Benny Haraba
JF-Expert Member
- Dec 7, 2012
- 8,395
- 6,361
Uchaguzi wa watu waliobeba mabegi yaliyojaa kwenye vituo vya kupigia kura kwa mara ya kwanza tumeuona awamu ya 5Haiwezekani sisi wananchi tupange foleni kwenye vituo vya kupigia kura kumchagua Tundu Lisu na Halima Mdee kwa mfano hapa Kawe halafu leo kirahisi rahisi tu Chadema wanadai hawazitaki nafasi za ubunge wa viti maalumu wala ruzuku eti wanataka haki!!
Haki gani wanayoidai hawa Chadema?
Mbona hawaendi mahakamani?
Hivi vyama vya siasa ni mali ya wananchi siyo mali ya mtu binafsi.
Sasa kama Chadema wamekataa viti maalumu wale akina Halima Mdee wanamuwakilisha nani bungeni?
Yule mbunge wa Nkasi status yake ikoje pale bungeni?
Kiukweli Chadema mnapaswa kutuomba radhi wapiga kura wa Tanzania hakuna namna.
Peoples...........Power!