Kama hana kazi asishiriki VICOBA, utalia

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,883
Na, Robert Heriel

Vikoba ni msaada mkubwa kwa watu wasioweza kuhifadhi pesa, watu wasio na msukumo wa kutafuta pesa. Vikoba humsaidia mtu kupata msukumo wa kutafuta pesa ili apate pesa ya marejesho.

Vikoba vina faida nyingi sana, lakini faida kuu ni msukumo wa kutafuta pesa iwe kwa halali au kwa haramu. Vikoba vinampa mtu uwezekano wa kupata mkopo ndani ya kikundi aliko.

Hata hivyo bado faida kuu ya Vikoba ni msukumo wa kutafuta pesa, hilo tuu ndio ninaweza kulisema.

Wanawake wengi wapo kwenye vikoba, Wapo wa vikoba vya buku buku kwa siku, wengine elfu tano kila wiki, wengine elfu hamsini kila wiki au mwezi, basi kila mtu kulingana na uwezo wake.

Vikoba ni hatari kama sumu, vikoba vinaua familia kuliko kawaida. Vikoba ni chanzo cha ndoa nyingi kusambaratika, vikoba kwa sasa ni chanzo kikubwa cha Umalaya kwa wanawake waliowengi, umalaya walioupa jina la kudanga.

Vikoba vinafanya wanaume waliooa kunyiwa uroda usiku. Vikoba vinafanya wanawake kuliwa na kujiuza hata kwa elfu tano. Sisemi kwa kukandia, naongea jambo la uhakika nililolichunguza na kulithibitisha.

Vikoba ni kitanzi kwa wanawake wetu, na mtego kwa sisi wanaume.

Vikoba vimefanya scale ya vizinga kuongezeka na kuzidi maradufu. Wanawake wamechachamaa na vikoba, hii inaongeza kasi ya misumari na mizinga ya namna zote.

Mwanamke kama hana kazi yoyote usimruhusu acheze vikoba, hata akulilie vipi usimruhusu acheze huo mchezo, akishupaza shingo piga chini akatafute wacheza vikoba wenzake huko mitaani. Usimuonee huruma asijeakakuponza baadaye. Kama hunisikii jaribu ujionee.

Mwanamke kama hana kazi na anacheza vikoba nakuhakikishia lazima atapasuliwa na wahuni wa mjini kwa bei sawa na bure, mkeo atagawa kwa mshahara wa punda ambao ni kama bure tuu.

Mkeo akicheza Vikoba akiwa hana kazi, nakuhakikishia utakonda na kuwa na unyafunzi kama sio kwashakoo kwa kukosa lishe bora. Kwani ataibana hela na kukulisha matembele na mlenda kila siku huku akisingizia hela unayompa ni ndogo kumbe pesa ingine anaipeleka kwenye vikoba bubu huko mtaani. Utakonda na kuwa na afya duni.

Mkeo akicheza vikoba na hana kazi, nakupa mwezi mmoja ataanza kukupimia penzi robo kwa robo tatu badala ya kukupa nzima nzima. Atakupaje penzi wakati anastress za marejesho, atakupa mchezo wakati anamadeni kila kikundi. Utapimiwa mpaka ukome na upumbavu wako.

Kama hana kazi asicheze vikoba, hilo sio ombi bali ni lazima. Hakuna mjadala hapo, wala hakuna mashauri katika hilo.

Mkeo hana kazi alafu anacheza vikoba, kwa nini ukirudi nyumbani usimkute amenuna na kujivimbisha mashavu kama kobra, utamkuta amenuna ukimuuliza sababu hana anachoeleza isipokuwa blah blah zisizo na maana yoyote.

Kama hana kazi na anacheza vikoba sio ajabu akakuibia pesa au akakutapeli pesa kwa kukudanganya kuwa kuna mtu anaumwa, au mtoto anahitaji pesa fulani, au uongo wowote ilimradi tuu akupige.

Hata kama anakazi yake, lazima ujue marejesho ni kiasi gani, marejesho yasije yakawa hayalingani na kipato chake, lazima atobolewe, niamini mimi hata kama unakichwa kigumu kisichoelewa,

Vikoba ni kichaka cha utakatishaji wa pesa ndani ya ndoa.
Mkeo anaweza kuwa anafanya umalaya huko pasipo wewe kujua, anadanga lake linalompa mapesa, sasa kuziingiza zile pesa ndani ya familia inakuwa mtihani kwani mume lazima utahoji, sasa mbinu rahisi ni kujiunga vikoba kisha atajifanya anahela anapokea wiki ijayo kama milioni mbili kumbe ni pesa aliyohongwa huko na madanga yake.

Vikoba viendane na kipato cha mtu.
Hana kazi asicheze vikoba.

Kiasili mwanamke ni dhaifu mbele ya pesa na mali.
90% ya wanawake duniani ni malaya wawapo mbele ya pesa.

Kama ilivyo kwa wanaume kuwa asilimia 90% ni dhaifu mbele ya wanawake wazuri.

Hana kazi Asicheze Vikoba!

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Morogoro
 
Hawa watu ni balaa,akihitaji kucheza atacheza tu hata kwa siri. Utagundua siku marejesho yakimfika shingoni ,wamekuja kubeba masofa, friji, Tv,n.k.
Na ile michezo ya upatu pia,tuwe nayo makini.

Daah yaani...

Hahahah!

Pengine mkeo hakujui na hakuogopi. Mke ukishamkataza jambo kama anakujua lazima afuate lakini kama hakujui atafanya kwa siri kwa kukupuuza
 
Huu angalau umeakisi hali za mitaani huko

Kuna mdada amepigwa mimba tatu kisa vicoba

Sent from my TECNO KA7 using JamiiForums mobile app

Huku mitaani huwezi amini ndoa za wanyonge zinapumulia mashine kisa vikoba.

Mtu hana kazi wala biashara lakini anacheza vikoba zaidi ya vikundi vitatu kwa nini asipewe mimba huyo na wahuni
 
Mtu mzima huwezi kumchunga mkuu,hata ukimpa kila kitu,akiamua kudanga atadanga tu,hata umpe kila kitu.Tumuombe Mungu atufanyie wepesi kwakweli..

Sent using Jamii Forums mobile app

Mtu anawekewa utaratibu ili asifanye upuuzi, sasa akifanya upuuzi na umempa utaratibu ni kuwa ameasi Kwa makusudi.

Ila hujampa utaratibu wowote hata akifanya uasi hatakuwa na makosa
 
Mtu anawekewa utaratibu ili asifanye upuuzi, sasa akifanya upuuzi na umempa utaratibu ni kuwa ameasi Kwa makusudi.

Ila hujampa utaratibu wowote hata akifanya uasi hatakuwa na makosa
Sasa unampa taratibu na anaasi? Utafanyanye? Utamfukuza na baada ya muda utamrudisha.na hizi ndoa zingine hizi mke anadinda ukimfukuza hatoki..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom