Yamesemwa mengi, yamefanyika mengi na yanaendelea kufanyika mengi mabaya dhidi ya haki za Zanzibar kuanzia haki za kwenye Muungano, haki za kisiasa, kiraia, kiuchuimi n.k. Watu wamekosoa na kufanya jitihada nyingi za kistaarabu kwa kufuata mifumo ya kisiasa, kidiplomasia na kidemokrasia.
Kabla ya 2015 kulifanywa jitihada nyingi kuinusuru Zanzibar kurejea kwenye mitafaruku na kikomo ilikuwa ni kuundwa kwa GNU baaDA YA KATIBA KUFANYIWA UKARABATI. Hata hivyo hali hio haikuwafurahisha wale WATESI WA ZANZIBAR na mawakala wao ambao kwa kuzingatia tu maslahi yao basi ndani ya miaka mitano mgogoro ukarudishwa kupitia ZEC na JECHA baada ya kufuta matokeo halali ya uchaguzi wa 2015.
Hii si bahati mbaya maana wote wanaohusika walijitokeza. Kwanza jamuhuri ya Muungano iliruhusu kutumika vyombo vyake kulinda wavunja taratibu na tulisikia kauli zote za vitisho zilivyotolewa. Tulishuihudia mizinga na maderaya ya JMT yakipita mitaani na tulishuhudia HAKIKISHO LA RAIS MAGUFULI kwa Dr Shein baada ya kufanyika ubatili ule wa uchaguzi wa Marudio. Hapa JMT haiwezi kukwepa Lawama na ushiriki wake kuhusu kupora HAKI YA WAZANZIBARI.
Kwa upande wa dunia kuna masuali bado. Jitihada za wazi hazijaonekana isipokuwa tulipata kauli za awali za kusema uchaguzi wa 2015 ulikuwa huru na haki na kutaka mshindi halali atangazwe (USA), Aidha Jumuiya za kikanda za kusimamia uchaguzi na zile za ndani zote zilikubali kuwa uchaguzi ulikwenda sawa. Jumuiya kama UNDP, EU, SADC, EA nk. zote zilisifu uchaguzi ule.
Baada ya kufutwa uchaguzi mzigo uliwaelemea CUF na Maalim Seif wao( Masikini mzee wa watu), kwa kuhangaika kuwatuliza wafuasi na kuanza safari ndefu yenye uchovu. Lengo ni kutaka HAKI ITENDEKE na kunusuru uvunjifu wa amani.
Ushiriki wa Jumuiya za Kimataifa za wazi umeoneshwa na Liberal International (LI) ambapo waliahidi kulibeba suala hilo na hatujuwi limeishia wapi kwa sasa baada ya suala hilo kufikishwa Umoja wa Mataifa.
MASUALI YANAENDELEA.
Hivi jumuiya ya kimataifa hawajuwi ulaghai na ushiriki wa CCM katika kuvuruga Haki ile ya 2015? na nini nafasi yao ?
Ikiwa kabla ya 2015 dunia ilishiriki kuleta utatuzi wa mgogoro wa Zanzibar hadi kuzaliwa miafaka kadhaa mpaka ulipofika wa kikatiba mwaka 2009 hivi huu wa 2015 hauwahusu na wameiwacha mkono Zanzibar na kuiwacha CCM ifanye itakavyo?
MTAZAMO.
Kwa mtazamo wangu Dunia inajuwa kinachoendelea Zanzibar, Tanzania na Afrika kwa jumla. Vipi ushiriki wao hilo ni suala lengine. Lakini ikumbukwe kwamba Tanzania ina DENI LA KIMATAIFA KUHUSU HAKI NA DEMOKRASIA ZANZIBAR KUTOKANA NA UCHAGUZI WA 2015. Kwa maana hio SULUHU haijapatikana na DUNIA vile vile ina DENI kwa Zanzibar kuhusu HAKI , DEMOKRASIA na HESHIMA. Hili la uchaguzi wa 2015 Dunia haiwezi kukwepa wajibu wake, ndio nikasema ikiwa haki haitapatikana ni Dhahiri imebariki uonevu wa CCM.
Jee dunia imebariki hilo tusubiri tufike huo mwaka 2020 tuone nini kitafuata au kabla ya hapo nini kitajiri.
Akili ya kichambuzi haikubali, LAZIMA KUNA KITU KINAENDELEA NA NAFIKIRI KADIRI MUDA UNAVYOKWENDA TUTAPATA JAWABU.
KUWEPO AU KUTOKUWEPO MGOGORO ?
Hili limekuwa ni suali linachagiza wasomi na wanasiasa. Kwa nini useme Zanzibar hakuna mgogoro au kwa sababu kuko kimya na watu hawauani? Kule kuna mgogoro mkubwa na nadhani dunia inalielewa hilo. Kama hawaelewi basi lazima wana ajenda ya SIRI NA CCM kuhusu Zanzibar. Kwani migogoro ya aina hii imetatuliwa vipi nchi nyengine zikiwemo za Afrika. Mifano hai ni kule IVORY COAST na karibuni hivi kule MALI.
Kwa mara nyengine tunataka kuona ubeberu ulivyo linapokuja suala la maslahi yake. Hili la Zanzibar ni kufeli kwa Dhana YA DEMOKRASIA Duniani na ni kufeli kwa Vyombo vya Kidunia KUSIMAMIA HAKI ZA WACHACHE.
Muda utasema
I love Tanzania, I love Zanzibar
Kishada.