Kama dunia duara na inazunguka tunapataje mashariki na magharibi kwenye ramani?

kwenye suala la dunia ni duara au lah. nimeamua kutokuamini chochote mpaka sasa maana bado sijathibitisha mimi mwenyewe huku majibu ya maswali niliyonayo yakikosa majibu yenye ushahidi halisi zaidi ya nadharia,
Dunia ina umbo la tufe...
 
No suala la makubaliano ya kisayansi tu. Wataalam wametransform mduara huo kuwa kwenye plain surface. Kuna njia nyingi tu za transformation. Kama umesoma geography utaelewa.

Transformation hiyo ndiyo ilipelekea kuweka imaginary lines za latitude na longitude. Na kuweka hali iliyopelekea kupata 2D location na hatimaye 3D kwa kuweka degrees (location).

Hii yote imefanyika ili tuweze kuji-locate tulipo. Anyway hili ni somo kubwa kwenye mambo ya land survey. Nakushairi umtafute mtaalam wa land survey, Geomatic Engineer, GIS expert, Geographer, Astronant na wengine wanaofanana na hao, wakupe somo hilo na mahesabu ya Azimuthal.
 
Dunia ina umbo la tufe...
sawa but silioni hilo tufe sasa ndio maana nasema nimeamua kuwa sijui chochote mpaka nitakapopata majibu ya maswali yangu. kwa mfano nikiifikiria ikweta na hali ya hewa inayopatikana katika ukanda huo, je nchi zote zilizomo ktk ikweta zinafanana tabia ya hali ya hewa?
 
Apo chacha!
a79ce2604f68d8f861bc134efc399c2c.jpg
Ushawahi kuona Ngoma ya mduara inavyochezwa??
Kama hujui basi hua watu wanakuaga wamepanga mstari lakini unaokua kama duara hivi.
Sasa basi watu wale hucheza kwa kwenda mbele lakini sababu ni duara basi hujikuta wakizunguka hapo hapo,
Sasa swali linakuja kwako, kama watu wale hua wanazunguka hapo hapo, tunapataje mtu wa mbele na wa nyuma??
Yaani inakuaje wewe ulie kati kati kuwe na wa nyuma yako na wa mbele yako always wakati wote mnazunguka??
Ukipata jibu hapa basi fananisha na swali lako
Mduara.jpg
 
No suala la makubaliano ya kisayansi tu. Wataalam wametransform mduara huo kuwa kwenye plain surface. Kuna njia nyingi tu za transformation. Kama umesoma geography utaelewa.

Transformation hiyo ndiyo ilipelekea kuweka imaginary lines za latitude na longitude. Na kuweka hali iliyopelekea kupata 2D location na hatimaye 3D kwa kuweka degrees (location).

Hii yote imefanyika ili tuweze kuji-locate tulipo. Anyway hili ni somo kubwa kwenye mambo ya land survey. Nakushairi umtafute mtaalam wa land survey, Geomatic Engineer, GIS expert, Geographer, Astronant na wengine wanaofanana na hao, wakupe somo hilo na mahesabu ya Azimuthal.

Thank you sir. Kwa kiswahili rahisi wameamua tu wapi waite magharibi na wapi waite mashariki.
Mimi nataka wabadilishe sisi tuitwe magharibi wao waitwe mashariki.

Nakumbuka tulipoingia form three kuna darasa la mazoba lilikataa kuitwa form three D. Ikabadilishwa wao wakaitwa form three A sisi tukaitwa form three D.
 
sawa but silioni hilo tufe sasa ndio maana nasema nimeamua kuwa sijui chochote mpaka nitakapopata majibu ya maswali yangu. kwa mfano nikiifikiria ikweta na hali ya hewa inayopatikana katika ukanda huo, je nchi zote zilizomo ktk ikweta zinafanana tabia ya hali ya hewa?
Sisi ni wadogo sana ukilinganisha na uso wa tufe tunaona kama tambarare...unahitaji safari ya mbali kidogo na tufe ili uweze kuliona kama unavyotaka, wenzetu walishafanya hivyo.
Kwa hali ya hewa ya kiikweta ni kweli zinafanana ila tofauti ni ndogondogo kutokana na mabonde na milima, umbali kutoka baharini n.k
 
Thank you sir. Kwa kiswahili rahisi wameamua tu wapi waite magharibi na wapi waite mashariki.
Mimi nataka wabadilishe sisi tuitwe magharibi wao waitwe mashariki.

Nakumbuka tulipoingia form three kuna darasa la mazoba lilikataa kuitwa form three D. Ikabadilishwa wao wakaitwa form three A sisi tukaitwa form three D.
aahhaahhaa! Kituko kinafurahisha sana!
 
Apo chacha!
a79ce2604f68d8f861bc134efc399c2c.jpg
Ni rahisi sana mkuu.

Kama ilivyo Latitude ya nyuzi sifuri (au Equator) ndiyo inayotenganisha kusini na kaskazini hivyo hivyo

Longitude ya nyuzi sifuri inayopitia mji wa Greenwich, Uingereza (Greenwich Meridian) ndiyo inayotenganisha mashariki na magharibi katika ramani.

I hope hii imesaidia.
 
Thank you sir. Kwa kiswahili rahisi wameamua tu wapi waite magharibi na wapi waite mashariki.
Mimi nataka wabadilishe sisi tuitwe magharibi wao waitwe mashariki.

Nakumbuka tulipoingia form three kuna darasa la mazoba lilikataa kuitwa form three D. Ikabadilishwa wao wakaitwa form three A sisi tukaitwa form three D.
We zoba tu
 
Ni rahisi sana mkuu.

Kama ilivyo Latitude ya nyuzi sifuri (au Equator) ndiyo inayotenganisha kusini na kaskazini hivyo hivyo

Longitude ya nyuzi sifuri inayopitia mji wa Greenwich, Uingereza (Greenwich Meridian) ndiyo inayotenganisha mashariki na magharibi katika ramani.

I hope hii imesaidia.

Poa ni suala uamuzi wa kinadharia kwa jinsi walivyoigawa dunia. Ina maana ingewezekana hiyo mistari ya kufikirika Longitude kuanzia bahari ya hindi na bongo tungekuwa magharibi badala ya mashariki.
 
kwenye suala la dunia ni duara au lah. nimeamua kutokuamini chochote mpaka sasa maana bado sijathibitisha mimi mwenyewe huku majibu ya maswali niliyonayo yakikosa majibu yenye ushahidi halisi zaidi ya nadharia,

Jibu rahisi ambalo unaweza kuliona ni baharini jinsi meli inavyokuja utaanza kuiona meli yote au ile milingoti yake pekee

-kitaalamu pia ningekua na uwezo ningekualika siku moja twende field na level/theodolite tupime elevetion ya dunia kwa umbali fulani halafu tuchore ungeona curveture inavyotokea
 
Poa ni suala uamuzi wa kinadharia kwa jinsi walivyoigawa dunia. Ina maana ingewezekana hiyo mistari ya kufikirika Longitude kuanzia bahari ya hindi na bongo tungekuwa magharibi badala ya mashariki.
Kama Tanzania ingekuwa superpower kama ilivyokuwa Uingereza enzi hizo basi hii meridian ya nyuzi sifuri (Greenwich) ingepitia Dar es Salaa au Dodoma.

Kwa hiyo sisi ndio tungekuwa katikati ya dunia. Wengine wangekuwa mashariki au magharibi ya hii longitude ipitayo Tanzania.

Mfano:
Badala ya kuwa na Greenwich Mean Time (GMT), tungekuwa na Dodoma Mean Time (DMT).
 
Back
Top Bottom