Kama Chadema hamtambui JK tuone haya ... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kama Chadema hamtambui JK tuone haya ...

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mwanamayu, Nov 16, 2010.

 1. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #1
  Nov 16, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Kama ni kweli msimamo wa chama kuwa hamtambui Rais, JK basi lazima mfuate yafuatayo:
  1. Wabunge wenu wasipige kura ya kuridhia jina la waziri mkuu leo hii, watoke nje ya ukumbi wa Bunge (kuinuka kwa pamoja na kutoka nje, sio kuonekana kama hamkuingia ukumbini);

  2. JK atakapo hutubia Bunge hapo kesho na siku zijazo basi, wabunge wote wa Chadema watoke nje ya ukumbi wa Bunge (kuinuka kwa pamoja na kutoka nje, sio kuonekana kama hamkuingia ukumbini);

  3. Msiunde baraza la mawaziri kivuli; mkiunda tu baraza la mawaziri kivuli basi mjue kuwa mnashirikiana na JK;

  4. Wabunge na viongozi wa Chadema wasihudhurie sherehe zozote ambazo JK au Nuclear Scientist au Waziri Mkuu atakuwa mgeni rasmi au kuhudhuria - kama ni sherehe ya kimataifa au kitaifa;

  Otherwise mtakuwa mnatudanganya tu na kauli yenu haitakuwa na uzito!
   
 2. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2010
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii imekaa vizuri,onyesha usichokitaka wala usiparaze.
   
 3. K

  KAPONGO JF-Expert Member

  #3
  Nov 16, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,374
  Likes Received: 167
  Trophy Points: 160
  :tape:!!!????
   
 4. i

  ifolako Member

  #4
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we wajua,wao mmmmmh.
   
 5. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #5
  Nov 16, 2010
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hiyo mbinu wameitumi CUF kwa miaka 15 na sasa wako serikalini; Chadema naona wanajiandaa na serikali ya mseto mwaka 2025.
   
 6. i

  ifolako Member

  #6
  Nov 16, 2010
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nina wasiwasi wewe unaishi pamoja na Yahaya hussein!Ulijuaje kama hiyo ndiyo kanumba yao?Kweli hawa jamaa kiboko!
   
 7. Naloli

  Naloli JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2010
  Joined: Aug 26, 2010
  Messages: 416
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CHADEMA wana kazi kubwa waliotumwa na wananchi kuisimamia na kuikosoa serikali ya kidhalimu ya JK. Kutounda baraza la mawaziri kivuli ni kutowatendea haki watanzania waliowatuma BUNGENI.
  Kumbuka hayo mawazo yako ndio yaliyofanyiwa kazi kwa nguvu zote na CUF toka 1995-2005 Lakini walichovuma ni kuuwawa kwa wanachama wao uchaguzi ktk uchaguzi wa 2000 na wanachama wengine kuwa wakimbizi huko SHIMONI-MOMBASA. Kabla ya kufanyia kazi hayo mawazo yako ni lazima CHADEMA wapime kwanza je yanafaida kwa watanzania, pili je yanafaida kwa chama, tatu je hayawezi kuwa kikwazo ktk kuimarisha chama Tanzania nzima?

  Tukumbuke kuwa CHADEMA wakitekeleza mambo hayo hapo juu kuna watanzania watawaelewa na wengine hawato elewa na itaitajisomo la zaidi ya miaka mitano kuwaelewesha kwa nini chama wanachokiamini kuwaletea mabadiliko kimefanya hivyo. Pili kutekeleza ushauri wako hapo juu lengo kuu ni kuwajulisha jumuia ya kimataifa kuwa CHADEMA wameibiwa ushindi ili jamii hiyo isaidie je? msaada walio toa KENYA, ZIMBABWE ndio tunao uhitaji? (kuunda serikali ya umoja wa kitaifa) Jiulize serikali ya namna hiyo inakuza Demokrasia au inaangamiza? jibu rahisi angalia moto wa CUF unavyozimika taratibu baada ya maridhiano,pili Mugabe anavyompeleka puta Shivangirai (PM wake), angalia Rafu za kibaki kwa chama cha ODM na jinsi hasivyoheshimu maamuzi ya mawaziri wa ODM, msimamo wa RAILA ODINGA na nguvu ya umma waliyo nayo ODM ndio salama ya serikali ya ummoja wakitaifa KENYA.SWALI LA KUJIULIZA JE SERIKALI ZA UMOJA WA KITAIFA NDIO DEMOKRASIA MPYA YA AFRIKA NA NDIO SULUHU YA MATATIZO YETU?

  Hivyo kila vita inambinu zake mbinu ya Vita ya kagera ni tofauti na vita ya Afighanistan, hivyo si lazima CHADEMA watumie mbinu ambazo MWANAMAYU umezipendekeza ili waonekane wapinzani wa kweli na wamekataa kumtambua rais. Ni lazima waangalie mbinu muafaka isiyoathiri Watanzania, Chama na Wanachama na Ustawi wa CHADEMA kuelekea uchaguzi wa 2015.

  Kumbuka NCHI ZA MAGHARIBI ndio zinazonufaika na rasilimali za Tanzania hivyo hawatokuwa na ubavu wa kuisaidia CHADEMA kumng'oa JK maana ndie anawasaidia kuvuna rasilimali zetu bila vikwazo vyovyote. hivyo CHADEMA wamtambue wasimtambue kwao ni sawa tu. Maana kwao uwepo wa CCM na JK ndio faida kwao ktk kudumisha ukoloni mamboleo na unyonyaji wa rasilimali za TANZANIA. Pia nchi za Afrika viongozi wake wote sio wakubali matokeo pindi wakishindwa ndio maana AU ilishindwa kutoa kauli yeyote baada ya MUGABE na KIBAKI kuchakachua, hata wlipoambiwa MUGABE atengwe walikuwa wa kwanza kumtetea.Hivyo kumeshajengeka utamaduni wa marais wa AFRIKA kulindana na kuteteana pindi wanaposhindwa Chaguzi nchini mwao. Hivyo si AU,SADC wala ECOWAS zitakuwa na msaada kwa CHADEMA wote ni walewale.
  CHADEMA inajukumu la kufikisha ujumbe huo kwa watanzania na watanzania wauelewe na kutafuta mbinu mbadala za kukabiliana na hali hiyo mwaka 2015. Yawapasa kupigania mabadiliko ya sheria ya uchaguzi kwa kuondoa mmlaka makubwa NEC kutangaza mshindi wa urais bila kupingwa, kupatikana kwa wagombea huru ili CCM iweze kugawanyika au kupata upinzani mkubwa ndani na nje, mabadiliko ya katiba, Kuundwa kwa tume huru ya UCHAGUZI na mambo mengine mengi tu ili TANZANIA iweze kuwa na DEMOKRASIA YA KWELI na WATANZANIA waweze kufaidi Rasilimali zao.
   
 8. kijana makini

  kijana makini Member

  #8
  Nov 17, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 48
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  naunga mkono hoja..
   
Loading...