mkalamo
JF-Expert Member
- Sep 7, 2013
- 324
- 347
TAKRIBAN miezi sita sasa imepita tokea Chadema waseme hawatambui matokeo ya uchaguzi mkuu wa 2020.
Kutokana na msimamo huo ni wazi kwamba hawaamini,chama hicho hakitambui uwepo wa baraza la madiwani popote nchini,halitambui uwepo wa Bunge na wabunge waliopo bungeni na hawatambui pia uwepo wa Rais aliyepo madarakani,aliyetokana na uchaguzi wa 2020.
Msimamo huu uliwekwa hadharani na katibu mkuu wa CHADEMA, John Mnyika Novemba 25 mwaka jana aliposema kamati kuu ya chama ambayo inadhamana ya kupokea maombi, kupitia na kufanya uteuzi wa wabunge wa viti maalumu haikufanya mchakato huo, kutokana na chama hicho kutangaza hadharani kutoyambua matokeo ya uchaguzi uliomrejesha madarakani rais John magufuli na kupita kwa idadi kubwa ya wabunge kutoka chama cha mapinduzi CCM.
Pia Mwenyekiti wa chama hicho Freman Mbowe katika kukazia uamuzi huo alisema
"kilochofanyika si uchaguzi ni unyang'anyi wa demokrasia uliofanywa na ZEC (Tume ya Uchaguzi Zanzibar) na NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi) .''
Hata yalipotangazwa nafasi ya ubunge wa viti maalum chama hicho walisema hawatapeleka wabunge.
Lakini miongoni mwao waliona msimamo huo unaminya fursa ya wao kuwa viongozi na wakayatambua matokeo yote ya 2020 na hatimaye wakaenda kuapa bungeni wakiongozwa na Halima Mdee.
Baada ya uamuzi huo,chama kiliingia katika mchakato wa kuwafukuza uanachama.
Jambo la kusikitisha sasa kila kukicha viongozi hao wanataka wale waliowatimua uanachama,pia watimuliwe katika bunge wasilolitambua
Yaani iko hivi unasema wewe si mtanzania na huutambui utanzania,lakini miongoni mwa watoto wako wakasema wao ni watanzania na mzazi ukawakana kuwa si watoto wako
Wameenda kutafuta ubini kwingine napo mzazi anataka pia huko wafukuzwe.
Wanapoulizwa je unawatambua unaosema wawafukuze jibu hakuna.
Sasa basi wajibu haya
Je, madiwani na mbunge mmoja hawa nafasi yao katika msimamo huo ni upi?
2.Kwa kuwa msimamo wa chama ni kutotambua chochote kilichotokana na uchaguzi na kwa kuwa kina Mdee wamekiuka hilo, walikuwa na haki ya kuchukua hatua waliyochukua
Katika eneo hili kwanini wasipiganie bunge lote lisiwepo kwa kuwa msimamo wa chama ni kutotambua yale yote yaliyotokana na uchaguzi wa 2020 na sasa wanajielekeza kutaka watu wasio wanachama wao kutoshitiki kile wasichokitambua(Ubunge