Kama chanjo ya COVID-19 ni hiyari basi watakaochanjwa watoe hela. Hatuwezi kutumia pesa za Watanzania kufurahisha wachache

The lost

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
2,695
8,208
Huu ndiyo ukweli, kwa hii ya Msaada uliotolewa basi watakaopatiwa pia wachangie gharama ambazo zitatumika kuwalipa posho wahudumu maana pesa za wananchi haziwezi kutumiwa na wachache.

Tumeambia serikali itakoma pesa takribani 500m USD ili iweze kununua chanjo na pesa hizo zitalipwa na Watanzania wote bila kujali umechanjwa ama la.

Sasa kulingana na swala hili kuwa si la lazima na pia siyo la kitaifa (yes siyo la kitaifa maana ni hiyari) basi watakaoitumia chanjo hiyo walipie ili pesa hizo zitumike kufanya mambo mengine ya maendeleo kwa wote.

#povu ruksa.
 
Anayekataa chanjo kwa hiari ndio achangie kiasi kikubwa kuliko, anayetaka kuchannjwa,kwa asiyetaka yupo kwenye hatari ya kuugua zaidi na kuwaambukiza wengine na hivyo kuongeza uwezekano wa kuligharimu taifa pesa za walipa kodi, kwa maana ya matibabu yake nawale atakao waambukiza.
 
Anayekataa chanjo kwa hiari ndio achangie kiasi kikubwa kuliko,anayetaka kuchannjwa,kwa asiyetaka yupo kwenye hatari ya kuugua zaidi na kuwaambukiza wengine na hivyo kuongeza uwezekano wa kuligharimu taifa pesa za walipa kodi,kwa maana ya matibabu yake nawale atakao waambukiza.
Hata sijakuelewa
 
Msaada huo bwashee, mzungu kalipia kila kitu hapo. Hakika mzungu anatupenda sana zaidi anavyowapenda ndugu zake.
 
Hata sijakuelewa
Usichoelewa ni nini,hapa wapo watu wawili anayetaka kuchanjwa na mwingine hataki kuchanjwa,ni yupi Kati yao anaye taka kulipu guzia taifa mzigo?kwa hiyo yuleanaye liwekataifa kwenye hatari,achangishwe kiasi zaidi ili taifa liweze kumhudumia,pindi atakapo hitaji hudumu,mawazo haya yametokana na wazo la mchangiaji,kuwa taifa limetumia gharama kununua chanjo.
 
CCM inawadanganya sana. Chanjo tumepewa bure na beberu (Marekani). Dozi milioni 1.
Huu ndiyo ukweli, kwa hii ya Msaada uliotolewa basi watakaopatiwa pia wachangie gharama ambazo zitatumika kuwalipa posho wahudumu maana pesa za wananchi haziwezi kutumiwa na wachache.

Tumeambia serikali itakoma pesa takribani 500m USD ili iweze kununua chanjo na pesa hizo zitalipwa na Watanzania wote bila kujali umechanjwa ama la.

Sasa kulingana na swala hili kuwa si la lazima na pia siyo la kitaifa (yes siyo la kitaifa maana ni hiyari) basi watakaoitumia chanjo hiyo walipie ili pesa hizo zitumike kufanya mambo mengine ya maendeleo kwa wote.

#povu ruksa.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom