Elections 2010 Kama CCM itamsimamisha JK

Jan 16, 2007
721
176
Kama ccm itamsimamisha jk basi wabunge wa ccm wachaguliwe kutoka hospital ya vichaa milembe watanzania tuamke mungu ibariki tanzania
 
Kama ccm itamsimamisha jk basi wabunge wa ccm wachaguliwe kutoka hospital ya vichaa milembe watanzania tuamke mungu ibariki tanzania
Mkubwa maneno makali sana hayo.
Ila kimsingi ameboa hivyo hukumu ya haki ni hapo october, vinginevyo watanzania tutakuwa na ujuha wa namna fulani hivi!!
 
Nitashangazwa sana kama hakutakuwa na mabadiliko,kuna baadhi ya mikoa wananchi wengi ni wajinga!Wakirudia makosa tujitenge wataingiza akili,kwasababu utaratibu wa sasa wa kupeleka mapato yote makao makuu na huku tukiambiwa ni masikini uishe,hao wanaokubalina na viongozi kuwa sisi ni masikini na wakati si wananchi wote wametokea maeneo enye umasikini ni ujinga inaotakiwa kwisha,wananci wanaotoka maeneo yasiyokuwa na uzalishaji ama mchango kwa taifa wawasikilize wale wasioitaka ccm na wenye rasilimali,la sivyo wabaki na ccm na maeneno yao,mfano huko Tabora na Singida wanatia hasira sana,masikini lakini wao na ccm tu kwasababu ya chuki,pambafu sana!
 
Kama ccm itamsimamisha jk basi wabunge wa ccm wachaguliwe kutoka hospital ya vichaa milembe watanzania tuamke mungu ibariki tanzania
Advocate Jasha, CCM kumsimamisha JK sio suiala la kama, ni uhakika bila shaka na Watanzania kwa umoja wetu tutawachagua tena na kutoka na ushindi wa kishindo!. Naomba usibishe. Subiiri November utashuhudia kwa macho na masikio yako.
 
Pasco, umezungumzia ukweli unaouma. Inasikitisha kuwa hata baada ya karibu nusu karne baada ya kujitawala, bado tunadanganywa na kuwa miaka mitano ijayo tutafika nchi ya ahadi, ambayo maziwa yatatoka kwenye mabomba, na kwa imani hiyo kura zetu zinatumika kuwapa KULA.
 
Kwanza nataka kuwaweka sawa kuwa uchaguzi mkuu utafanyika mwezi February,2011 ukitaka bisha hadi uzimie,habari ndio hiyo.Pili wananchi ndio wenye mamlaka ya kuwaweka madarakani viongozi wazuri au wabaya,katika hao wananchi na sisi wa JF tumo humo hakuna cha kukwepa,kilichobaki tujiachie wenyewe tufanye tunachoona kizuri wakati wa uchaguzi na kamwe tusianze kuwa upande wa vyama ambavyo hata bendera zao tuu zinawashinda kukarabati!
Mungu ibariki Tanzania yetu
 
Please do not insult inteligensi ya watu, ni dalili ya kuwa na upungufu wa akili kama unakimbilia mitusi na kushutumu watu. Vyama vina misimamo yao na ni hiyo misimamo ama inawavua madaraka au inawaingiza kutokana na jinsi hali inavyoruhusu na mahitaji ya watu wakati huo. Kama muda bado CCM itarejea madarakani; kama muda tayari CCM italazimika kuungana na vyama vingine kutengeneza serikali lakini si kutukana watu; ni upuuzi kushabikia matusi badala ya kuwavutia watu wakakuelewa nini unahitaji ,wapo watu wanachukizwa sana na matusi na kukufanya uwakimbize soma siasa ili ujuwe utaratibu wa siasa na kutambua mantiki ya watu kutaka kutawala wengine na wengine kuishia kunawa kula wasile na kama mimi ninayetaka mtawala awe mkweli si mbabaishaji wa matusi na kuniongea hasira.:target:
 
Mkubwa maneno makali sana hayo.
Ila kimsingi ameboa hivyo hukumu ya haki ni hapo october, vinginevyo watanzania tutakuwa na ujuha wa namna fulani hivi!!
Mkuu
ni kweli umetoa maneno mazuri sana, kwamba hukumu yao ni hiyo octobar
lakini bahati mbaya sana humuku hiyo i mikononi mwa watanzania wenye njaa, na ukosefu wa ufahamu na
kujitambua kwetu ni kugumu, hasa kwa kuwa ni wepesi wa kusahau maumivu na vituko vya hawa viongozi wetu
 
