Kama DPP haondolewi ofisini mpaka afanye makosa au awe na tatizo la kiafya, Rais kamuondoa katika mazingira gani?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
Nimesoma mtandaoni kuhusu taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

F9FB4A54-644A-4B8F-B648-607C0F02C88A.jpeg



Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Rais atapaswa kuunda tribunal kumchunguza kabla ya kumuondoa.

Sasa kama haya yana ukweli, Rais Samia amemuondoa DPP ofisini kwa kigezo gani?

Kama ana makosa, kwanini asichunguzwe kama sheria inavyotaka na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
 
Samia kavunja sheria kwa kumuondoa mtu kwenye nafasi yake bila ruhusa hiyo, wasaidizi wake hawakuona hilo? au labda waliona wakapuuza kutokana na ulazima wa kuliunganisha taifa uliopo sasa, ningependa Mganga aende mahakamani kupinga kuondolewa kwake, tatizo wote ni wale wale.
 
Samia kavunja sheria kwa kumuondoa mtu kwenye nafasi yake bila ruhusa hiyo, wasaidizi wake hawakuona hilo? au labda waliona wakapuuza kutokana na ulazima wa kuliunganisha taifa uliopo sasa, ningependa Mganga aende mahakamani kupinga kuondolewa kwake, tatizo wote ni wale wale.
ana uwezo huo.wa kupinga kuondolewa
 
Samia kavunja sheria kwa kumuondoa mtu kwenye nafasi yake bila ruhusa hiyo, wasaidizi wake hawakuona hilo? au labda waliona wakapuuza kutokana na ulazima wa kuliunganisha taifa uliopo sasa, ningependa Mganga aende mahakamani kupinga kuondolewa kwake, tatizo wote ni wale wale.
Mbona feleshi Naye ilikuwa hivo tu

Sent from my Moto E (4) using JamiiForums mobile app
 
Masheria ya kipumbavu yaliyoletwa na mwendazake yafutwe yanasababishwa contradictions
Waanze kuziondoa kinga za kushtakiwa kwa Waziri Mkuu, Speaker na Naibu Speaker.

Huo ujunga wa kuwapa kinga ya kutoku shtakiwa ndio unawafanya wawe viburi na washenzi.

Isingekuwa kinga ya kushtakiwa aliopewa Job Ndugai na marehemu, angekua ameshaburuzwa mahakamani muda mrefu sana kwa kuvunja katiba ya nchi.
 
Nimesoma mtandaoni taratibu za kisheria zinazotakiwa kufuata ili kumuondoa DPP ofisini, ambapo sheria imetamka wazi kuwa DPP hapaswi kuondolewa ofisini isipokuwa tu kama ana tatizo la kiafya(illness) au amekwenda kinyume na maadili ya kazi.

Hata katika hili la kwenda kinyume na maadili ya kazi/ professional yake, Raisi atapaswa kuunda tribunal kumchunguza kabla ya kumuondoa.

Sasa kama haya yana ukweli, Raisi Samia amemuondoa DPP ofisini kwa kigezo gani?

Kama ana makosa, kwanini asichunguzwe kama sheria inavyotaka na badala yake anapewa ujaji?

Wanasheria tusaidieni kuhusu jambo hili.

Najaribu kuweka hicho kipande Chenye hizo sheria kinachozunguka mitandaoni ila bado sijafanikiwa.
Kwaiyo ni Bora angeendelea kumuacha,, kipi afadhali,kwaiyo angefuata sheria aendelee kumuacha mtu ambae hata nyinyi na sisi tunajua kwamba DPP biswalo hakuwa msafi!!?
 
Imekuwa ni desturi kwa chadema kujiona wana haki ya kukosoa tu!
Kwa muda mrefu uhuru wa habari kichwani mwa Chadema unamanisha ni kutukana na kukosoa wengine ila wao kukosolewa hapana.

Ukiwakosoa chadema watakuita ni dikteta ila wao wakikukosoa wanaita ni uhuru wa habari!!!

Kitendo cha Chadema kuanzisha kampeni ya kuunfollow Clouds kisa tu wamehoji watu wanaowakosoa siyo haki kabisa na ni unyumbu na uzwazwa wa hali juu kwenye chama hicho.

Jiulize kama Lema ambaye hana cheo chochote anaishi kwa kulelewa na wanaume wenzake huko Ulaya anaweza kuanzisha kampeni ya kipuuzi namna hiyo kisa tu dikteta Mbowe amekosolewa, vipi Lema angekuwa rais wa nchi angechukua hatua gani kwa clouds na wakosoaji wa mienendo ya Chadema?

Bila shaka chadema wanaohubiri demokrasia na uhuru wa kutoa maoni hawana chembe hata tone la uvumilivu pindi wanapokosolewa.
Huu ni uzi mpya?
Maana ni tofauti na uzi husika
 
Kimantiki hakumuondoa ila dpp atajiuzulu mwenyewe baada ya kupokea uteuzi na kuukubali,it’s game of politics.
Whatever the case, simply alionekana hafai hapo, though I doubt stance kulingana na historia ya watawala wetu kwenye kufuata sheria.
 
Amempandisha che kuwa jaji na ndio njia pekee ya haraka na rahisi kumuondoa ofisini hizi zingini ni mchakato mrefu lakini pia Biswalo huenda alisababishiwa yote hayo na mhimili mwingi na wala hakuwa yeye kama yeye, pengine ni mtu safi tu,hillo nalo mkae mkilizingatia wapo watu wengi tu kupitia awamu ya 5 wamechafuka sana ili kutimiza matakwa ya mtu.
 
Back
Top Bottom