Kama CCM inataka kushinda uchaguzi kabla ya kupiga kura, Magufuli ndiyo mtu sahihi

Hizi sio porojo Lizaboni huu ndio ukweli, Mafisadi yatakiteketeza chama chenu na atakaye kiua ni Lowasa endapo hatapita believe me mamvi kajipanga. Kwa sasa hivi nyinyi ccm sio wamoja tena kama tulivyozoea siku zote kila mgombea anatoa kashfa za mwenzie badala ya kujikita kwenye hoja ya uraisi. Narudia kusema tena Makufuri hatakuja kuwa raisi katika maisha yake

Unless wewe ni 'little puppy' umezaliwa juzi hujui nini kinaendelea kwenye siasa za nchi hii...haikuwahi kutokea kwenye historia (toka mwanzo wa vyama vingi) kukawa na chaguzi bila makundi. Lowassa atachinjiwa baharini (kama alivyofanywa kwenye uwaziri mkuu) na hawezi kufanya lolote.
 
Last edited by a moderator:
Unless wewe ni 'little puppy' umezaliwa juzi hujui nini kinaendelea kwenye siasa za nchi hii...haikuwahi kutokea kwenye historia (toka mwanzo wa vyama vingi) kukawa na chaguzi bila makundi. Lowassa atachinjiwa baharini (kama alivyofanywa kwenye uwaziri mkuu) na hawezi kufanya lolote.
Hapo pa kuchinjiwa baharini ndipo tunapaombea wapenda amani
 
Shwari wakuu,

Siku zote huwa naamini kuwa nchi hii ilipofika inahitaji kiongozi mkali anayeweza kusimamia sharia kwa nguvu zote. Anatakiwa awe dikteta (na awe kiongozi wa kijeshi) mwenye moyo wa kuijenga nchi, ambaye anaweza kutumia sheria zilizopo (sheria zetu ni nzuri tu), kubadilisha mind set za watanzania waache kufikiri kuwa lazima tuishi kwa ku-piga deal (kuiibia serikali) ambako kimsingi ni kujiibia wenyewe. Sasa kwa mazingira haya tuliyonayo hatuwezi kupata kiongozi huyo kwa sababu ya stori za demokrasia na upuuzi mwingine ambao ndio umetufikisha hapa.

Mara zote nimekuwa muumini mzuri wa sera za Hayati baba wa Taifa, na ninajaribu kuziishi kwa kadri ninavyoweza. Lakini nimegundua kwamba, kusipopatikana kiongozi wa nama niliyoielezea hapo juu, basi hakuna sababu ya kuendelea kuwa na fikra (sera?) ambazo watu hawataki kuzifuata tena.

Sasa basi, kwa mtazamo wangu, kiongozi anayeweza kupatikana kidemokrasia (f.u.c.k democracy!) ambaye anafanana kidogo na kiongozi ninayemtaka ni JOHN POMBE MAGUFULI. Sijawahi kuelewa siasa za Tanzania kwa sababu pamoja na mapungufu yote, huyo jamaa angepewa uwaziri mkuu tungeweza kusonga mbele kidogo kwa sababu ni mkali na anaweza kusimamia vitu anavyoviamini. Eti wao wakaweka pale Lowassa. Aliposhindwa wakaweka Pinda!!!! Seriously??!!!! What do they have in common??? Yaani kuna sifa zipi alizonazo Lowassa ambazo zilimfanya ateuliwe PM ambazo hizo pia ndio zilifanya ateuliwe Pinda baada ya Richard wa Monduli kujiuzulu???

