Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,011
- 144,371
Japo ni kweli kuwa umeme unaotokana na maji huwa ni wa bei nafuu kulinganisha na umeme unaotokana na vyanzo vingine kama vile mafuta, gesi, nuclear, n.k , lakini je,si kweli kuwa mkataba wa ujenzi wa chanzo husika cha umeme unaweza kufanya bei ya umeme kuwa kubwa kuliko inavyotarajiwa?
Kwa mfano, kama mkataba una kipengele kinachosema kiasi fulani cha fedha zitazotokana na mauzo ya umeme zitatumika kumlipa mjenzi/mkandarasi wa mradi, mkataba wa aina hii hauwezi kufanya bei kuwa kubwa kuliko inavyostahili?
Au kama mradi umejengwa na mkandarasi kwa gharama zake (awe amechukua mkopo au vinginevyo) huku akijilipa kwa kutumia sehemu ya fedha za mauzo ya umeme, hapa bei ya umeme haiwezi kuwa kubwa kuliko inavyotarajiwa?
Kwasababu ya kujiuliza ni mengi na kwakuwa hatujui kilichomo katika mkataba, ni bora tu tukawa walpole kuliko kuwa washangiliaji.
Tukumbuke ya gesi ya Mtwara na hatima yake kwa Watanzania na Taifa kwa ujumla.