Kama Capitalism ni mfumo bora basi akina mama wengi Africa wangekuwa matajiri

mcomunisti halisi

Senior Member
Jan 17, 2017
103
328
Capitalism kama ingekuwa bora kihivyo basi akina mama Africa wengi wangekuwa matajiri lakini kinachosikitisha wanatumia nguvu kubwa kulima na faida wanayoipata ni kiduchu na matajiri ndio wanaofaidika na mazao ya huyu mama anayetumia nguvu kubwa kulima.

Falsafa ya hapa kazi tu haiwezi kuwa applicable kwenye capitalism sababu exploitation ni kubwa mno mtu anatumia nguvu kubwa kuzalisha na mwishoni faida inaenda kwa matajiri na mkulima masikini anaendelea kubaki kuwa forced labour.

Kunatakiwa kuwe na mfumo imara ambayo italeta haki na usawa baina ya watu na kupunguza gap kati ya high income earners na low income earners kama capitalism ni mfumo bora mbona Africa na South America hakuna maendeleo ,

Zawadi ya nguvu na kazi "hapa kazi tu" katika capitalism mbona hatuioni kwa wakulima na wengi katika watu wengine wanaozalisha kwenye jamii

61afb0ee85cd2ba76dbdb0f5e2a275dc.jpg
 
Mkuu umepinga capitalism ila sijaona mfumo uliyopendekeza kama mbadala wake.

Au nijiongeze kwa avatar? Elezea mfumo unaohisi ni bora ndiyo wengine tuweze kukujibu maana mada haijakamilika.
 
  • Thanks
Reactions: t2t
umechanganya mifumo

capitalism ni mfumo ambao mtaji (mkwanja) ndio msingi w uzalishaji huku kukiwa na matabaka kati ya walio nacho na wasio nacho

walio nacho ndo hao matajiri ambao wananunua mazaa ya wamama kijijini ambao hawana kitu (naweza sema wako kwenye mfumo wa feudalism ambao ardhi ndo msingi wa uzalishaji)

kifupi falsafa ya hapa kazi tu itafanikiwa kama serikali itajitahidi kuweka mazingira rahisi kwa watu wa chini (hao kina mama) ili kuwawezesha kufikisha mazao yao sokoni na kupewa mikopo rahisi kuwezesha kilimo
 
Capitalism ina mapungufu yake lakini bado unabaki kuwa mfumo bora wa uchumi duniani. Africa ni maskini kwasababu ya ujinga, vita, maradhi. Sio capitalism. South America nchi yenye uchumi mbovu zaidi ni Venezuela ambao ni socialist sio capitalist. Angalia nchi zenye uchumi mkubwa duniani karibu zote ni capitalist. Marekani, south korea, japan, canada na nchi za ulaya. Hata wewe umepinga capitalism bila kuweka mbadala kwasababu unajua hakuna mbadala
 
Ubepari ni mfumo wa uchumi ambapo uzalishaji unafanyika kwa kutumia mtaji(capital) ili kupata faida kubwa. Hawa akina mama maskini ambao nguvu zao ndio mtaji wao hawawezi kuitwa mabepari
 
Back
Top Bottom