo?!) Hii nchi inakera na inaudhi... hebu tazama ukienda kwa wenzetu utaona shule na vyuo kibao... hapa kwetu ni utitiri wa gest, grosary na matangazo ya kondomu kila kona! Tukitoka hapo tunasema tuna maendeleo....
   
 4. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,109
  Likes Received: 455
  Trophy Points: 180
  Mimi kwa mawazo yangu nafikiri tuna matatizo machache tu.

  1. Tunapenda ushabiki: Hivyo usipofanya kitu au kusema kitu chenye ushabiki watu hawa vutiwi kabisa. Mafano Tatizo kubwa la elimu ni kwamba hakuna mtu anayepigia kelele shule zinazofelisha. Tunajua kabisa kuna shule zinatoa division 0 kila mwaka lakini hakuna hatu mtu mmoja aliye jiuliza ni kwa nini hizi shule zinaruhusiwa kuchukua wanafunzi. Serikali vilevile ingeweza kuweka mipango na wanafunzi wanaomaliza vyuo vikuu kufundisha kwa miezi sita kabla ya kupewa vyeti kama ilivyokuwa JKT. Lakini hizi habari hazina mvuto!!. Nchi za Asia na hata hapa US elimu ni kitu ambacho watu wanaweka mbele kwasababu ya ushindani hasa uko mbele lakini sisi ni porojo tu.
  2. Ubinafsi: Rushwa ni ubinafsi
  3. Hatujui Utawala bora: Kama mimi ningekuwa raisi leo ninge ajiri consulting company na kuwa ambia wa pitie utendaji wa serikali nzima na kunishauri ni sehemu gani tuta ongeza utendaji/productivity kwa kutumia six sigma, Bechmarking methodologies na Project Mgmt methodologies na ninge iweka kwa manufaa ya nchi. Kama kuna watu au wizara zina ingiliana zingefutwa na kama kuna namna ya kuongeza ufanisi na vitu kama hivyo. Lakini watu wengi hawajui kutawala kisasa!
   
Loading...