Kama hali itaendelea hivi ni bora nifunge haka kabiashara | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama hali itaendelea hivi ni bora nifunge haka kabiashara

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kurunzi, Mar 1, 2011.

 1. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2011
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,003
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Nipeni mawazo wa JF wenzangu, baada ya kuona kamshara kangu hakatoshi nilifanya mpango nikazama bank na kukopa nikafungua kamradi kangu ka kuuza vinyaji ka pub, mwanzo mauzo kwa siku wastani ilifika lak 2 mpka 350 wikend kawaida laki 120 mpaka lak 2 ambayo ilisaidia kusukuma siku lakini toka hilitatizo la umeme na kupanda kwa gharama za maisha watu hawaspend na vinyaji havitoki kabisa madhalani mwezi uliyoisha mauzo ni elf 60 mpka 100000 wkend siku za kawaida 30000 mpaka elf 60. Wafanyakazi kaunta namlipa 120000 na wanje 90000 na pango 150000 bado gharama zingine nimejikuta na run in loss hata wale wana JF Wenzangu siwaoni tena kuja wamekata mguu ,nafikiria nipafunge au nipakodishe naombeni ushauri wenu.
   
Loading...