Kama Christopher Ole Sendeka angekuwa Mwalimu... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Christopher Ole Sendeka angekuwa Mwalimu...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mbunge wa CCM, Dec 30, 2009.

 1. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Waungwana nimepata kisa hiki kwenye gazati la habari leo na nimeguswa na maoni ya mmoja wa wasomaji wa gazeti hilo. Hebu jisomee na wewe:

  Habari yenyewe
  WALIMU wawili mkoani Singida wanatuhumiwa kumbaka na kumpa ujauzito mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayesoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari ya Mtinko.

  Walimu hao katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida akiwemo wa shule ya msingi wanatarajiwa kupandishwa kizimbani leo kujibu mashitaka yanayowakabili.

  Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa na Hakimu Chiganga Tengwa wa Mahakama ya Hakimu Mkazi mjini hapa, na Mwendesha Mashitaka, atakuwa Mkaguzi wa Polisi, Nasoro Shekevi.

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Singida,Celina Kaluba,amewataja walimu hao kuwa ni Deogratius Donald (23) wa Shule ya Sekondari Mtinko na William Mwidunda (2 wa Shule ya Msingi Mtinko.

  Kamanda Kaluba amesema, ujauzito wa mwanafunzi huyo hivi sasa umefikisha umri wa miezi minne.

  Kaluba amesema,walimu hao wanatuhumiwa kumbaka mwanafunzi huyo kwa nyakati tofauti na kumpa ujauzito. Watuhumiwa hao wanaishi katika nyumba moja ya kupanga kijijini Mtinko.

  Inadaiwa kuwa Donald ndiye aliyekuwa akimfundisha masomo ya ziada (tuisheni) mwanafunzi huyo kwenye nyumba anayoishi na kwamba, mara baada ya kumaliza kumfundisha, alikuwa akimbaka msichana huyo.

  Kwa mujibu wa Sheria ya Makosa ya Kujamiana nchini, msichana yeyote mwenye umri wa chini ya miaka 18, hata kama akiridhia kufanya tendo la kujamiiana, mwanamume anayefanya naye tendo hilo anafanya kosa la kubaka.

  Habari zaidi zinadai kuwa wakati Donald akiwa kwenye majukumu mengine, alikuwa akimpa rafiki yake Mwidunda jukumu la kumfundisha mwanafunzi huyo.

  Kwa mujibu wa Kamanda Kaluba, Desemba 14, baba mzazi wa msichana huyo, Abdallah Omari, alitoa taarifa katika Kituo Kidogo cha Polisi Mtinko kuhusu mwanawe kupewa ujauzito


  Maoni ya msomaji
  Walimu siku zote nikuonewa tu! hivi nilini mwalimu yeye atapata haki hata kulindwa katika jamii? mzazi huyu alishindwa kumlipa mwalimu huyu hela yake ya tuition na baada ya kumdai sasa imekuwa kesi ya kubaka. binti huyu kapewa ujauzito na wanafunzi wenzake sasa ni walimu kulaumiwa. Watanzania umefika wakti tutambue kazi anayoifanya mwalimu katka jamii na kuiheshimu. we cannot blame teacher for evrything they do it is uncouth and very discouraging. Angekuwa afisa mwingine yeyote habari hizi yawezekana zi singetolewa kwa uzito huu.


  Tafakari
  1.
  Majuzi tulimsikia Sophia samba aisema kuwa mh. Sendeka ana kesi inayofanana nah ii lakini kahifadhiwa kwa sababu anazozijua samba na wenzie. Hivi hawa walimu wangekuwa saizi ya mh. Sendeka wangefikishwa mahakamani?

  2.
  Kuna ukweli gani kwenye maoni ya msomaji kuwa walimu kila siku ni wa kuonewa tu? Na eti wamesingiziwa baada ya mzazi kushindwa kulipia tuition?

  3.
  Hii sheria inayowamulika wanaume tu na kutosema chochote kwa upande wa msichana hata kama aliridhia kufanya ngono, inatufaa kweli? Si ubaguzi?

  Leteni maoni yenu.
  Source: http://www.habarileo.co.tz/kitaifa/?n=5025
   
 2. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #2
  Dec 30, 2009
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,068
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  Acheni uzushi mmefanya genetic test? au kuchafuana? Huyo mwalimu si adai genetic test
   
 3. Oscar Kimaro

  Oscar Kimaro Member

  #3
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ebwanaee! walimu wanaonewa kweli kwasababu;
  1.waliwahi kumfundisha na akapata ujauzito pengine ilikuwa mida iliyosogea (si kigezo)
  2.huenda kweli mzazi aalikosa ada ya tuisheni hivyo akasingizia
  3.walimu wanasingiziwa kwasababu ndio pekee wenye muelekeo mtaani kwao hivyo mzazi anataka anufaike kupitia hilo na,
  4.chuki binafsi baina ya upande wa binti na teacher
   
 4. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  DNA test is the only solution
   
 5. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,462
  Likes Received: 1,354
  Trophy Points: 280
  huku ni kumchafua mh. sendeka kwa kutumia jina lake kwenye kisa kama hiki chenye lengo la kudhalilisha
   
 6. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapana mzee, sina nia ya kumdhalilisha mh. sendeka, ila najaribu kuweka sawa hii double standard ya serikali inavyoonekana katika kisa hiki. kumbuka waziri wa utawala bora aliwahi kusema kule dodoma jambo linalofanan na hili kumhusu mh. sendeka. sasa kama mh. alihusika kweli na hakuchukuliwa hatua, je si double standard hii.

  rejea pia na hoja nilizoorodhesha kama za kutafakari.
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ishu hapa ni:

  hivi ni kweli binti wa miaka (tuseme) 17 hana utashi kuhusu ngono? sheria inatenda haki kwa kushughulikia mwanaume pekee katika jambo lililotokea kwa makubaliano?

  hao walimu wakifungwa miaka 30 au wakinyongwa, maisha ya mama na mtoto yatakuwaje?
   
 8. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kama umesoma vizuri, hakuna pale ubishi wa nani baba wa mtot! soma vizuri uelewe hoja mzee.

  hata baba halisi akijulikana kwa kutumia DNA bado wote wawili watakabiliwa mashtaka (akiwemo na yule asiye baba wa mtoto) kwa sababu naye atakuwa "kabaka" kwa mujibu wa sheria!
   
Loading...