kluger
JF-Expert Member
- Jun 16, 2016
- 2,093
- 1,894
Wakuu salaam kwenu,
Naomba kuuliza kuna kero moja imeniaharibia kabisa siku yangu leo.
Mdogo wangu katumia gari yangu kwenda kanisani, bahati mbaya week mbili zilizopita niliwahi kamatwa kwa kosa la speed iliyozidi kiwango cha 50 nikiwa safarini mkoani.
Sikufanikiwa kulipa na fine hizo zimeongezeka mara dufu.
Leo wamemkamata na kumpeleka kituoni kwa kosa langu.
Nichojiuliza kama fine hizi usipolipa ndani ya siku saba zinaongezeka kwa shillings 7,500/- kwa nini umkamate mtu anapochelewa kulipa?? Maana ya hiyo elfu 7 mia 5 ni nni??
Huu ni uonevu, hawa traffic imefika mahali wanatengeneza uhasama mkubwa na raia, najua wapo viongozi wao watasoma humu, tunawafikishia tu salamu, kuweni na hekima katika kusimamia sheria na si kukomoana.
Siku njema.