Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Kuna msemo mkongwe sana usemao "kama elimu ni ghali basi jaribu ujinga". Huo ni msemo usioweza kupoteza mantiki hata kizazi cha sasa kikitoweka na kuja kingine.
Madhara ya elimu kuchezewa ni makubwa, na mara nyingi huweza kuonekana dhahiri. Kutokuwepo kwa umakini kwenye elimu huchangia katika kulifanya taifa likawa halina watu wenye kupenda ushindani maishani, watu ambao ni rahisi kudanganyika.
Viwango vya udadisi huwa ni vya chini mno, ni rahisi watu kutapeliwa, kuuziwa vitu feki visivyo na maisha marefu. Pia taifa lenye ujinga mwingi mpaka katika ngazi ya chuo kikuu huzalisha watu wenye kupenda mizaha ya mitaani wenye kuaminishwa na kuuamini dhana potofu kirahisi tu.
Kutakuwa na gharama nyingi za kuwachuja wanafunzi wasiostahili kusoma vyuo vikuu, lakini gharama hizi haziwezi kuwa kubwa kulinganisha na hasara za kuendelea kuwa na watu wasiostahili, kwenye nafasi nyeti serikalini na katika sekta binafsi.
Dunia ya viwanda ni adui mkubwa sana wa ujinga, hatuwezi kuiingia kwa kutegemea rasilimali watu wenye viwango duni. Bila ya kukuza competency ya wasomi wetu, nchi ya viwanda itabakia kuwa ni ndoto nzuri.
Kama tunadhani kwamba elimu ni ghali basi na tuujaribu ujinga. Lakini dunia halisi wala haipo tayari kutusubiri mpaka tutakapokuwa tumeshatambua kuwa ujinga ni mzigo mzito.