Elections 2010 Kama dr slaa ni mzushi mbona hashtakiwi na usalama, rostam na lowassa?

skeleton

Member
Aug 17, 2010
60
3
Hivi karibuni usalama wa Taifa, Rostam na Lowassa waliongea na vyombo vya habari na kukanusha kuwa hawakuhusika na uchakachuaji wa kura wakati wa uchaguzi. Rostam na Lowassa wakatoa vithibitisho vinavyoonyesha walikuwa maeneo mengine katika tarehe husika.

Sasa najiuliza ni kwanini wasimshtaki mahakamani kama kweli wana ushahidi na vielelezo kuwa Dr Slaa anawasingizia?

Kama kweli hawatamshtaki mimi nitaamini kuwa ni kweli walihusika na uchakachuaji wa kura wao pamoja na watu wengine waliohusishwa na uchakachuaji huo ambao Dr Slaa na CHADEMA wameishawataja.

Na ni aibu kubwa sana kwa chombo kikubwa kama usalama wa Taifa kuhusishwa na kashfa kubwa kama hiyo na kutompeleka mahakamani mhusika. Hivyo kwa kutompeleka mahakamani ntaendelea kuamini kuwa kashfa hizo ni za ukweli na chombo hicho hakina maana kwetu wananchi, until proven otherwise!

Kina Rostam na Lowassa ni bora mngekaa kimya kwani nyie ni mafisadi papa wakubwa mliozoeleka! Moto wa milele unawasubiri!
 
Ngoja tusubiri tuone kama walochafuliwa majina yao 'masafi' watampeleka aliyewachafua mahakamani. Na Dk. Slaa alisema waende ili ukweli ujulikane. Hawachelewi kusema "tumeamua kutomshitaki ili kulinda amani ya nchi kuepusha umwagaji damu".

Tusubiri tuone
 
tushawazoea hao na kwa historia dr huwa hakurupuki katika kauli zake......elishasema haogopi kusema lolote ambalo ni ovu lenye harufu ya ufisadi
 
hakuna atakayekwenda kumshtaki, watu wataelezwa ukweli ni upi kisha watamfanya alichofanyiwa Mrema..WATA MDHARAU
 
Hawawezi kwenda mahakamani wakati ni kweli kabisa wamechakachua kwani kwani hivi nani asiyejua lowasa aliingia arusha mjini kutaka kuchakachua matokeo ya gobdless lema? Wanaarusha tulisema angechakachua tungemtoa roho, wote aliowataja dr slaa hawana moral authority kwenda mahakamani ni mafisadi wa kutupwa wanaoingamiza nchi yetu, mabepari wa kutupwa hawamuwezi clean person dr slaa.
 
Kuna sababu kubwa tatu zinazofanya Slaa asishtakiwe.

1. Madai yake ni ya kweli.

2. Madai si ya kweli ila kumshtaki kunaweza kuchafua hali ya hewa kwa watu wengi kumsapoti Dr Slaa kwa huruma.

3. Madai si ya kweli ila ukimshtaki unampandisha chati na kushusha chati ya Serikali.

All in all kutomshitaki is the best option for now.
 
Back
Top Bottom