Ok Turudi kwenye mada. Ninachotaka kusema ni hivi, naona kama huko kwenye urais Magufuli haonekani onekani hivi! Na anaweza asipite huko kwenye kupitisha mgombea. Na ndani ya CCM ni yeye tu mwenye unafuu kiuongozi. (Upinzani kuna jembe Wilbroad ambaye pia anaweza asipate huo urais) Asipopita Magufuli manake nchi itaendelea na sera za chukua chako mapema kama ilivyokuwa miaka yote 30 iliyopita. Na mimi sasa ntaweka Unyerere pembeni nashiriki deal zote zenye mianya ya ufisadi ambazo mwanzo nilikuwa nazikataa!!! Huyu jamaa (Pombe)namjua kwa sababu nilikuwa naishi nyumba moja na binti yake na namfahamu pia mtu wake mmoja wa karibu na nimefuatilia utendaji wake kwa miaka mingi (ana mapungufu yake pia.

Nadhani watanzania sasa tuanze kuweka watu serious kwenye nafasi kubwa, tusipeane kama zawadi bana, mtu unapewaje ukuu wa mkoa kama asante???? Halafu tunategemea performance? CCM achene ujinga bana, mshaimaliza kabisa hii nchi wekeni mtu ambaye anaweza irudisha kwenye msatari kidogo, ah!

Wekeni Magufuli hapo kwenye urais nchi isonge mbele!

I honestly love your way of thinking.
 
Magufuli anafaa, tatizo lipo kwenye kukubali kuwa atalinda maslahi ya wakubwa zake waliotangulia. Hapo jamaa hawamuamini.

Uwezekano wa Magufuli kuwageuka ni mdogo ukilinganisha na uwezekano wa UKAWA kuwafilisi (endapo CCM watamuweka mgombea mwingine atakayesababishia CCM kuanguka).
Upinzani wakichukua nchi ni wazi kabisa makada wote wa ccm waanze kuhamishia nyumbazao na fixed assets nche ya nchi...
So kama CCM ni rational thinkers, watamchagua Magufuli
 
Kutafuta mgombea msafi ndani ya ccm ni sawa kutafuta mwanamke bikra kwenye wodi ya wazazi .
kwenye familia ya majambazi hakuna mwenye afadhali wote ni wezi.

Sijawai kukusikia ukiulizia majibu ya ufisadi wa chadema uliofukuliwa na report ya CAG
 
Uwezekano wa Magufuli kuwageuka ni mdogo ukilinganisha na uwezekano wa UKAWA kuwafilisi (endapo CCM watamuweka mgombea mwingine atakayesababishia CCM kuanguka).
Upinzani wakichukua nchi ni wazi kabisa makada wote wa ccm waanze kuhamishia nyumbazao na fixed assets nche ya nchi...
So kama CCM ni rational thinkers, watamchagua Magufuli

YES! UKAWA sio chaguo sahihi kwa CCM, lakini ukweli kwamba hata kati yao hofu ya kumuweka atakayekuwa ni winning candidate itategemea sana uwezekano wa candidate huyo kuwa mtu anae tabirika hasa kwenye kulinda mali na maisha ya wakubwa waliopo madarakani sasa. Magufuli is a presidential material, but likely unpredictable.
 
Unless wewe ni 'little puppy' umezaliwa juzi hujui nini kinaendelea kwenye siasa za nchi hii...haikuwahi kutokea kwenye historia (toka mwanzo wa vyama vingi) kukawa na chaguzi bila makundi. Lowassa atachinjiwa baharini (kama alivyofanywa kwenye uwaziri mkuu) na hawezi kufanya lolote.

Makundi yalianza 1995 ndio maana Nyerere alipompendekeza Mkapa aliamua kuingia kwenye kampeni mzima mzima, na lile kundi lililoshindwa ndio lililo ingia 2005 na ndilo linautaka uraisi mwaka huu. Believe me Lowasa hazuiliki ingawa sio mimi shabiki wake
 
Mungu amesikia dua zangu na amewaongoza viongozi wangumkufanya maamuzi
 
Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kujaalia kutimia kile nilichokifikiria
 
