Kama chadema wamesababisha haya yote bila ya dola basi wapewe nchi waogoze. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama chadema wamesababisha haya yote bila ya dola basi wapewe nchi waogoze.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngandema Bwila, May 25, 2011.

 1. N

  Ngandema Bwila JF-Expert Member

  #1
  May 25, 2011
  Joined: Sep 8, 2010
  Messages: 1,000
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Serikali ya awamu ya nne yenye vyombo vyote vya ulinzi na usalama na Amri jeshi mkuu imejivua wajibu wa kulinda maisha na mali ya wananchi wake na kuibebesha jukumu hilo CDM.

  Ni wazi sasa kuwa kila yanapotoke maafa yoyote nchini tutambiwa CDM wamewashiwishi wananchi, kama vile wananchi wamewachia CDM wafikiri kwa niaba yao.

  Inawezekanaje serikali yenye wakuu wa wilaya , mashushu, majeshi, polisi (sasa wauwaji wa raia) mawaziri ikamtupia lawama mbunge mmoja tena wa upinzani kuwa amewashawishi watu wajimbo lingine zaidi ya 800 kuvamia mgodi.

  kama mbunge mmoja wa chama pinzani toka jibo lingine ameweza kushawishi watu wakafanya uvamizi mpaka wakauwawa na polisi waliopaswa kuwalinda basi huyo mbunge na chama chake wanaushiwishi mkubwa.

  Kama wabunge wawili wa CDM toka mbali (Mmoja Toka SINGIDA) wameweza kuwashwishi familia nne tofauti wasizike ndugu zao walio uwawa, wakati kuna mbuge wajimbo hilo, kuna mkuu wa wilaya, RPC,Wapelezi, kuna mkuu wa mkuo na utili wa viongozi kibao ambao tungetegemea watu Wanyamongo wanawaelewa zaidi ya hao wa kuja kina Lisu.hapa inaashiria hatuna serikali kuanzia viji, kata, wilaya na mkoa.

  Mtu toka mbali aje kwangu awashawishi wanangu wavamie kile kiduka chetu(mimi na wanangu), wanangu wakubali kuvamia duka nami nichukue panga kuwauwa wanangu nani kichaa? Swali ni je hilo duka ni letu na wanangu? Je hawa ni watoto wangu kweli? Inawezekana ni watoto wa huyo aliyewashwishi na kama ni hivyo sinabudi nimwechie wanae!

  Hili ni la Tarime, lakini tumeambiwa CDM walliwashawishi watuwaandamene Arusha polisi wakawauwa watatu, tunambiwa CDM imeshawishi wananchi wavamie mashamba ya wawekezaji Babati.
  Swali ni kwamba hawa wananchi walio kaa mkao wa kushawishiwa na kutekekeleza kila wanacho ambiwa na CDM hatawakubali kupoteza maisha yao ni mbumbu kiasi hicho? Au kuna mambo yanafunikwa kwa jina la CDM?

  Lakini kwa upande mwingine CDM haohao wamefanya Madamano yanahudhiliwa umati mkubwa wawatu katika mikoa yote ya kanda ya ziwa na Nyanda za juu Kusini bila polisi kuingiliai. Kote huko hatujasikia mtu kakanyagwa achilia mbali kupigwa kibao. Kwa hiyo CDM wamewashawishi wananchi huko kote wasifanye fujo na wananchi wakawasikia.

  Inamaana wanachotaka CDM ndicho kinacho fanyika wala si asemacho Rais,Makumu, Waziri mkuu, Mawaziri,wakuu wa mikoa na viongozi wengine .Wamepoteza ushawishi hao.

  Sasa kwanini tusiwape CDM nchi kwa sharti moja tu ambalo naamini wanaliweza kutokana na ushawishi wao. Wawashawishi wananchi kuchapa kazi na kusimamia jasho lao kwa ghalama yoyote ile. Nchi Itaenda na sisi tutaanza kutoa misaada kwa nchi zingine badala ya kuwa matonya wa kudumu.
  Baba haombi kutambuliwa na wanae maana anajulikana na anasilikilizwa na wote waliokatika himaya yake! Kinyume chake ni matatizo makubwa!

