Mpira wa kona
JF-Expert Member
- Nov 25, 2016
- 350
- 338
Nawashangaa sana wanachama wa CCM eti wanahoji kwanini CHADEMA inawatetea waliotumbuliwa. Inawezekana CHADEMA wana hoja pengine taratibu na sheria za kiutumishi hazikufuatwa.
Mimi nawashangaa sana hao CCM, wao ndio chanzo cha matatizo yote ya utumbuaji unaofanyika. CCM ndio imeulea kwa miaka yote uzembe wizi na kila aina ya uchafu ambao Mh. Rais Magufuli anahangaika nao. Sikutegemea kama wangethubutu kuwalaumu CHADEMA au wapinzani wanapowakosoa.
CCM ilitakiwa ikae kimya kwani umasikini na unyonge wa mtanzania umesababishwa na CCM.