Makundi yalianza 1995 ndio maana Nyerere alipompendekeza Mkapa aliamua kuingia kwenye kampeni mzima mzima, na lile kundi lililoshindwa ndio lililo ingia 2005 na ndilo linautaka uraisi mwaka huu. Believe me Lowasa hazuiliki ingawa sio mimi shabiki wake
Kazuilika sasa. Waseme kingine
 
Wadau, tumewaona watangaza nia wote na tumewasikia nini wanataraji kukifanya wakipata ridhaa ya kutuongoza Watanzania. Hakika niseme kwa dhati ya moyo wangu kuwa karibu wote waliotangaza nia kwa mbwembwe wamejipalia mkaa kwani wameenda kabisa kinyume na misingi ya chama ambapo wao wamejifanya wakubwa kuliko chama. Pia wengi wao wamo serikalini na chama tawala lakini wamejikuta wakiiponda serikali yao katika mambo ambayo wao ni sehemu ya matatizo.

Binafsi nilikuwa simpi nafasi kabisa John Pombe Magufuli. Si kwa sababu nachukia jina lake la Pombe tu bali ni kwa jinsi alivyo mbali na wafanya maamuzi ndani ya CC, NEC na MM. Kwa ujumla Magufuli yupo mbali sana na politics ndani ya chama. Hali hii inamfanya aonekane kama mtu ambaye hatakuwa na msaada kwa watu ambao wamezoea kujipendekeza ndani ya chama kwa lengo kuwa wanakisaidia kumbe wanataka kupiga deal zao. Hayo tumeyaona kwa Rostam na wengi ambao leo ndio friends of Lowasa.

Kwa nini nasema Magufuli ndio jibu sahihi?