   
 2. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #2
  May 25, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Well said. Wampe raisi wetu wa Moyoni aiongoze nchi. Hatuwataki mafisadi na watu wanaotuua.
   
 3. O

  Omr JF-Expert Member

  #3
  May 25, 2011
  Joined: Nov 18, 2008
  Messages: 1,160
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Slaa apewe nchi hii? Jamani hivi vitumbua mnavyo kula maofisini vinawekewa nini siku hizi ?
   
 4. S

  Shamwile Member

  #4
  May 25, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Well said! you have spoken the truth of what is going on in our country. If CDM has got that influence in the society, that shows they are capable running the government.
   
 5. G

  Gurtu JF-Expert Member

  #5
  May 25, 2011
  Joined: May 15, 2010
  Messages: 1,202
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kimantiki kiongozi ni yule mwenye ushawishi kwa wale anaowaongoza na wale anaowaongoza wako tayari kumfuata hata kama jambo lenyewe lipo kinyume cha sheria(lakini naamini sivyo ilivyo kwa CDM na Wananchi). Hata majambazi wanakuwa na kiongozi wao na ndiye yule mwenye ushawishi kwao na ndiye anayetoa dira ili wanaoongozwa waweze kufuata. Vivyo hivyo, chama cha siasa kinapoomba kuongoza dola kinafanya jukumu la kunadi sera zake ili wananchi wanaoongozwa wakubali kukichagua chama ambacho wanataka kiwaongoze.

  Kwa mtazamo wa sasa hapa Tanzania, viongozi wa CDM ndio wenye ushawishi kwa wananchi na ndio wanaosikilizwa na wananchi. Hivyo, hata kama tutawaita kwamba viongozi wa CDM wanawashawishi wananchi wavunje sheria(kadiri ya mawazo ya serikali ya CCM), basi wenye lengo la kuvunja sheria hizo ni wananchi wenyewe ila CDM ndiyo wanaowaongoza tu. Swali linakuja: kwanini wananchi wa TZ (katika ujumla wao) wanaasi sheria ya nchi yao? Ninasema hivyo kwasababu kwa tafsiri ya Serikali ya CCM inaonekana kuwa wananchi wa Tanzania wana mwelekeo wa kuasi sheria za nchi yao.

  Haiwezi kuingia akilini kwamba kila mara wananchi washawishiwe kuandaa maandamano na kushiriki mikutano ya CDM kwa uwingi halafu tuseme kuwa chama hicho kina malengo yasiyoendana na utashi wa wananchi.

  Kwa maana hiyo ni sahihi kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaongoza nchi hii kimabavu lakini wananchi wangependa waongozwe na Chama Cha Maendeleo na Demokrasia(CDM). Kwa hiyo suala linalobaki kwetu Watanzania ni kuwa tuliporwa vipi haki hiyo ya kuongozwa na CDM?
   
 6. f

  fikiriakwanza Member

  #6
  May 25, 2011
  Joined: May 11, 2011
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kusema CDM wamewashawishi wananchi hayo ni mawazo mfu tena dhaifu.Kila mara CDM wanatupiwa lawama ya kuwa wamewashawishi watu,kwani na nyie si mfanye ushawishi wa watu kuwakataa CDM kama wao wanavyofanya?Tena mna nguvu na Dola na mko wengi zaidi mtashindwa je na hawa wachache,tena hawana miaka 50,tena chama cha msimu,halafu watu wa kabila fulani na dini fulani tu?Mtashindwa je sasa maana nyie ni wengi,watu wa dini zote,makabila yote na mna exprience ya zaidi ya 50 years.Hayajaniingia akilini.
   
Loading...