Wakuu salaam,
Nimejaribu kutafakari mwenendo mzima wa taifa letu na matukio kadhaa ambayo yamelikumba taifa letu kufikia sasa na hasa haya ya hivi karibuni bado nabaki na maswali lukuki kichwani bila majibu.
Ukianzia mgomo wa madaktari, mgogoro wa posho za wabunge, "kufilisika kwa serikali", kupanda kwa kasi kwa gharama za maisha......., ni wazi kuwa tuna tatizo kubwa sana ambalo kiujumla tunaweza kusema ni Tatizo la Uongozi".
Kama hivyo ndivyo, na tunajua kuwa serikali iliyopo madarakani ni serikali ya ccm, hapana shaka kuwa chama hiki kimeshindwa kutuongoza na kutufikisha kwenye "Tanzania tunayoitamani".
Kama wote tunakubaliana kuwa serikali ya ccm imeshindwa kutuongoza, ni wazi kuwa tunahitaji chama/watu mbadala wa kututoa katika matatizo haya na kutupeleka kwenye mafanikio tunayoyaota.
Wengi wanaweza kusema chama hicho ni CHADEMA na kiongozi mkuu wa kuliendesha gurudumu hilo ni Mh. Dr. Wilbroad Slaa kipenzi cha Watanzania.
Changamoto inabaki kuwa:
Je kama Dr. Slaa anakuwa Rais na CHADEMA inaachiwa nchi kuanzia leo, kitu gani wanaweza kukifanya ambacho kitasaidia kutatua matatizo lukuki ya Watanzania na kuwapa matumaini mapya katika kipindi hiki kifupi hadi kufikia 2015?
Kumbuka, mabadiliko hayo ni lazima yaonekane waziwazi na wananchi kama ilivyo rahisi kuyaona matatizo sasa.