Kama chama ni chombo cha juu kuliko serikali kama anavyodai Nape, tumekwisha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama chama ni chombo cha juu kuliko serikali kama anavyodai Nape, tumekwisha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Jul 9, 2011.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Jul 9, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Kwa nini serikali inadai chenji ya rada ? Kumbe chenji inayodaiwa ni ya CCM na si taifa. Kwa nini kamati ya CCM haikutumwa Uingereza kufuatilia hizo chenji na badala yake ikatumwa kamati ya bunge ? Je ndani ya katiba yetu ni kipengele kipi kinaipa CCM hizi nguvu za kutuhumu, kushitaki, kuendesha kesi na kutoa hukumu nje ya vyombo husika ?
  Yawezekana ni kweli na ndio sababu wahalifu hawana wasiwasi wakiwa ndani ya CCM, nani atathubutu kuwachukulia hatua za kisheria ? Ndio maana vyombo vyote vya dola vinafanya kazi kwa maagizo ya viongozi wa CCM hasa jeshi la polisi, usalama wa taifa na mwaka jana likatumika hadi JWTZ. Tumeshuhudia polisi wakiwaua raia na hakuna hatua zinachukuliwa kwa sababu wanatekeleza maagizo ya vikao halali vya CCM. Kumbe tume ya uchaguzi na msajili wa vyama mahakama ni kweli vinaipendelea CCM !
  Mbona siku zote CCM inavikoromea vyama na hasa Chadema kutoa ushahidi wa ufisadi wa viongozi wa CCM kuanzia Mwenyekiti wake kama ile Orodha ya Mafisadi ya Mwebeyanga mwaka 2007 ? Je vipi wale watuhumiwa wa KAGODA, Meremeta, Kiwira, Dowans, Tangold, Richmond n.k.
  Kama nakumbuka vizuri Chenge alijiuzulu kufuatia kelele za Wananchi kwa kashfa ya kuita dola milioni moja kwenye account yake, vijisenti !
  Naona CCM imeamua sasa kuvaa ngozi yake halisi na kuonyesha kuwa mageuzi ya mwaka 1992 yalikuwa ni danganya toto tu, chama kumbe bado kimeshika hatamu. Hakuna cha katiba, hakuna cha serikali, hakuna cha watu milioni arobaini, hakuna cha vyama vingi na hakuna cha taifa, hapana, ni genge la watu milioni tano (?) tu. Na kwa Nape wamevuna walichopanda !

  By the way kuna jambo naomba mwongozo kutoka kwa wana JF, hivi kwenye kashfa ya rada aliyetoa tuhuma na kusababisha uchunguzi kufanywa ni aliyeibiwa (Tanzania) au aliyeiba (Uingereza) ? Ninavyofahamu aliyeibiwa hakuchukua hatua yoyote ile ama ya kulalamika au ya kutoa tuhuma hadi pale wasamaria wenye uchungu nchini Uingereza walipoanza kuuliza kulikoni. Wakafanya uchunguzi na ikabainika kuwa kuna uhalifu ulifanyika na baada ya hapo mpira tukapasiwa tuchukue hatua lakini tukashindwa hata hilo. Baada ya kuona jitihada zetu ni sufuri wakaamua kuridhia mapatano nje ya mahakama na hapo walafi kama kawaida yao na bila aibu wakapata mwanya wa kutaka kuvuna wasichopanda, loooo ! Tulioibiwa ni sisi, walioshtuka na kufanya uchunguzi ni wao ila sisi bila hata kuwafungulia wezi wetu kesi tumeshakaa mkao wa kula.
   
 2. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mag3 CCM imejitahidi sana kuficha makucha kwa muda mrefu lakini kupitia kwa watu ambao hawakufundwa kufunika ndipo unakuta wanaropoka kwa kutojua au kujua wanamwaga mtama, lakini kadri anavyomwaga ndivyo kuku wanavyozidi kufaidika.
   
 3. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Linalonitisha zaidi ni hatma ya taifa na watu wake kuwa mikononi mwa watu kama huyu Nape, duh hakika inatisha !
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Ndiyo maana yake Mag3,watu wanaposema zisirudishwe serikalini wanajua serikali ni chama. Hela za mabango 2015 zitatoka wapi! hata hivyo kuna swali naomba muongozo. Hii kamati ya bunge tulisikia imeshafika UK, iliteuliwa au ilipewa nguvu na kipengele kipi cha bunge.
  Kama serikali yenye vyombo vya dola haina ushahidi na integemea mtu au watu binafsi, tunasababu ya kuwa na vyombo kama polisi,PCCB na usalama wa taifa?
  Sakata lilipoanza Mkuu alisema wote walioshiriki watapelekwa mbele ya vyombo vya sheria, kauli hii inaishia wapi. UKitaka kujua mazingaombwe hakuna anayesema pesa zilitokaje, wote wanaanzia mahakama ilitoa uamuzi, na anayeendesha kampeni hii ni waziiri husika.
  Lakini ushahidi upi tena ikiwa shahidi namba moja ndiye allikuwa waziri wa mambo ya nje na sasa ni mkuu. Hii ina maana Rais wetu hakumbuki nini kilifanyika.
  ! Na hakuna anaye hoji dollar million moja na ushee akiwa kama mtumishi wa umma alizipataje na je aliziorodhesha katika mali ndani ya fomu ya maadili ya viongozi. Je yeye hawezi kuwa shahidi namba mbili iwe upande wa serikali au mashtaka?
  Yeye alikuwa mwanasheria mkuu na mh rais alikuwa waziri wa mambo ya nje.
  ! Milioni 5!!! naona unawaonea wengine Mag3, mimi ningesema genge la watu 22 wa CC

  Nakumbuka kuna waziri wetu mhe. Mramba alisema hata nyasi watu watakula,rada lazima inunuliwe. Profesa Lipumba akapiga kelele wakamuona mwendawazimu. Mama wa Kiingereza akapoteza kazi yake kutetea masikini. Serikali ikampa kazi Hosea na kila mara alisema jambo linashughulikiwa kwa ushirikianao na SFO, na hajarudi tena kutueleza ushirikiano umeishia wapi. Sasa mpira anao DCI naye anasema hana ushahidi.
  Wasichokisema ni kuwa Chenge anahusika au la, kinyemela tunaona utakaso bungeni.

