Kama hataki nipe mie. Kasusa? Nipe mie

Kasie

Platinum Member
Dec 29, 2013
21,168
36,056
Habari za mwanzo wa wiki, habari za Jumatatu na habari za mwisho wa mwezi...

Mie sijambo niko njema tuu sema nilikula kungu leo asubuhi bila kujua, sasa narembuajeee! Yaani macho yanafunguka robo muamala tuu daaaah!!! Halafu ndo kwanza subuhi sijui ikifika saa kumi jioni itakuwaje...!!!

Na sina mpango wa kunywa redbull hata, ukijumlisha na nilivyotupia leo (mavazi) basi tuu ila ilitakiwa niwe na extra Sunday leo.

Well turejee kwenye kichwa taja cha uzi huu, jana nilikuwa mahali kwenye eneo lenye umati wa watu wengi. Sasa nikawa nakula ubuyu wangu taratiibuu utasema sina ulimi kumbeee... (alamba alambaa aaaammmhh aaaaammmmmhhh....)

Sasa pembeni yangu upande wa kushoto alikuwa amekaa mtanashati ambaye sketi ikipita itajikuta tuu inatabasamu bila kujielewa. Tulikuwa tunakula wote huo ubuyu tangu mwanzo baadae akasema asante imetosha, nikawambia mie sijatosheka sasa ntaendeleaje kula huu ubuyu peke yangu?

Pumbeni yangu upande wa kulia alikuwa amekaa baba tuu wa makamo sio mzee sio kijana yuko katikati, huyu sikuwa nafahamiana nae hata. Yaonekana alikuwa anafatilia mazungumzo yetu ya mimi na mtanashati. Wakati nambembeleza mtanashati aendelee kula ubuyu ili tule wote huku tukizungumza ndo yule baba akaniambia ''Kama Hataki Nipe Mie....''

Usiniulize nini kiliendelea na kutokea baada ya hapo.....

1569837177296.png

Kaka mtanashati ni mfano wa huyo aliyevaa tshirt ya kijivu amevaa miwani ya jua mukono amekunja ngumi na amevaa headphones, na Kasinde ni mfano wa huyo dada aliyevaa maua kichwani.

Mtanashati hoooyeeeeeeeee........

Codes: Lemon Grass, Lemon, Chauro and Ubuyu.

1569839358379.png

Another Code: Juice ya Miwa, Juice ya Ukwaju....

Mahaba Matata ya Kasinde.
 
miss inaonekana unaweza sana......nimeliona hilo kutoka katika utangulizi wako.
content imeniacha kidogo kwani siko njema kwenye fasihi!
 
miss inaonekana unaweza sana......nimeliona hilo kutoka katika utangulizi wako.
content imeniacha kidogo kwani siko njema kwenye fasihi!

Heheheheeehehee naweza nini tena?
Umeona kitu gani kwa Kasie?

Content ni kijana mtanashati, tulikuwa tunamumunya ubuyu pamoja baada ya kitambo akasema anaenda break nikawa nambembeleza tuendelee kumumunya ubuyu, jamaa wa pembeni nae akatamani (chanzo cha kichwa cha uzi- kama hataki nipe mie..)

Hizo codes ni vibwagizo ambavyo viko kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa muamala.

Natumai nimeshakufasihi eehehehehe kama bado atakuja mwalimu wa Kiswahili hapa muda si mrefu tuwe na subira.
 
🤣🤣🤣🤣
nimeelewa sasa........nahisi una utaalamu wa kuhamasisha maana jinsi ulivyozungumzia ulaji wako wa kungu na matokeo yake ni balaa tupu!
 
🤣🤣🤣🤣
nimeelewa sasa........nahisi una utaalamu wa kuhamasisha maana jinsi ulivyozungumzia ulaji wako wa kungu na matokeo yake ni balaa tupu!

Aahahahhahahaaaa looh

Kasinde mie Mahaba yananipelekesha nimepondeka kama nyanya masalo na kulegea kama bamia....

Natamani kuendelea kusema neno kwa mtanashati ila najizuia bin kujikaza kisabuni.

K' Matata.
 
mtanashati unaitwa huku!!!🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mmmh!!!

Tumba za ubuyu mlikiwa mwatupa wapi? Si ajabu mlikuwa mwampa babu awahifadhie...
 
Babu anajua kunyonya ubuyu lakini?

Hata sijui mwenzangu, sikufanikiwa hata kumjibu. Kijana mtanashatialipoona baba anajaribu kurusha kete akabadilishana kiti na mie, hivo mie nikawa pembenina kijana mtanashati yuko katikati.
 
miee ntakulaa na mbeguu zakee Kama na huyoo mzee atachokaa nisitueee

Wuuu Koiso......

Jua tuu kuwa nimecheka sanaaaaa......

Asante kwa kunipa cheko mwanana.

Bila ajizi taarifa utapata.

Matata K.
 
Similar Discussions

6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom