Kama habari hii ya wabunge kutaka kuongezewa posho na mishahara ni kweli..

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Tamaa huondoa mantiki nzima ya watu kuishi pamoja katika taifa. Tamaa na ubinafsi ni adui wetu mkubwa katika kusimamisha taifa imara na lenye watu wenye umoja. Sisi watanzania tumechagua wabunge ili waende kusimamia maslahi yetu sio yao. ili waende kutetea kila jimbo walilotoka na kuelezea changamoto zinazotukabili kama taifa katika majimbo yao. Hatujachagua wabunge waende bungeni kutafuta utajiri na maisha ya anasa ni kinyume na utumishi wa umma. Nawaonya wabunge na serikali kuacha ulafi na ubinafsi na kuangalia maisha ya watu wa chini wa taifa hili waliowachagua ili kuleta maendeleo kwa faida ya wote. Wananchi hawatoweza kamwe kuwa watii kwa serikali isiyo tenda haki. Pale serikali inapokuwa ya kihalifu pamoja na bunge nchi nzima inakuwa hivyo. Serikali yenye tamaa na ya kibinafsi itazalisha magenge na mfarakano. Huzalisha magenge ya wauza unga, umalaya na kila aina ya uchafu na hakuna mtu atakaye kemea mwenzake kwasababu ya uovu, tutapigana wenyewe kwa wenyewe. Hatuwezi kujenga nchi katika misingi ya uchu na ufisadi khalafu tukawa salama hata kidogo. Wananchi wanapoona bunge linajiangalia lenyewe lina jijazia mali na utajiri, viongozi wao wanajijazia mali na utajiri watahamia katika uhalifu na uuza unga na magenge ya kihuni, taifa zima litakosa mwelekeo kwakuwa bunge na serikali imekosa mwelekeo.
 
''Tafakarini mambo ya msingi, juu ya ujenzi wa taifa letu na mwelekeo wetu katika nyakati hizi za hatari''
 
Back
Top Bottom