Please do not insult inteligensi ya watu, ni dalili ya kuwa na upungufu wa akili kama unakimbilia mitusi na kushutumu watu. Vyama vina misimamo yao na ni hiyo misimamo ama inawavua madaraka au inawaingiza kutokana na jinsi hali inavyoruhusu na mahitaji ya watu wakati huo. Kama muda bado CCM itarejea madarakani; kama muda tayari CCM italazimika kuungana na vyama vingine kutengeneza serikali lakini si kutukana watu; ni upuuzi kushabikia matusi badala ya kuwavutia watu wakakuelewa nini unahitaji ,wapo watu wanachukizwa sana na matusi na kukufanya uwakimbize soma siasa ili ujuwe utaratibu wa siasa na kutambua mantiki ya watu kutaka kutawala wengine na wengine kuishia kunawa kula wasile na kama mimi ninayetaka mtawala awe mkweli si mbabaishaji wa matusi na kuniongea hasira.:target:
Mzee wa Lukwangule, hawa ndiyo type ya vijana wetu wa kisasa hapa JF, daily na weekly top posters, ndio hawa wako kileleni. Faraja moja ni kuwa 'ivumayo haidumu' na ngoma ikilia sana, mwishowe hupasuka, baathi yetu humu JF ni ngoma ivumayo sana!, usijisumbue trying to put sense into an empty bin!, sio debe tupu, debe tupu angalau hupiga kelele, hili ni debe wazi liko open both sides hivyo upepo una go thrugh na halipigi kelele.
 
Nitashangazwa sana kama hakutakuwa na mabadiliko,kuna baadhi ya mikoa wananchi wengi ni wajinga!Wakirudia makosa tujitenge wataingiza akili,kwasababu utaratibu wa sasa wa kupeleka mapato yote makao makuu na huku tukiambiwa ni masikini uishe,hao wanaokubalina na viongozi kuwa sisi ni masikini na wakati si wananchi wote wametokea maeneo enye umasikini ni ujinga inaotakiwa kwisha,wananci wanaotoka maeneo yasiyokuwa na uzalishaji ama mchango kwa taifa wawasikilize wale wasioitaka ccm na wenye rasilimali,la sivyo wabaki na ccm na maeneno yao,mfano huko Tabora na Singida wanatia hasira sana,masikini lakini wao na ccm tu kwasababu ya chuki,pambafu sana!

kijana umenena, But watch your tongue! Ningefurahi sana mkoa wa pwani hasa chalinze na bagamoyo wakianza. maana it haina mchango wo wote according to your analysis japo unaonekana kuwa na chuki na Tabora. au ni issue za tucta nini mkuu. Maana waziri wa kazi antoka huko. tehe tehe teheheheh
 
kijana umenena, but watch your tongue! Ningefurahi sana mkoa wa pwani hasa chalinze na bagamoyo wakianza. Maana it haina mchango wo wote according to your analysis japo unaonekana kuwa na chuki na tabora. Au ni issue za tucta nini mkuu. Maana waziri wa kazi antoka huko. Tehe tehe teheheheh

ni kweli isiyopimika, chuki hazifai ndani ya jf, kwa taarifa singida hulijaza soko la tanzania kila siku kwa vitunguu,mafuta safi ya alzeti,mifugo mingi sana-kuku,ngo'mbe na mbuzi ,pia hulima mahindi kwa kiasi ambacho ingefaa kuingizwa the big four, halikadhalika tabora ni mashuhuri kwa tumbaku,asali na mifugo.
1. Na kwa sababu hizo wananchi wamepumbaa, kinachotakiwa kuelimishwa tu wakuu.
2. Wakuu watawala wetu wanahakikisha jamii haipati ufahamu wa haki za kikatiba ili wao waendelee kufyonza.
3.historia inaonyesha wazi kuwa upo muda jamii huamuka na kudai haki.
4.historia pia huonyesha mahali ambapo kura zimeshindwa kuleta ufumbuzi wa matarajio ya kundi kubwa ktk jamii ( class ) basi jamii hujitwalia utawala kwa nguvu (tunao mfano mzuri sana wa zanzibar.)
 
Lukungwale maoni yako ni sawa ila. Mambo mengine yanaleta hasira sana. Japo sishabikii uwakilishaji wa hoja wa ndugu Jasha!
Ila Nina wasiwasi kama watanzania kweli tunataka mabadiliko Maana uchangiaji wa baadhi ya wadai ni wamashakamashaka!
 
CCM itamsimamisha lakini wananchi ndiyo watakaomua kumchagua au la suali linakuja jee wananchi wakimchagua una maana ni vichaa wandawazimu??????
 
yani wananchi atuna kura ya kuingoa ccm madarakani mana usiipigie ccm kura yako yenyewe itashinda tu sijui ina mapepo na majini yanakuja kuipigia kura yani inabidi kufunga na kuomba sana ilikuingoa madarakani bila kumwaga damu kwani hawajamaa wanambinu zote za ushindi yani atawakinisimamisha mimi nitashinda
 
Back
Top Bottom