Kama ccm wanalalamikia mafisadi nani amewachukulie hatua ?

fige

JF-Expert Member
Jul 4, 2010
376
61
Kuna wakati najiuliza hivi chama chetu kinachoongoza kimechanganyikiwa ?

Wajibu wa kukamata na kuwashitaki watu wote wanaovunja sheria ni wa serikali,inatia huzuni pale ambapo anayetakiwa kukamata mkwepa kodi,mwizi,fisadi anapokuja kututangazia kwamba fulani ni mwizi kama mimi(ccm).

Hakika kwa kufanya hivyo ni kukiri kushindwa kutimiza wajibu wake .

Mwaka huu nimeona maajabu ya siasa hapa Nchini kwa kauli tata za viongozi wa juu wa serikali na chama tawala,leo anasema hivi kesho anageuka anasema kinyume.hivi huko nikuchanganyikiwa au ndio uwezo mdogo wa kufikiri ?

Kama kuna fisadi ndani au nje ya chama chenu wajibu wa kuwashitaki ni wenu na serikali yenu,kututangazia bila kuchukua ni udhaifu mkubwa kuliko kuwajua na kutowatangaza bila hatua.
 
Naomba kufanya marekebisho ya hiyo heading ninaomba isomeke,
'Kama ccm wanalalamikia mafisadi,nani awachukulie hatua'

Naomba kuwasilisha
 
Hii ni sawa na baba kulalama kukosekana chakula mezani wakati hakuacha mshiko
 
Naomba kufanya marekebisho ya hiyo heading ninaomba isomeke,
'Kama ccm wanalalamikia mafisadi,nani awachukulie hatua'

Naomba kuwasilisha
Wa-PM Mods wakurekebishie!

By z Way, ccm wanachofanya ni kuangalia upepo na kufanya mnaigizo Tom &Jerry!!
Wameona kuwa wananchi wameshaielewa hoja ya Ufisadi kutokana na mahubiri ya cdm, wakaamua kuwa nao watumie hiyohiyo bila kutathmini na kugundua kuwa inawagusa wao direct na kuwafanya vikatuni majukwani!
 
Kama kuna fisadi ndani au nje ya chama chenu wajibu wa kuwashitaki ni wenu na serikali yenu,kututangazia bila kuchukua ni udhaifu mkubwa kuliko kuwajua na kutowatangaza bila hatua.

Kwa hali ilivyo sasa Watanzania wengi ni MAFISADI kwa kuwa vipato vyao halali haviendani na matumizi yao na mali walizo nazo! Haijalishi ni wananchama wa vyama vya siasa au wasio kuwa na vyama. Mbali na tuhuma dhidi ya viongozi wa Chama tawala hata wale viongozi wa vyama vya siasa wakichunguzwa utakuta nao wako katika mkumbo huo huo wa kuwa na mali na matumizi ambayo hayatokani na vipato halali. Sijui ni panya gani atamfunga paka kengele manake hata wale waliopewa jukumu la kuwashitaka watu wenye makosa ya ufisadi nao ni Mafisadi vile vile!!
 
Asante kwa kuchangia Mkuu,

Kuna tabia moja ya wenyeji wa sumbawanga ni ya ajabu sana.

Watu wa sumbawanga ni wakulima wazuri sana ,wakishavuna mazao yao huhifadhi kwenye vihenge nje ya nyumba.
Tatizo la ndugu zangu wale wanapenda sana pombe.

Kinachotokea baada ya mavuno kila mwanafamilia huanza kuiba yale mazao na kuyauza na mara nyingi baba huanza kuiba.Na kwa vile kila mtu hushiriki kuiba no matter ameiba kiasi gani kunakuwa hakuna mtu wa kukemea /kuhoji/kulalamika juu ya wizi huo.

Matokeo yake ni kwamba pamoja na kuwa wanavuna vizuri lakini;-
1.kila mwaka wana njaa
2.watoto wengi hawasomeshwi

Vipi watz tuendelee na utamaduni kama wa wenzetu hawa ?
 
Back
Top Bottom