Elections 2010 Kama hali ndio hii, basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu

Kimewakaaaaaaaaaa!!! Hadanganyiki mtu tena. Ila bado nawashangaa watu wengine. Mtu hata nyuma ya mabati huna unaishi kijijini. Hlserikali haijawahi kukuwezesha hata kidogo JK anakuja na kundi lake la kina michuzi wapo kwenye mahelikopta wewe unapanua limdomo lako unaimba NAMBAR WAI +Eeeeeeeeeee nambARI 1 ..PUMBAFU KABISA WEWE.HAINA AKILI WEWE KABISA , WW NI SAWA NA MFU...
Read my status please!!
 
Jamani hii kitu mwanzo nilidhani ni utani. Leo nimeongea na kaka yangu aliyekwenda kata moja ya Chabutwa. Alipofika pale alikuta jamaa mmoja amebandika picha kubwa sana ya Kikwete ukutani. Kaka yangu bila wasiwasi akaanza kumwambia jamaa juu ya UFISADI wa EPA na Richmond ulivyofanyika na kuwa hela za Richmond zilimnufaisha Lowassa na EPA ndiyo zilimuingiza Ikulu.

Walienda leo, ameshangaa kukuta jamaa AMELICHANA kabisa hilo picha na kuliondoa ukutani. Analaani saana kuwa alikuwa MJINGA kwa kiasi kikubwa namna ile. ANa hasira sana na CCM nzima ingawa kwa miaka kadhaa, baba yake alikuwa Mwenyekiti wa CCM.

Bahati mbaya saana Operation Sangara haikufika Sikonge na hata Uchaguzi huu Slaa hafiki Sikonge. Kama angelifika, ingelibadili saana mawazo ya watu. Tusiwadharau watu wa Vijijini maana kama wakiambiwa na mtu vizuri, wataelewa tu kuwa USANII Tanzania ni mwingi na kuwa wameibiwa sana na wataendelea kuibiwa saaana.

Hapa kijijini kwetu kwa sasa karibu kila sehemu kuna mavitabu, makaratasi na kila aina za takataka za Kikwete, CCM na Mbunge. Ila watu taratibu wameanza kufunguka macho. Nina imani hata kama Slaa atashindwa, basi atumie muda mwingi kutembelea wanachama vijijini ambako Chadema hawajaingia na kujenga zaidi Chadema huko kwenye Mashina.

Acha watumie hela nyingi ila sisi zetu ni kampeni za Kifamilia na kijirani zaidi. Tutaelimishana hadi kieleweke.
 
Tusibweteke kabisa! na hizi wiki tano zilizobaki bado kuna kazi kubwa mbele yetu ya kukiondoa chama filisi cha mafisadi madarakani. Hivyo inabidi kuhakikisha tunafanya kampeni za nguvu sana katika kila kona ya nchi yetu na kuhakikisha tunazilinda kura zetu ili kuhakikisha hakuna wizi wowote utakaofanywa na chama filisi cha mafisadi katika zoezi la kuhesabu kura.
 
Mimi kwetu ni karatu vijijini, ikubukwe mwaka 2005, watu wengi walimchagua Slaa kuwa mbunge wao lakini kwa Urais walimchagua Kikwete. Lakini juzi juzi nilienda huko vijijini nikiwa na nia ya kuwashawishi pia wale conservatives wabadili nia.
Cha kushangaza kabla mimi sijaanza kuwaeleza habari ya umuhimu wa kuchagua chadema, wao ndio walikuwa wa kwanza kunishawishi kwanza,

Ndipo nikajua kuwa sasa basi!
 
Mwaka 2005 mzee wangu alikuwa haabiwi lolote juu ya Kikwete. Alidiriki hata kumpigia kampeni nyumbani kwetu na hata kwa majirani. Hakutaka kumsikia mtu yeyote akiongea jambo lolote baya juu ya JK. Kwa kifupi mapenzi yake kwa CCM na JK yalikuwa motomoto.

Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu nikaona si vibaya nikafunga safari kwenda kumtembelea mzee na kumsikiliza msimamo wake juu ya Kikwete na chama chake.
Kama kawaida nilijua mzee bado hapendi kusikia ubaya wowote wa CCM na hivyo ili nisimuudhi nikaona ni bora nianzishe mada kwa kumsifu Kikwete na chama chake kuwa wametekeleza ahadi nyingi walizoahidi kipindi kile. Nilianza kwa kusema 'Mzee, hivi hapa kampeni zinaendeleaje maana kule mjini ni kivumbi na jasho ila tunamwamini rais wetu Kikwete atashinda maana kutekeleza ahadi karibu zote alizotoa kipindi kile'.
Sikuamini nilichosikia kuto kwa mzee wangu. Akasema kama umekuja kwa ajili ya kumpigia kampeni Kikwete, hapa umepotea njia na inawezekana labda ulikokuwa ukienda bado haujafika hivyo tuulize ni wapi ili tukuelekeze.
Nilichanganyikiwa ikabidi niwaulize taratibu waliokuwa karibu kilichomsibu mzee na nilichoambiwa ni kwamba mzee hivi sasa hataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Kikwete na chama chake. Na kweli mzee wangu kaweza kubadilisha watu wengi tu ikiwemo na majirani zake.
Nilifurahi sana kusikia hivyo na nikamwambia kuwa nilikuwa namsanifu tu, ndipo tulipoanza kuongea lugha moja, yaani mwaka 2010 HATUDANGANYIKI

Ndio maana ninasema kama mambo yenyewe ndo hivi basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu maana kama ushindi tayari amekwisha upata.

Kadri CCM wanavyozidi kupiga kampeni, ndivyo wanazidi kuipipigia debe kambi ya upinzani. Ndio, watu wanaenda kwenye mikutano ya kampeni ya CCM - KUWAZOMEA - lakini kwenye mikutano ya upinzani WANASHANGILI!

Hivi CCM haijagundua hili? Au sasa ndio wanafanya maandalizi ya kuchakachua kura, washinde kwa kishindo?
 
Nahisi kupona ugonjwa nisioujua very soon
Post of the year to me.
Nimetamani kucheka nikaanza kulia ghafla.

Mwaka huu chama changu CCM lazima kile makapi maana kimedanganya na kufanya madudu vya kutosha.
TUKIANGUSHE kwenye KURA
 
Mwaka 2005 mzee wangu alikuwa haabiwi lolote juu ya Kikwete. Alidiriki hata kumpigia kampeni nyumbani kwetu na hata kwa majirani. Hakutaka kumsikia mtu yeyote akiongea jambo lolote baya juu ya JK. Kwa kifupi mapenzi yake kwa CCM na JK yalikuwa motomoto.

Tukiwa tunaelekea kwenye uchaguzi wa mwaka huu nikaona si vibaya nikafunga safari kwenda kumtembelea mzee na kumsikiliza msimamo wake juu ya Kikwete na chama chake.
Kama kawaida nilijua mzee bado hapendi kusikia ubaya wowote wa CCM na hivyo ili nisimuudhi nikaona ni bora nianzishe mada kwa kumsifu Kikwete na chama chake kuwa wametekeleza ahadi nyingi walizoahidi kipindi kile. Nilianza kwa kusema 'Mzee, hivi hapa kampeni zinaendeleaje maana kule mjini ni kivumbi na jasho ila tunamwamini rais wetu Kikwete atashinda maana kutekeleza ahadi karibu zote alizotoa kipindi kile'.
Sikuamini nilichosikia kuto kwa mzee wangu. Akasema kama umekuja kwa ajili ya kumpigia kampeni Kikwete, hapa umepotea njia na inawezekana labda ulikokuwa ukienda bado haujafika hivyo tuulize ni wapi ili tukuelekeze.
Nilichanganyikiwa ikabidi niwaulize taratibu waliokuwa karibu kilichomsibu mzee na nilichoambiwa ni kwamba mzee hivi sasa hataki kusikia kitu chochote kinachohusiana na Kikwete na chama chake. Na kweli mzee wangu kaweza kubadilisha watu wengi tu ikiwemo na majirani zake.
Nilifurahi sana kusikia hivyo na nikamwambia kuwa nilikuwa namsanifu tu, ndipo tulipoanza kuongea lugha moja, yaani mwaka2010 HATUDANGANYIKI

Ndio maana ninasema kama mambo yenyewe ndo hivi basi Dr. Slaa asubiri kuapishwa tu maana kama ushindi tayari amekwisha upata.

Huyo kausoma Mwongozo wa Kanisa vizuri. Teh teh teh!
 
Back
Top Bottom