  1. Magufuli hana kashfa kubwa za rushwa na ufisadi ambazo zinaweza kumfanya ashindwe kunadi vema sera ya chama ya kupambana na rushwa na ufisadi. Kwani ni ukweli ulio wazi kwamba ukitaka kupambana na rushwa ipasavyo, wewe mwenyewe unapaswa usiwe sehemu ya wala rushwa au usizungukwe na mchwa ambao wanaweza kuharibu utawala wako. Mengi yanayosemwa kama yale ya uuzwaji wa nyumba za serikali kwa watu wasiohusika na sub standard ya barabara zetu huwezi kumuingiza Magufuli moja kwa moja kwani tumeshuhudia jinsi anavyofukuza makandarasi wabovu kila kukicha
  2. Magufuli hakutangaza nia kabla ya kuchukua fomu. Hali hii imemsaidia kwani angeongea mambo ambayo yangemchanganya yeye na wakati mwingine angeishia kujisifu na kuwachafua wenzake.
  3. Magufuli anatoka kanda ya ziwa ambayo ina wapiga kura wengi sana hapa nchini. Ikiwa Magufuli atateuliwa, kanda ya ziwa watakuwa na imani na chama tawala kwani ni muda mrefu wamekuwa na kilio cha kuwekwa kando inapofika wakati wa kuwapata wagombea ilhali wanaamini kwamba wana majembe mengi yanayoweza kuiongoza vema nchi na chama tawala
  4. Ikiwa Magufuli atateuliwa katika hatua ya tano bora, upo uwezekano wa wagombea wote wa kanda ya ziwa na maeneo mengine kama yamkusini, mashariki na kati kujitoa na kumuunga mkono magufuli hali itakayomsaidia kushinda kwa kishindo kikubwa.
  5. Magufuli amefanya mambo mengi yanayoonekana katika jamii kama vile ujenzi wa nyumba bora na za kisasa pamoja na ujenzi wa barabara. Bahati nzuri ni kwamba barabara hizi zinaonekana kwa macho na wananchi wanazitumia. Kubwa zaidi ni kwamba wananchi wanaona juhudi anazofanya Magufuli kutatuaa changamoto za barabara pale zinapojitokeza. Watu wa mikoa ya kusini hawatamsahau Magufuli jinsi alivyosimamia ujenzi wa kipande korofi kutoka Muhoro hadi Somanga barabara ambayo ndiyo ilikuwa kilio cha muda mrefu. Kwa sasa kwenda Lindi inachukua masaa sita tu tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inachukua siku nzima. Pia tumeona jinsi alivyosimamia kurejesha mawasiliano baada ya narabara kuharibiwa na mvua zilizonyesha Aprili 2014 na hivyo barabara za Morogoro na Bagamoyo kutopitika. Magufuli alikuwa anakesha kuhakikisha barabara zinakamilika ndani ya muda mfupi huku akishirikiana vema na Jeshi la Ulinzi. Ujenzi wa daraja la Kigamboni ni jambo jingine linalomuongezea credit.
  6. Magufuli amejipa muda wa kusoma na kuelewa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2015 hadi 2020. Amesema baada ya kusoma na kuielewa, atawaita waandishi wa habari na kueleza msomamo wake na wa chama chake. Hilo ni bao jingine ambalo amewapiga washindani wake. Wengi walikuwa wanabwabwaja tu bila kuwa na kitendea kazi. Kumbuka Mgombea Urais anawakilisha chama ambacho huandaa Ilani ambayo ndiyo itatumika kuomba kura kwa wananchi. Waswahili wanasema kuwa mkono mtupu haulambwi.
  7. Wakati anaenda kuchukua fomu, Magufuli kaambatana na watu watatu tu akiwemo mbunge wa Nkenge Assumpter Mshama. Hapa pia kawapiga bao wapinzani wake. Wengine wameenda kwa mbwembwe na kuambatana na watu ambao tashwira zao katika jamii ni mbaya. Huwezi kufuatana na watu kama akina Karamagi, Chenge nk then utegemee kupata ushirikiano kwa wananchi.
  8. Magufuli hajawa na shauku ya kuwa Rais wa Tanzania. Ni wananchi na wapenda maendeleo ndio walioona umuhimu wa Magufuli. Tofauti na hawa wengine ambao wanataka kwenda Ikulu kufilisi rasilimali zetu, kulipa fadhila za maswahiba wao na kulipa visadi.
  9. Magufuli si mkurupukaji. Anafanya mambo kwa mujibu wa sheria za nchi. Sote tumeshuhudia jinsi alivyokwaruzana na viongozi wake wa juu katika kusimamia sheria za nchi. Mnakumbuka lile sakata la jengo la TANESCO pale Ubungo? Mnakumbuka sakata la malori kuzidisha uzito kinyume na sheria?
  10. Magufuli hana makundi. Tofauti na hawa wagombea wengine ambao wana kundi ambalo litataka kuona linafaidi kwa kumsaidia mgombea wao. Magufuli hatafungwa na siasa za makundi na hivyo kumfanya awe huru zaidi katika utendaji wake. Pia Magufuli atasaidia kukomesha siasa za makundi kwani wengi wataanza kuona kuwa kumbe mtu anaweza kuwa Rais wa nchi pasi na kuwa namkundi lolote.

Wadau, huu ni msimamo wangu binafsi na sijafungwa na msimamo wowote. Nipo huru kukosolewa na nipo tayari kupokea changamoto zitakazojitokeza kwenye mjadala huu. Narudia kusema kuwa Magufuli ndiye jibu sahihi. Hao wengine hawana vigezo vinavyotakiwa na wananchi. Mtawapa bure UKAWA hoja za kusema kwa wananchi. Nawahakikishia ikiwa Magufuli atateuliwa na chama kugombea, hawa UKAWA hawatasimamisha kabisa mgombea Urais kwani hawana mtu wa hali kama ya Magufuli
😄😄😄👍👍👍
 
Magufuli naaamini ni raisi pekee mwenye sifa kati ya hawa.
Tanzania kuongozwa na hawa wadada ni ngumu

Raisi kikwete akitaka ccm ishuke ikose matarajio yapotee wamuweke mwana mama hapa
 
Back
Top Bottom