Kama CHADEMA wanazidua mashina na kuweka mawe ya msingi, lini watashika dola?

Idugunde

JF-Expert Member
May 21, 2020
6,273
6,637
Chama ambacho kipo nchini na kinafanya siasa kila siku zaidi ya miaka ishirini kinaanza kuweka mawe na kuzindua mashina kina hali gani sasa!

Kinampango wa kukamata dola? Kwa staili hii watakamata dola?

Kama watakamata dola itakuwa lini? Maana kama baada ya miaka ishirini ndio wanaanza ujenzi wa ofisi na kuzindua mashia!

Kuna mwananchi anayewakubali kweli?
 
Waache wanaichungulia 2025 kwa darubini.

Na hapo anajipanga mwenyewe kugombea urais hakuna tena nafasi kwa Toto tundu.
 
Lengo la chama sio kushika dola bali ni kujipatia kula kutoka kwa wapiga kura, kwani wapiga kura wakiwapigia kura na kufanikiwa kushinda viti vingi vya upinzani hapo ndipo panapopatikana kula, maana watapata ruzuku ya kutosha tu. Ila kwa swala la kushika dola hakuna mwenye ndoto nalo maana wanajua it's impossible watanzania kuwapa nchi.
 
Ikumbukwe chama tawala kilizuia mikutano ya kisiasa kwa miaka 5 uku chenyewe kikifanya mikutano hiyo,sasa chama kingejijenga vipi? Lakini nchi inaongozwa na fedha za kodi za wananchi na sio fedha za chama, ivyo uzinduzi wa ofisi za chama hauna uhusiano wowote na kuongoza nchi.

Mwaka huu 2020 siku chache kabla ya Mwendazake kutwaliwa na mwenye dunia kuelekea motoni,alizindua ukarabati wa ofisi za CCM Lumumba. CCM inahitaji vijana wenye akili na hoja za mashiko,hoja kama hizi zinadhalilisha chama.
 
Chama ambacho kipo nchini na kinafanya siasa kila siku zaidi ya miaka ishirini kinaanza kuweka mawe na kuzindua mashina kina hali gani sasa!..
Kikubwa ni kuchangia kukuza uchumi wa Watanzania. Huwezi kukaa na kusibiri kushika dola. Yaani huwezi kusubiri miaka kumi kuletewa maendeleo eti unasubiri kushika dola kama chama wanatakiwa kuendelea kudai haki na maendeleo ya watu maana wote ni walipa kodi.
 
Chama ambacho kipo nchini na kinafanya siasa kila siku zaidi ya miaka ishirini kinaanza kuweka mawe na kuzindua mashina kina hali gani sasa!...
Una nyuzi za kipuuzi mno, najua una muda mfupi sana wa kuendelea kuwepo
 
Back
Top Bottom