  Ninawahakikishia kuwa hata kelele za kamati ya bunge kuwa wamefikia muafaka na watu washtakiwe ni kutudanganya ili watu watulie pesa zirudi halafu watuambie hakuna ushahidi. Kamati inarudi tena kukutana na serikali ya Uingereza na SFO mwezi December, mambo ni magumu bado.

  Taarifa ya rais akiwa mkutanoni ilisema muafaka na waziri wa misaada wa Uingereza umeshafikiwa. Haya yote ni kuvunja nguvu hoja za wasamaria ambazo zimesikika vema. Naomba watu waendelee kutuma email hizo pesa zisitue mikononi mwao. Ni afadhali zipotee kuliko kurejeshwa kwa udanganyifu. Tukiachia hali hii wataendelea kutufanya wajinga kama miaka 50 iliyopita.

  Wapo watakaosema uzalendo! nitashangaa kwanini tuwe na uzalendo na bilioni 70 na tukose uzlaendo na bilioni 40 za Kagoda. Nani alisema fimbo ya mbali inaua nyoka? Kama uzalendo,ni upi ulioonyeshwa kwa meremeta, harusi, Tangold n.k ambazo zenyewe tu ni zaidi ya bilioni 70.
  Nani amepanga zinunue viatabu na si kujenga wodi za wazazi wanaolala na vichanga chini kule Temeke, Mahenge na Nantumbo.
  Wapi CAG ameonyesha fungu hilo kuwa na chenji na wapi CAG alionyesha sisi kuibiwa.
   
 5. F

  FJM JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hii kauli ya Nape kuwa Chama kiko juu ya Serikali imenistua!

  Na kwa maoni yangu Nape & Co are dillusional!
   
 6. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2011
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,290
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 160
  Nimeogopa sana, mweeeee kazi kweli kweli. Nape anaweza kumwamrisha jaji mkuu ufungwe milele, mweeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee
   
 7. kinepi_nepi

  kinepi_nepi JF-Expert Member

  #7
  Jul 9, 2011
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 870
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Vijana wa CCM walishawahi kunitisha kwamba naweza kufungwa bila kesi. Hii habari ya Nape si ya kuifanyia mzaha. Ndivyo wanavyofanya. Nchi isiyo na katiba ndivyo inavyo kwenda.
   
 8. Alwatan

  Alwatan JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 409
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Mi naona mnamlaumu Nape bure kwenye hili.

  Mzizi wa haya yote ni Katiba iliyopo sasa, na Nape kimsingi hajakosea kusema chama kiko juu ya serikali.

  Katiba inasema;
  • Rais wa JMT lazima atokane na chama cha siasa
  • Spika wa bunge lazima atokane na chama cha siasa
  • Waziri mkuu pamoja na mawaziri lazima wawe wanachama wa chama cha siasa
  Hapa utaona kuwa kazi ya utungaji wa sheria na usimamizi wa sheria zote wakuu wake lazima watokane na vyama vya siasa.

  Kimsingi viongozi almost wote ukiacha wa mahakama, wanatakiwa kuwa watiifu kwa mwelekeo au sera ya vyama vyao kwanza.
  Hapa ndio ninapoona tatizo!... Na hii ni hatari zaidi hasa katika scenario ambayo mwenyekiti wa chama na rais wa nchi ni watu
  tofauti na ikatokea wamekwaruzana.

  Kwa maana hiyo hata uchaguzi mkuu ukiwa umefanyika miezi 6 tu nyuma, halafu chama cha siasa kikaamua kumtimua uanachama
  rais aliye madarakani, maana yake hakuna rais halali, na uchaguzi wa rais unarudiwa. Kwahiyo utaona tatizo sio Nape, tatizo ni katiba
  tuliyonayo.
   
 9. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 718
  Trophy Points: 280
  yule kijana ana matatizo ya akili.achananeni nae huyo!!!1
   
 10. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,187
  Trophy Points: 280
  Ni kweli kulingana na katiba ya sasa kama ilivyo, chama ndicho kinamteua mgombea Uraisi lakini anapigiwa kura na watanzania wote wenye sifa na si wananchama tu. Serikali ya Jamhuri ya Muungano anayounda Raisi baada ya kuchaguliwa inakuwa na mamlaka juu ya mambo yote ya Muungano katika Jamhuri ya Muungano na pia juu ya mambo mengine yote yahusuyo Tanzania Bara. Nape anaongea kama vile nchi haina katiba hata kama ni mbovu, hii ya wana CCM kutanguliza maslahi ya chama kuliko ya nchi ndio imetudumaza na itaendelea kutudumaza kama taifa. Tumwombe Mungu atuondolee hii kadhia inayosababishwa na CCM na watu wote wenye mawazo mgando kama Nape tuwaogope kama ukoma.
   
Loading...