Kama hali itaendelea hivi hadi December mwaka huu basi sitakuwa na namna yingine zaidi ya kwenda kupambana mbali na hapa Tz

Uliwahi kukaa huko kabla?
Itakua ni habar za chura mkuu, chura mmoja aliwaambia wenzake kua majembe hua ni mazito sana, wenzake wakamuuliza kua ulishawahi kuyabeba hayo majembe?? Yule chura akajibu, hapana bali nilikanyagwa na watu waliokua wamebeba majembe
 
Hiyo nauli ya kwenda huko ni bora ukaigeuza mtaji hapa hapa Nyumbani, inaweza kukutoa..!!
 
Hiyo nauli ya kwenda huko ni bora ukaigeuza mtaji hapa hapa Nyumbani, inaweza kukutoa..!!
 
Mkuu Karibu sana Korea. Ni kweli earning ni kubwa na kazi zipo. Ila kwa sasa hali siyo nzuri, foreigners wanazidi kuingia na competition imekuwa kubwa mno. Mfano, kuna jamaa alimaliza masomo juzi kati,akaanza kutafuta kazi ya kupiga kwa miezi mitatu hajapata. Si kwamba kazi hazipo,zipo. Ila competition imekuwa kubwa. Kuna wageni wengi sana kutoka Vietnam, Russia , Philippines, India.....
Alafu kitu cha msingi,ambacho unapaswa kukielewa ni kubwa Wakorea ni wachache sana wanaojua English. Hivyo lugha ya mtaani,kazini na kila mahali ni Kikorea. Hivyo kufahamu kikorea unakuwa na chance kubwa ya kupata kazi na pia ku-survive vizuri.
Ila jaribu kufuata malengo yako na ndoto zako,Karibu Korea.
 
Mkuu south korea is the best. Asikuambie mtu. Mm pia nina mtazamo wa kusogea pande za hukk, soon after finishing masters. Jamaa wanahitaji sana watu wa kupiga kazi.. Ku earn 3000-6000 Usd ni kitu cha kawaida huko. Na possibility ya ku save ipo
Mkuu kazi gani professional zinazopatikana wingi huko?
 
Usitarajie kama wa Tanzania walio wengi watakutia moyo katika safari yako hii,kwan wa Tanzania ni waoga wa kutoka sehemu waliozo kulia na wengi pia wanatatizo linaitwa bongolala ....
Inawezekana wengine wametoka ila wanampa tahadhari kwasababu wanajua NJE maisha sio rahisi kama tunavyoaminishwa. Kuna mkazi wa huko amempa ushauri KUWA KOREA SIO KURAHISI KIHIVYO competition kubwa hadi kwenye kubeba box
 
Ila mentality ya kusema kwamba kwenda kupambana nchi nyingine ni kukimbia tatizo si sawa,hiyo ni namna nyingine ya kucheza mchezo.Na cha muhimu ni kwamba utapambana miaka kadhaa nje then utarudi nyumbani na capital, business ideas , exposures na mengine. Watu ambao walishawahi kuishi nje ya nchi wamekuwa chachu ya maendeleo nchini watu kama Marehemu Ruge, Mo na wengine. Hivyo unaposikia mtu anataka kutoka kwenda nje,unapaswa kufurahi na kumsapot coz atakunufaisha hata wewe.
 
Kikubwa unapokuja huku, kama una uhakika wa kupata visa...Hakikisha either unakuja na hela itakayokusaidia ku-survive kipindi unatafuta kazi au uwe na mtu ambae atakuhudumia.
Vinginevyo usiogope,fuata ndoto zako....competition hiyo ni tahadhari coz hata unapoenda vitani unapaswa kujua unaenda kupambana na nani....
 
Kwa hali hii nimejipa muda wa kuendeleza mapambano ndani ya hii nchi yangu ni mwisho December mwaka huu basi.. Baada ya hapo sitakuwa na namna zaidi ya kutafuta nafuu kwenye nchi nyingine.

Ni jambo lililo wazi kwa sasa bongo haisomeki si kwa wafanyakazi, wasomi hata wajasiliamali na ukizingatia muda unazidi kwenda.

Siwezi kufanya makosa ya kujidanganya kusubili kudra za mwenyezi Mungu ili hali mambo ni dhahir hayawezi kutengemaa kwa miaka ya hivi karibuni.

Mipango yangu ni kwenda Moja wapo ya nchi kati ya botswana au s.korea maana ndizo nchi ambazo nina access nazo kwa sasa na wenyeji huko.

Kwa anayefahamu zaidi kuhusu nchi hizo tafadhali share hapa uzoefu na unayoyajua hasa kuhusu hali ya maisha kwa ujumla huko.

Maisha ni popote, mkuu! Nikutahadharishe tu kwamba mara nyingi ng’ambo ya pili ya mto huonekana ya kijani zaidi kuliko ya upande uliopo. Kuna watu wengi wa mataifa mengine wanafanya kila wawezalo kuingia na kubaki TZ wakiamini kuna fursa nyingi za kuwawezesha kuboresha maisha yao.

Good luck!
 
Tafuta wimbo "running away" wa bob marley utajifunza kitu kipya.
We endelea kukariri minyimbo ya watu wanaoimba ili mkono uende kinywani halafu wewe ridhika na umaskini.

Mwenzio mpambanaji anatafuta maisha popote.
 
Ila wabongo hatupendani nina ndugu S.Korea Ni doc , ila hata kunialikamo huko hata holiday hajawahi ukimwambia anasema mambo hayaruhusu anyway ngoja nijibangaize hivi kwa diploma tuu siwezi kufanya kazi nchi za watu.

Nikiwa na diploma ya Animal science ya huku tz vp huko mambele inakubalika, hata nkiwa na 30 years ntapitaga hivi tuu
 
Back
Top Bottom