kama CCM wasipoiangusha Chadema sasa basi watapoteza urais 2015.

Godwine

JF-Expert Member
Jan 15, 2010
1,371
281
Ni kitu cha ajabu kwa serikali ya CCM kushindwa kuiteketeza chadema inayoelekea kuchukua nchi 2015 mbali kuwa na taasisi zote za mashambulizi. kitu ninachokiona watumishi wa serikali na wanachama wengi wa CCM wameasi chama chao na kungojea tu kushuhudia kudodonga na kufa kwake 2015.

Kwa mwendo huu wa CCM ni vema wakaanzisha kitengo cha kuwafariji wazee wa toka enzi za TANU na ASP hili muda wa kuanguka utapofika wasife kwa presha au kufadhaika sana na tukio hilo kama vile wazee wa URUSI walivyofadhaika kuona sovieti ikivunjika na kusambaratika.

Hakuna kilichobaki ndani ya CCM zaidi ya kuanzisha kitengo cha kufariji makada na wanachama watiifu kwa chama pindi watapotangaziwa matokeo ya Uchaguzi 2015, la sivyo mapambano kama ya kujitoa muhanga yatajitokeza kwa makada wa zamani wenye uchungu cha chama chao.
 
Godwin kwani hali ni mbaya sana? Mi niko kijijini bado wanashabikia hicho chama twawala.
 
Ccm bado ina nguvu kubwa sana, cdm wamejikita mijini tena mikoa mitano tu kati ya mikoa 29 wewe hapo unategemea nini? Tatizo la viongozi wa cdm hawashauriki tangu tuwaambie waende vijijini hawaelewi.
 
Hata hivyo co rahisi kama unavyofikiri. Cdm wana kazi ngumu ya kufanya. Wakikaza uzi vijijini watafaniki vinginevyo wataishia kulalamika tu. Wanaweza kutumia uongozi wa wilaya kufanya uhamasishaji kila kijiji kwa kushirikiana na memba mmoja toka hq kisha kuhitimishwa na mikutano japo 3 ktk kila wilaya na viongozi wa kitaifa.
 
Mchwa wakishazaliana kwenye udongo wa volkano basi wewe tumia chuma kujenga milango na madirisha.MA....A yajue kwamba MA....D. Ni MCHWA HIVYO HAKUNA SUMU ISIPOKUWA CHUMA TU KUTEKEZA CDM.
 
Ccm bado ina nguvu kubwa sana, cdm wamejikita mijini tena mikoa mitano tu kati ya mikoa 29 wewe hapo unategemea nini? Tatizo la viongozi wa cdm hawashauriki tangu tuwaambie waende vijijini hawaelewi.

Shida ni kwamba... Wana CCM wenyewe wamekichoka chama chao! Hawakipigii kura.. Kwa hiyo kama mazingira hayo CUF inashamiri,basi wanakipigia hicho... Au kama ni CDM,wanakipigia hicho vilevile..

Niko mkoa wa Mtwara... Mbunge wa wilaya kama Tandahimba,ameingia kwa mbinde sana,fujo,FFU,mabomu ya machozi,n.k.
Nadhani kama si DC,CUF wangeiendesha H'shauri,kwani CCM imechokwa to the maximum! Mpaka na wanachama wake...
 
Chama tawala kiko njia panda. Kuna ******* na antmagamba. Kwa vyovyote mgombe urais lazima atoke kundi mojawapo, je kundi pinzani litamsapoti? Hii ni advantage kwa cdm kama wataimarisha mtandao wa kiuhamasishaji hadi ngazi ya kijiji. Ktk hili ni muhimu kutafuta uungwaji mkono toka vyama vingine kwa nafasi ya urais
 
Jamani, bila vjijini kuamka na kuitambua CDM kama ilivyo mjini, 2015 tutaambulia ubunge tu baadhi ya majimbo.
 
Hata hivyo co rahisi kama unavyofikiri. Cdm wana kazi ngumu ya kufanya. Wakikaza uzi vijijini watafaniki vinginevyo wataishia kulalamika tu. Wanaweza kutumia uongozi wa wilaya kufanya uhamasishaji kila kijiji kwa kushirikiana na memba mmoja toka hq kisha kuhitimishwa na mikutano japo 3 ktk kila wilaya na viongozi wa kitaifa.

maisha magumu ndiyo rungu pekee la kuiangusha ccm.
Na ndiyo rungu limpalo ulahisi cdm kupata wafuasi wengi.
Hata huko vijijini wengi hata kabla ya cdm hawajafika kupiga kampen wananchi washa kuwa upande wao.
 
Godwin kwani hali ni mbaya sana? Mi niko kijijini bado wanashabikia hicho chama twawala.[/QUOTT

Tazama chaguzi ndogo zinazofanyika vijijini utapata picha, kama CCM inasumbuliwa mpaka chaguzi za serikali za vijiji ujue mambo si sawa. zamani tulikuwa tukiona chadema wanaishia ubunge kwenda juu. lakini sasa naona wanashuka mpaka serikali za vijiji , na kama mambo yataenda kwa kasi hii basi kifo cha CCM 2015 kitalete simanzi kwa makada watiifu wa chama hiki
 
karibu kunapambazuka!
 
We endelea kulala tu hujui upepo unaelekea wapi au? Au unajua lakini inakuwa ngumu kwako kusema!!!
 
Maisha magumu+mfumuko wa bei + bei ya mafuta ya taa= ???
Wenye maumivu makali wanajua wapi pa kwenda kuponea.
 
wengi tunapenda upinzani lakini kwa sasa wapinzani bado ni wachanga vyama vyama ni vya kikanda.
 
mimi sijui mfumo mzima wa chadema unafanyaje kazi'ninaamini kama kweli chadema wanataka kuchukua 2015 wanaweza kuwatumia watanzania kujiimarisha vijijini na baadhi ya mikoa ambayo wanaona ni migumu kwao'wasipotumia hela kuelimisha na kutengeneza ajira za muda kwa watanzania wenye nia na mabadiliko kwenda kuelimisha vijijini itakuwa ni ngumu sana kuchukua nchi bana''
 
wengi tunapenda upinzani lakini kwa sasa wapinzani bado ni wachanga vyama vyama ni vya kikanda.

ID yako na unachoandika vinaonyesha hujitambui.

Hivi hukujua hizo kanda ni sehemu ya tanzania?
Ktk urais wako hukujua harakati za uhuru zinahusishwa na wakazi wa Tabora na Pwani zaidi, je huoni uhuru uliletwa kikanda?
 
Back
Top Bottom